Ghost voters walimsaidia Ruto kuingia Ikulu

Kindus

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2014
Posts
3,384
Reaction score
2,073
Najua wengi mnakumbuka kura za maruhani kule Pemba zilivyoishangaza nchi yetu sasa ukistajabu ya Pemba ambapo maruhani walizaliwa baada ya kutokuwa na wagombea wa CUF ujayaona ya Nairobi.

Ghost voters (kura za mizimu) ndizo zilizomnufaisha rais Rutto ambapo zinakadiriwa kuwa zaidi ya 500k sawa na 3.5% ya kura zote.

Najua mtajiuliza kuwa mizimu ilipigaje kura. Lakini, pia mwahitajika kujiuliza kwa vipi maruhani walipiga kura kule Pemba.

Wote mkinyamaza mawe yataongea.

Kipo cha kujifunza hapa kwa wana CCM wenzangu ipo siku mizimu itafufuka kuja kututoa madarakani hata kama tunatumia udhaifu wa Watanzania kujisimika mamlakani ipo siku itafika tutatolewa.
 
Acha uongo ww
 
Mkuu kuandika uzi wenye tuhuma kubwa namna hii pasipo kuwa na chanzo chenye kuthibitisha madai hayo, inakuwa ni uzushi kama mwingine uwao wowote ule.
 
Uchaguzi umeshakamilika

Waacheni Wakenya wajenge nchi yao
 
Kabisa kabisa kabisa
 
I like the way tanzanians follow up Kenya news.
Following closely like its their birthright. Tatizo ni kwamba wengi wao(akiwemo mleta mada) hawana idea kabisa, kuhusu wanayoyafatilia na kuyajadili kwa ushabik mkubwa.

Jamaa anadhani kwamba Kenya bado tupo kwenye enzi za ule ushamba wa kufanya uchaguzi manual kama wao. Tangia uchaguzi wa 2013 wakenya wamekuwa wakipiga na kusajiliwa kupiga kura 'biometrically'. Kumaanisha kwamba kabla ukubaliwe kupiga kura lazima mashine za KIEMS Kit zisome 'biometrics' zako(fingerprints) kwanza, ili kuhakikisha kwamba wewe ni mpiga kura halali.

Sasa sijui jamaa anamaanishaje, kwamba baadhi ya wapiga kura walifika kwenye vituo na viganja vya mikono ya wafu au vipi?
 
Utawala wa kikuyu na kalenjin. Ni hizo kabila mbili tu tangu uhuru. Tofauti na Tanzania ni kubwa sana ujue, wewe nyang'au. Bado mnaendeleza mambo ya kishamba sana.
 
Wakenya wangese kweli aisee unaweza kukaa nae mnaongea Kiswahili fresh tu. Akitokea mtu wa kabila yake wataanza kuongea kiluga chao.
 
Kindly read my comment kule juu, Kaka watz we know everything about Kenya trust me hatuandiki tu and mark my words, by 2035 Tanzania will be the largest economy in East Africa ngojeni SGR ikamilike, Nyerere Dam ikamilike na Bagamoyo Harbour zikamilike mtakuja tz kufanya vibarua!

Bado tz tupate Rais afanye English as teaching language from elementary level basi wakenya hamtaweza tena kusogelea tz!

si umeona tumewafurusha wakenya kule Ngorongoro tukachukua mifugo zenyu? how did we know?
 
Upuuzi, kwamba Kenya ndio imekuwa ikiwakwaza kufikia malengo yenu kwa miaka yote hiyo tangia mpate uhuru? Au kwamba ili myatimize ni lazima wakenya wasifanikiwe kutimiza malengo yao? Hauleweki kabisa, hakuna nchi ambayo haina mipango ya kujiendeleza, hataY Somalia na Burundi pia.

Nchi ya Kenya inafanya mambo yake, ikiwa ni pamoja na kutimiza vipengele vya ruwaza ya Kenya 2030. Bila kuitizama nchi yeyote ile nyingine, masuala yenu hayawahusu wakenya wala Kenya haina deni lenu, hata la shilingi moja.
 
Wakenya wangese kweli aisee unaweza kukaa nae mnaongea Kiswahili fresh tu. Akitokea mtu wa kabila yake wataanza kuongea kiluga chao.
Sidhani kwamba ni kweli
 
Utawala wa kikuyu na kalenjin. Ni hizo kabila mbili tu tangu uhuru. Tofauti na Tanzania ni kubwa sana ujue, wewe nyang'au. Bado mnaendeleza mambo ya kishamba sana.

So you want to say that Kenya is behind tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…