Giants Simba Sc kuanzia round ya kwanza CAFCL

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
-Klabu ya Simba SC ya Tanzania sasa rasmi imekuwa miongoni mwa vilabu 10 ambavyo vitaanzia raundi ya kwanza kwenye mashindano ya CAF Champion League msimu 2022/23 kama msimu uliopita baada ya CAF kupitisha utaratibu wa vilabu 10 bora kuanzia raundi ya kwanza ya michuano ya CAF Champion League.

-Ubora wa vilabu kwa sasa Simba ipo nafasi ya 14 kama ifuatavyo (Al Ahly (01) ya Misri, Wydad (02) ya Morocco, Esperance (03) ya Tunisia, Raja (04) ya Morocco, RS Berkane (05) ya Morocco, Mamelodi (06) ya Afrika Kusini, Mazembe (07) ya DRC, Zamelek (08) ya Misri, Pyramids (09) ya Misri, Etoile (10) ya Tunisia, Orando (11) ya Afrika kusini, Horoya (12) ya Guinea, Petro de Luanda (13) ya Angola) na Simba SC (14) ya Tanzania

-Kwa Misri inatakiwa vilabu 2 kati ya vitatu (Al Ahly, Zamalek, Pyramids) kushiriki CAF Champion League, Morocco timu ya Berkane ameshindwa kufuzu kucheza CAF Champion League, Orlando naye hajafuzu kucheza Caf Champion League, Tunisia, Etoile Sahel hawezi kuzifikia pointi za Monastri ambayo ilimfunga jana kwa magoli 2-0. Hivyo timu 14 - 4 =10 ndio Simba imefaidika kuwa miongoni mwa vilabu 10 ambavyo vitaanzia raundi ya kwanza.

-Kwa mujibu wa kalenda ya CAF ratiba inaonesha raundi ya awali ya mashindano ya CAF (Caf Champion League na Caf Confederation Cup) yataanza August 12-14 kwa michezo ya mkondo wa kwanza na August 19-21 michezo ya mkondo wa pili. Wakati raundi ya kwanza imepangwa kuanza September 9-11 kwa michezo ya mkondo wa kwanza na September 16-18 michezo ya mkondo wa pili.
 
Hivi mfano Al Ahly angebeba kombe la klabu bingwa halafu kwenye ligi yao aahike nafasi ya tatu ingekuwaje? Misri wangeingiza timu tatu klabu bingwa au ingekuwaje?
 
Hivi mfano Al Ahly angebeba kombe la klabu bingwa halafu kwenye ligi yao aahike nafasi ya tatu ingekuwaje? Misri wangeingiza timu tatu klabu bingwa au ingekuwaje?
asingeshiriki,ni kama ilivyo hao wengine wapo juu lakini hawashiriki.
 
Nguvu moja..💪💪💪
 
Simba SC waamke, kwa huu mwenendo wao siku sio nyingi watashuka zaidi.
 
Mkuu OKW BOBAN SUNZU hapo kwenye list yako ya timu zilizofuzu kucheza champion league naona umeiweka na berkane ambayo umesema kuwa haishiriki champion league
 
Mkuu OKW BOBAN SUNZU hapo kwenye list yako ya timu zilizofuzu kucheza champion league naona umeiweka na berkane ambayo umesema kuwa haishiriki champion league
Mkuu Scars unarejea list ipi? List ya mwanzo ni timu 14 bora na Berkane ikiwa na nafasi ya 5. Aya ya 3 nikaonyesha Berkane ameshindwa kufuzu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…