Gigy Money asoma Quran, aomba Dua kwa Jamii: "Sisi bila wewe si lolote si chochote Mungu wangu"

Gigy Money asoma Quran, aomba Dua kwa Jamii: "Sisi bila wewe si lolote si chochote Mungu wangu"

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Msanii wa muziki na burudani nchini, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, ameamsha hisia za wengi mtandaoni baada ya kujirekodi akisoma Sura ya Quran na kuomba dua maalum asubuhi ya leo ya Ijumaa,.

Kupitia video iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, msanii huyo alionekana akianza kwa kusoma Aya za Quran kabla ya kuendelea na maombi kwa sauti, akilenga kuwatakia baraka na amani mashabiki na jamii kwa ujumla,.

Gigy Money alieleza kuwa nia yake kuu katika kuomba dua hiyo ilikuwa ni kuwa chachu ya baraka kwa vijana wenzake na jamii inayomzunguka badala ya kuwa kikwazo cha mafanikio.

Alimuomba Mwenyezi Mungu kuwafungulia riziki waliokwama, kuwaponya wagonjwa, na kuondoa migogoro ya kifamilia, vinyongo na ugomvi wa ndoa uliopo kwenye nyumba za watu mbalimbali,,.

Akiomba kwa hisia kali, msanii huyo alisikika akisema:

"Leo naomba niwe chachu ya kubariki wengine. Mwenyezi Mungu awabariki, waone huruma sisi... bila wewe si lolote si chochote Mungu wangu. Sisi bila wewe hatuna kauli". Gigy Money alihitimisha ujumbe huo kwa kutoa wito wa amani na kuwatakia waumini wote wa Dini ya Kiislamu Ijumaa Mubaraka.


​
 
Back
Top Bottom