Amalrik TZ
JF-Expert Member
- Aug 9, 2020
- 341
- 303
Wote tunaona namna mambo yanavyoenda hovyo sana katika kampeni za mwaka huu. Kampeni hizi hazina uhuru wala usawa kwa vyama vyote.
Vyombo vya habari vimekuwa vikitangaza habari ya chama tawala pekee huku Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC, ikiegemea upande mmoja wa chama tawala na kuvikandamiza Vyama vya Upinzani.
Ni leo hii tarehe 28/9 tumeshuhudia mgombea Urais wa CHADEMA Tundu Lissu msafara wake ukipigwa mabomu ya machozi huku Polisi wakizuia njia huko Nyamongo Wilaya ya Tarime. Mhe. Tundu Lissu amesikika akisema
“Kama una malalamiko peleka tume ya uchaguzi, sheria inasema kama una malalamiko unakwenda kwenye tume ya maadili sio unapiga watu mabomu,sasa wewe amua tulale hapa au unipige mabomu au unipige risasi”
Hatua ya kwanza kabisa ya uchaguzi ya kuteua wagombea kwenye tume ya uchaguzi ilijawa na mizingwe mingi. Haiwezekani wagombea wa chama tawala tuu ndio wapite bila kupingwa huku wa vyama vya upinzani wakitupwa nje ya kinyang’anyiro.
Haiwezekani mgombea ambaye alishawahi kuwa Mbunge na kushiriki vikao vya Bunge ashindwe kujua taratibu na namna ya kujaza fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge kwa usahihi.
Ndio, mapungufu ya kibinadamu yapo lakini kwanini yawe kwa wagombea wa CHADEMA na ACT Wazalendo tuu na si kwa chama tawala?
Siwezi kuamini wala haiingi akilini mwangu kamwe mtu kama Susan Limbweni kiwanga Mbunge wa jimbo la Mlimba (2015-2020) na Mbunge wa viti maalumu toka mwaka(2010-2015) ashindwe kujaza fomu kwa ufasaha.
Hapana! kuna sehemu haiko sawa, na nadhani wote tumeona namna wagombea wa vyama vya upinzani wakienguliwa pasipokuwa na hoja za msingi.
Ukweli ni kwamba chama tawala kimetumia mapungufu yaliyopo kwenye Katiba kuteua makada wake kuwa watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, huku wakinadi amani kwenye majukwaa ya siasa.
Tatizo kuu linaanzia kwenye Tume ya Taifa yaUchaguzi. Tume hii sio huru na haitendi haki kwa vyama vyote. Nasema kama sio huru kwa sababu tunaona namna inavyopendelea chama tawala na kuwakandamiza wapinzani.
Matendo ambayo wanafanyiwa watanzania wenzetu waliopo nje ya CCM yanaumiza sana moyo, huku kila siku wafanyakazi wa NEC wakizidi kuonyesha namna ndoa yao na chama tawala ilivyohai na tamu.
Hali hii inaashiria kwamba NEC na chama tawala wana nia ya kuviua vyama vya upinzania nchini Tanzania.
Kwa mfano Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, aliposema hadhari “watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hataki bla! Blah!”
Mkurugenzi huyo aliyasema hayo alipokuwa anazungumnzia kumuandikia barua mgombea Urais wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu ili kutoa maelezo dhidi ya tuhuma za uongo na kukashfu wagombea wenzake.
Binafsi najiuliza toka lini Refa akawa Kocha kwa wakati mmoja uwanjani kwa maana anachokifanya Mkurugenzi ni kampeni.
Ninachoshangaa zaidi ni namna Tume ya Uchaguzi kama Refa huru imegeuka waziwazi na kuvitaka vyama viwe na sera za namna gani katika uchaguzi huu.
Mambo haya yanaleta GIZA kwenye demokrasia na uchaguzi huu umetandwa na giza nene.
Watanzania tulio wengi hatuamini tena kama hii tume inaweza kusimamia na kutetea demokrasia katika nchi yetu.
Inatia uchungu sana na kuumiza kuona namna nchi hii inavyoendeshwa bila usawa. Binafsi najiulizaga sana haya yanayoendelea katika hii nchi ndiyo matunda ya Baba wa taifa kupigania UHURU?
Hatuwezi kusema nchi hii ni huru wakati katika nchi moja kuna watu wanaoishi peponi na wengine wanaishi jehanamu. Nchi hihi kuna watanzania wanateseka na kunyimwa haki zao hadharani alafu wapo ambao wanafurahia maisha.
Nadhani maana ya uhuru katika nchi hii inapotea kwa kasi, kwasababu matendo ambayo wakoloni walikuwa wanawafanyia wazee wetu ndiyo hayo hayo ambayo sasa sisi wenyewe tunafanyiana bila hata ya woga. Inasikitisha sana!
Pamoja na mambo hayo yote ya kusikitisha na kuvunja moyo kuendelea kutokea nchini, bado naamini nguvu ipo mikonomi mwa watanzania na tukihitaji uhuru wa kweli tutaupata.
Ngugu zangu naomba mukumbuke kuwa haki haiombwi haki inapiganiwa.
Nadhani kila mmoja wetu anakubali kwamba matatizo mengi yameletwa na Katiba iliyopo. Uchaguzi huu kama zilivyokuwa chaguzi zilizopita umeonyesha dhahiri umuhimu wa katiba mpya.
Tanzania inahitaji katiba mpya hii ndio dawa ambayo itaweza kutenganisha serikali pamoja na chama tawala. Taifa likiendelea na katiba hii hata siku ikatokea CCM ni chama cha upinzani nacho kitalalamika sana. Tunahitaji Katiba ambayo itaondoa malalamiko kwa vyama vyote.
Nchi hii ni yetu sote na lazima tupiganie maendeleo ya watu wote bila kujali dini, rangi ya ngozi wala kabila. Watanzania yatupa sana tuungane kwa pamoja kukemea uovu hata kama Katiba yetu inamapungufu tusikubali wenye mamlaka kufanya kinyume na katiba.
Itoshe kusema kwamba tarehe 28 Oktoba usikose kwenda kupiga kura kwani kura yako moja italeta mabadiliko makubwa sana katika kile unachokiamini pamoja na nchi yetu.