Uchaguzi 2020 Giza nene lazidi kutanda Uchaguzi Mkuu 2020

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2020
Posts
341
Reaction score
303
Wote tunaona namna mambo yanavyoenda hovyo sana katika kampeni za mwaka huu. Kampeni hizi hazina uhuru wala usawa kwa vyama vyote.

Vyombo vya habari vimekuwa vikitangaza habari ya chama tawala pekee huku Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC, ikiegemea upande mmoja wa chama tawala na kuvikandamiza Vyama vya Upinzani.

Ni leo hii tarehe 28/9 tumeshuhudia mgombea Urais wa CHADEMA Tundu Lissu msafara wake ukipigwa mabomu ya machozi huku Polisi wakizuia njia huko Nyamongo Wilaya ya Tarime. Mhe. Tundu Lissu amesikika akisema

“Kama una malalamiko peleka tume ya uchaguzi, sheria inasema kama una malalamiko unakwenda kwenye tume ya maadili sio unapiga watu mabomu,sasa wewe amua tulale hapa au unipige mabomu au unipige risasi”

Hatua ya kwanza kabisa ya uchaguzi ya kuteua wagombea kwenye tume ya uchaguzi ilijawa na mizingwe mingi. Haiwezekani wagombea wa chama tawala tuu ndio wapite bila kupingwa huku wa vyama vya upinzani wakitupwa nje ya kinyang’anyiro.

Haiwezekani mgombea ambaye alishawahi kuwa Mbunge na kushiriki vikao vya Bunge ashindwe kujua taratibu na namna ya kujaza fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge kwa usahihi.

Ndio, mapungufu ya kibinadamu yapo lakini kwanini yawe kwa wagombea wa CHADEMA na ACT Wazalendo tuu na si kwa chama tawala?

Siwezi kuamini wala haiingi akilini mwangu kamwe mtu kama Susan Limbweni kiwanga Mbunge wa jimbo la Mlimba (2015-2020) na Mbunge wa viti maalumu toka mwaka(2010-2015) ashindwe kujaza fomu kwa ufasaha.

Hapana! kuna sehemu haiko sawa, na nadhani wote tumeona namna wagombea wa vyama vya upinzani wakienguliwa pasipokuwa na hoja za msingi.

Ukweli ni kwamba chama tawala kimetumia mapungufu yaliyopo kwenye Katiba kuteua makada wake kuwa watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, huku wakinadi amani kwenye majukwaa ya siasa.

Tatizo kuu linaanzia kwenye Tume ya Taifa yaUchaguzi. Tume hii sio huru na haitendi haki kwa vyama vyote. Nasema kama sio huru kwa sababu tunaona namna inavyopendelea chama tawala na kuwakandamiza wapinzani.

Matendo ambayo wanafanyiwa watanzania wenzetu waliopo nje ya CCM yanaumiza sana moyo, huku kila siku wafanyakazi wa NEC wakizidi kuonyesha namna ndoa yao na chama tawala ilivyohai na tamu.
Hali hii inaashiria kwamba NEC na chama tawala wana nia ya kuviua vyama vya upinzania nchini Tanzania.

Kwa mfano Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, aliposema hadhari “watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hataki bla! Blah!”
Mkurugenzi huyo aliyasema hayo alipokuwa anazungumnzia kumuandikia barua mgombea Urais wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu ili kutoa maelezo dhidi ya tuhuma za uongo na kukashfu wagombea wenzake.

Binafsi najiuliza toka lini Refa akawa Kocha kwa wakati mmoja uwanjani kwa maana anachokifanya Mkurugenzi ni kampeni.

Ninachoshangaa zaidi ni namna Tume ya Uchaguzi kama Refa huru imegeuka waziwazi na kuvitaka vyama viwe na sera za namna gani katika uchaguzi huu.

Mambo haya yanaleta GIZA kwenye demokrasia na uchaguzi huu umetandwa na giza nene.
Watanzania tulio wengi hatuamini tena kama hii tume inaweza kusimamia na kutetea demokrasia katika nchi yetu.

Inatia uchungu sana na kuumiza kuona namna nchi hii inavyoendeshwa bila usawa. Binafsi najiulizaga sana haya yanayoendelea katika hii nchi ndiyo matunda ya Baba wa taifa kupigania UHURU?

Hatuwezi kusema nchi hii ni huru wakati katika nchi moja kuna watu wanaoishi peponi na wengine wanaishi jehanamu. Nchi hihi kuna watanzania wanateseka na kunyimwa haki zao hadharani alafu wapo ambao wanafurahia maisha.

Nadhani maana ya uhuru katika nchi hii inapotea kwa kasi, kwasababu matendo ambayo wakoloni walikuwa wanawafanyia wazee wetu ndiyo hayo hayo ambayo sasa sisi wenyewe tunafanyiana bila hata ya woga. Inasikitisha sana!

Pamoja na mambo hayo yote ya kusikitisha na kuvunja moyo kuendelea kutokea nchini, bado naamini nguvu ipo mikonomi mwa watanzania na tukihitaji uhuru wa kweli tutaupata.
Ngugu zangu naomba mukumbuke kuwa haki haiombwi haki inapiganiwa.

Nadhani kila mmoja wetu anakubali kwamba matatizo mengi yameletwa na Katiba iliyopo. Uchaguzi huu kama zilivyokuwa chaguzi zilizopita umeonyesha dhahiri umuhimu wa katiba mpya.

Tanzania inahitaji katiba mpya hii ndio dawa ambayo itaweza kutenganisha serikali pamoja na chama tawala. Taifa likiendelea na katiba hii hata siku ikatokea CCM ni chama cha upinzani nacho kitalalamika sana. Tunahitaji Katiba ambayo itaondoa malalamiko kwa vyama vyote.

Nchi hii ni yetu sote na lazima tupiganie maendeleo ya watu wote bila kujali dini, rangi ya ngozi wala kabila. Watanzania yatupa sana tuungane kwa pamoja kukemea uovu hata kama Katiba yetu inamapungufu tusikubali wenye mamlaka kufanya kinyume na katiba.

Itoshe kusema kwamba tarehe 28 Oktoba usikose kwenda kupiga kura kwani kura yako moja italeta mabadiliko makubwa sana katika kile unachokiamini pamoja na nchi yetu.
 
Mimi naamini tunapaswa kufanya zaidi ya kupiga kura tu. Ni wazi wazi kabisa sasa kuwa NEC wanaitafutia CCM ushindi wa hila. Nawaambia watanzania tusipoingia mtaani kwa maandamano makubwa hakuna haki yoyote tutakayopata. Tushinikize tume huru isiyoteuliwa na rais.
 
MWAKA HUU 2020 TANZANIA JAMBO LIPO
Salaaam Wana Forum wote.
Mwaka huu, Watanzania Bara na Zanzibar Tunajambo letu Adhimu
2020 ni mwaka teule wa matukio yasiyo na kifani kwa taifa hili la Muungano wa nchi mbili Kubwa na Ndogo.

Tuna kila sababu ya kuikataa CCM chama kikongwe kilichozeeka na kilichoijisahau kuwa kimepewa dhamana ya kuwalinda na kuwaletea watanzania :- maendeleo ,uhuru na Haki blia ya kuwa bagua au kuwakejeli.tuliyakosa hayo zama za mkoloni na tukaanza kutafuta UHURU wa nchi zetu .

Ikiwa UHURU unakosekana tena chini ya CCM ,shughuli ya kujikomboa UPYA japo kwa njia tofauti kwa vile Ndugu zetu wametugeuka na kuacha wajibu wao na kuwa WAKOLONI.

CCM imelewa Madaraka na kujifanya Mungu mtu. Wametugeuza Watanzania kama tambala la kupigia deki. Ikifika wakati wa Uchaguzi wanatudanganya na kisha kutufanyia kiini macho cha Demokrasia wakituaminisha tumeshindwa kwa haki katika sanduku la kura.\
Kwa hiyo mwaka huu
IMA FA IMMA

#1:Sisi Wahitimu tulionyimwa ajira kwenye Utumishi wa Umma ama kutotengenezewa uwezekano wa kuajiriwa kwenye taasisi na mashirika binafsi TUNA JAMBO LETU, October 28.

#2:Sisi Tuliopata Majanga ya tetemeko ya Ardhi na mafuriko tukadhihakiwa na kuliwa michango na misaada yetu TUNA JAMBO LETU, October 28.

#3:Sisi Ndugu, jamaa na marafiki wa wenzetu waliopotezwa, kushambuliwa,kutekwa na kuumizwa katika mazingira yenye ushahidi na tatanishi TUNA JAMBO LETU, October 28.

#4:Sisi vilaza wa Science, tuliokuwa tunasoma Ualimu chuo kikuu cha Dodoma, tukapotezewa muda na kufukuzwa kama mbwa as if tulijichagua TUNA JAMBO LETU, October 28.

#5:Sisi Waajiriwa wa toka 2014 na hatujapata NYONGEZA ya mishahara wala kupanda madaraja (Promotion) Pasi na sababu za msingi pia TUNA JAMBO LETU, October 28.

#6:Sisi Wakulima wa korosho wa mikoa ya Kusini tulioletewa jeshi kulazimishwa kuuza korosho zetu na kutishiwa mama zetu na shangazi zetu kuvunjwa viuno, ndo kwanza TUNA JAMBO LETU, October 28.

#7;Sisi Wandishi wa Habari na vyombo vyetu tunaopangiwa cha kutangaza, kulazimishwa kuimba sifa tupu, kucheka tunapolia, kufungiwa na kutozwa faini kwa kuripoti ukweli halisi wa mambo, pia TUNA JAMBO LETU, October 28.

#8:Sisi tuliobambikiwa kesi hatari kama Ughaidi, Uhujumu uchumi, Uchochezi na kutozwa faini ama kulazimishwa kukiri tusichofanya TUNA JAMBO LETU, October 28.#9:Sisi tuliotimuliwa kama mbwa kwa kuitwa Watumishi Hewa na wenye vyeti fake pia pia TUNA JAMBO LETU, October 28.

#10:Sisi Wazanzibar tulioletewa mteule wa Watanganyika, kwa uteuzi fake uliofanyika Dodoma, tukapewa pandikizi, naomba tuelewane TUNA JAMBO LETU, October 28.

#11:Sisi tuliopewa jukumu la kufanya Ukatili uliopitiliza kwa Watanzania wenzetu, tukipakwa damu isiyo na hatia na kubandikiziwa majina ya ' Watu Wasiojulikana' tumechoka kupewa maagizo ya Kijuha, TUNA JAMBO LETU, October 28.

#12: Sisi Wahitimu wenye mikopo HESLB tunaolipa mkopo wetu wa elimu ya juu kila mwezi na kila mwaka tena kwa makato makubwa sana lakini badala ya deni letu kupungua ndio kwanza linaendelea kuongezeka, tunadhubutu kusema TUNA JAMBO LETU, October 28 pia.

#13:Sisi Wafugaji tunaokamatiwa mifugo na kuuawa, kufungwa na kutaifishwa mifugo yetu kwa kigezo cha kwamba mifugo imeingia kwenye hifadhi, basi nasi TUNA JAMBO LETU, October 28.

#14: Sisi wakulima wa kahawa wa Kagera, Pamba kanda ya ziwa na wakulima wengine tunaopangiwa nani tumuuzie mazao yetu kwa bei isiyoendana na gharama ya uzalishaji, tena kwa mkopo, mjueni kabisa kwamba nasi TUNA JAMBO LETU, October 28.

#15:Sisi tuliokuwa tunataka kupata katiba mpya inayotokana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Judge Joseph Sinde Warioba, ikachakachuliwa na mwisho wa siku kutupwa kwenye dustbin TUNA JAMBO LETU, October 28.

#16:Sisi Watoto wa kike tuliopo kwenye mazingira magumu ya kusoma, tukabakwa na wengine kuhadaiwa lakini tukaambiwa tusirudi shule baada ya masaibu yaliyotukumba, Pia TUNA JAMBO LETU, October 28.

#17:Sisi Watanzania tuliokuwa tunapenda kulifuatilia BungeLive, kujua michango ya wawakilishi wetu na namna wanavyotuwakilisha vema hatuchoki, TUNA JAMBO LETU, October 28.

#18:Sisi wengine tusiopenda namna Chombo chetu cha Utoaji Haki (Mahakama) inavyoingiliwa na serikali katika maamuzi yake, ni wazi na Sisi TUNA JAMBO LETU, October 28

#19:Sisi Watanzania tuliochukizwa na namna C. A. G alivyoondolewa kihorera kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu hatupo kimya. Tunatambua mchango wa Prof. Mussa Assad na utumishi wake kwenye Ukaguzi na udhibiti wa Hesabu za serikali. Kwa hali hiyo tunaomba kuwa wazi, TUNA JAMBO LETU, October 28.

#20:Sisi tunaoishi maisha duni, tusiokunywa maji safi, kuzifikia flyovers, tusiopanda ndege, tunaotozwa gharama kubwa mapokezi kabla ya matibabu, tunaokosa vitanda mahospitalini na kupata elimu bure isiyo na misingi imara tumestukaaa, TUNA JAMBO

#21:Sisi waTanzania tuliovunjiwa majumba yetu na serikali bila ya kupewa fidia wala viwanja mbadala wala pole TUNA JAMBO LETU.October 28.

#22: Sisi Tunaotaka katiba Mpya baada ya maoni yetu ya tume ya warioba kufigiswa na Wana CCM kisha tukazimwa kiaina TUNA JAMBO LETU.October 28.
#23; Sisi Wafanya Biashara na waatu wa kawaida tuliingizwa kwenye hali ngumu za kimaisha na uchumi kwa kuharibiwa mzunguko wa fedha nchini TUNA JAMBO LETU.October 28.

Na wengine wengi mfanowetu walioathirika kwa namna moja au nyingine na Utawala huu wa CCM Tuna sema TUNA JAMBO LETU.October 28.

***********************​
 
Nongwa ilianza pale NEC ilipobariki kuengukiwa kwa wagombea zaidi ya 1500 wa upinzani ila hata wa mmoja wa dawa wa CCM kukutwa na zahma hiyo hakuna!!

Sasa mtu unajiuliza kama mazingira ya wagombea ni yaleyale, elimu ni ile ile, uelewa wao ni ule ule...iweje hawa 1500 wakosee kujaza form ilihali wenzao wa chama tawala wote wapatie..!!

Unajua hata kama ni kufanya fitna na figisu ni sawa ila fanya za kisomi kidogo kuficha aibu!!
 
Akuna giza kuna nuru inayong'aa pasi na shaka.
Watanzania wanasubiri kwa shauku kubwa kuapishwa kwa JPM.
Mpaka sasa kampeni zinaenda kwa weredi na amani iliyojaa.pamoja na kuwepo kwa maneno ya chuki na uvunjifu wa amani kutoka kwa Lissu lakini bado watanzania wanampuuza wanasubiri hiyo siku wamnyooshe mguu unyooke kwenye sanduku la kura.
 
Utashangaa kuna mtu atakupingaa. sijui wanalipwa shilingi ngap? na kwa muda gan! kuwa fanya kuwa wadhambi namna hiyo
 
MWAKA HUU 2020 TANZANIA JAMBO LIPO
Salaaam Wana Forum wote.
Mwaka huu, Watanzania Bara na Zanzibar Tunajambo letu Adhimu
2020 ni mwaka teule wa matukio yasiyo na kifani kwa taifa hili la Muungano wa nchi mbili Kubwa na Ndogo.

Tuna kila sababu ya kuikataa CCM chama kikongwe kilichozeeka na kilichoijisahau kuwa kimepewa dhamana ya kuwalinda na kuwaletea watanzania :- maendeleo ,uhuru na Haki blia ya kuwa bagua au kuwakejeli.tuliyakosa hayo zama za mkoloni na tukaanza kutafuta UHURU wa nchi zetu .

Ikiwa UHURU unakosekana tena chini ya CCM ,shughuli ya kujikomboa UPYA japo kwa njia tofauti kwa vile Ndugu zetu wametugeuka na kuacha wajibu wao na kuwa WAKOLONI.

CCM imelewa Madaraka na kujifanya Mungu mtu. Wametugeuza Watanzania kama tambala la kupigia deki. Ikifika wakati wa Uchaguzi wanatudanganya na kisha kutufanyia kiini macho cha Demokrasia wakituaminisha tumeshindwa kwa haki katika sanduku la kura.\
Kwa hiyo mwaka huu
IMA FA IMMA

#1:Sisi Wahitimu tulionyimwa ajira kwenye Utumishi wa Umma ama kutotengenezewa uwezekano wa kuajiriwa kwenye taasisi na mashirika binafsi TUNA JAMBO LETU, October 28.

#2:Sisi Tuliopata Majanga ya tetemeko ya Ardhi na mafuriko tukadhihakiwa na kuliwa michango na misaada yetu TUNA JAMBO LETU, October 28.

#3:Sisi Ndugu, jamaa na marafiki wa wenzetu waliopotezwa, kushambuliwa,kutekwa na kuumizwa katika mazingira yenye ushahidi na tatanishi TUNA JAMBO LETU, October 28.

#4:Sisi vilaza wa Science, tuliokuwa tunasoma Ualimu chuo kikuu cha Dodoma, tukapotezewa muda na kufukuzwa kama mbwa as if tulijichagua TUNA JAMBO LETU, October 28.

#5:Sisi Waajiriwa wa toka 2014 na hatujapata NYONGEZA ya mishahara wala kupanda madaraja (Promotion) Pasi na sababu za msingi pia TUNA JAMBO LETU, October 28.

#6:Sisi Wakulima wa korosho wa mikoa ya Kusini tulioletewa jeshi kulazimishwa kuuza korosho zetu na kutishiwa mama zetu na shangazi zetu kuvunjwa viuno, ndo kwanza TUNA JAMBO LETU, October 28.

#7;Sisi Wandishi wa Habari na vyombo vyetu tunaopangiwa cha kutangaza, kulazimishwa kuimba sifa tupu, kucheka tunapolia, kufungiwa na kutozwa faini kwa kuripoti ukweli halisi wa mambo, pia TUNA JAMBO LETU, October 28.

#8:Sisi tuliobambikiwa kesi hatari kama Ughaidi, Uhujumu uchumi, Uchochezi na kutozwa faini ama kulazimishwa kukiri tusichofanya TUNA JAMBO LETU, October 28.#9:Sisi tuliotimuliwa kama mbwa kwa kuitwa Watumishi Hewa na wenye vyeti fake pia pia TUNA JAMBO LETU, October 28.

#10:Sisi Wazanzibar tulioletewa mteule wa Watanganyika, kwa uteuzi fake uliofanyika Dodoma, tukapewa pandikizi, naomba tuelewane TUNA JAMBO LETU, October 28.

#11:Sisi tuliopewa jukumu la kufanya Ukatili uliopitiliza kwa Watanzania wenzetu, tukipakwa damu isiyo na hatia na kubandikiziwa majina ya ' Watu Wasiojulikana' tumechoka kupewa maagizo ya Kijuha, TUNA JAMBO LETU, October 28.

#12: Sisi Wahitimu wenye mikopo HESLB tunaolipa mkopo wetu wa elimu ya juu kila mwezi na kila mwaka tena kwa makato makubwa sana lakini badala ya deni letu kupungua ndio kwanza linaendelea kuongezeka, tunadhubutu kusema TUNA JAMBO LETU, October 28 pia.

#13:Sisi Wafugaji tunaokamatiwa mifugo na kuuawa, kufungwa na kutaifishwa mifugo yetu kwa kigezo cha kwamba mifugo imeingia kwenye hifadhi, basi nasi TUNA JAMBO LETU, October 28.

#14: Sisi wakulima wa kahawa wa Kagera, Pamba kanda ya ziwa na wakulima wengine tunaopangiwa nani tumuuzie mazao yetu kwa bei isiyoendana na gharama ya uzalishaji, tena kwa mkopo, mjueni kabisa kwamba nasi TUNA JAMBO LETU, October 28.

#15:Sisi tuliokuwa tunataka kupata katiba mpya inayotokana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Judge Joseph Sinde Warioba, ikachakachuliwa na mwisho wa siku kutupwa kwenye dustbin TUNA JAMBO LETU, October 28.

#16:Sisi Watoto wa kike tuliopo kwenye mazingira magumu ya kusoma, tukabakwa na wengine kuhadaiwa lakini tukaambiwa tusirudi shule baada ya masaibu yaliyotukumba, Pia TUNA JAMBO LETU, October 28.

#17:Sisi Watanzania tuliokuwa tunapenda kulifuatilia BungeLive, kujua michango ya wawakilishi wetu na namna wanavyotuwakilisha vema hatuchoki, TUNA JAMBO LETU, October 28.

#18:Sisi wengine tusiopenda namna Chombo chetu cha Utoaji Haki (Mahakama) inavyoingiliwa na serikali katika maamuzi yake, ni wazi na Sisi TUNA JAMBO LETU, October 28

#19:Sisi Watanzania tuliochukizwa na namna C. A. G alivyoondolewa kihorera kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu hatupo kimya. Tunatambua mchango wa Prof. Mussa Assad na utumishi wake kwenye Ukaguzi na udhibiti wa Hesabu za serikali. Kwa hali hiyo tunaomba kuwa wazi, TUNA JAMBO LETU, October 28.

#20:Sisi tunaoishi maisha duni, tusiokunywa maji safi, kuzifikia flyovers, tusiopanda ndege, tunaotozwa gharama kubwa mapokezi kabla ya matibabu, tunaokosa vitanda mahospitalini na kupata elimu bure isiyo na misingi imara tumestukaaa, TUNA JAMBO

#21:Sisi waTanzania tuliovunjiwa majumba yetu na serikali bila ya kupewa fidia wala viwanja mbadala wala pole TUNA JAMBO LETU.October 28.

#22: Sisi Tunaotaka katiba Mpya baada ya maoni yetu ya tume ya warioba kufigiswa na Wana CCM kisha tukazimwa kiaina TUNA JAMBO LETU.October 28.
#23; Sisi Wafanya Biashara na waatu wa kawaida tuliingizwa kwenye hali ngumu za kimaisha na uchumi kwa kuharibiwa mzunguko wa fedha nchini TUNA JAMBO LETU.October 28.

Na wengine wengi mfanowetu walioathirika kwa namna moja au nyingine na Utawala huu wa CCM Tuna sema TUNA JAMBO LETU.October 28.

***********************​
Ni lazima tufanye jambo letu October 28 ili kurudisha uhuru, haki na maendeleo yaliyodidimia kwa miaka mingi.
 
Wote tunaona namna mambo yanavyoenda hovyo sana katika kampeni za mwaka huu. Kampeni hizi hazina uhuru wala usawa kwa vyama vyote.

Vyombo vya habari vimekuwa vikitangaza habari ya chama tawala pekee huku Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC, ikiegemea upande mmoja wa chama tawala na kuvikandamiza Vyama vya Upinzani.

Ni leo hii tarehe 28/9 tumeshuhudia mgombea Urais wa CHADEMA Tundu Lissu msafara wake ukipigwa mabomu ya machozi huku Polisi wakizuia njia huko Nyamongo Wilaya ya Tarime. Mhe. Tundu Lissu amesikika akisema

“Kama una malalamiko peleka tume ya uchaguzi, sheria inasema kama una malalamiko unakwenda kwenye tume ya maadili sio unapiga watu mabomu,sasa wewe amua tulale hapa au unipige mabomu au unipige risasi”

Hatua ya kwanza kabisa ya uchaguzi ya kuteua wagombea kwenye tume ya uchaguzi ilijawa na mizingwe mingi. Haiwezekani wagombea wa chama tawala tuu ndio wapite bila kupingwa huku wa vyama vya upinzani wakitupwa nje ya kinyang’anyiro.

Haiwezekani mgombea ambaye alishawahi kuwa Mbunge na kushiriki vikao vya Bunge ashindwe kujua taratibu na namna ya kujaza fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge kwa usahihi.

Ndio, mapungufu ya kibinadamu yapo lakini kwanini yawe kwa wagombea wa CHADEMA na ACT Wazalendo tuu na si kwa chama tawala?

Siwezi kuamini wala haiingi akilini mwangu kamwe mtu kama Susan Limbweni kiwanga Mbunge wa jimbo la Mlimba (2015-2020) na Mbunge wa viti maalumu toka mwaka(2010-2015) ashindwe kujaza fomu kwa ufasaha.

Hapana! kuna sehemu haiko sawa, na nadhani wote tumeona namna wagombea wa vyama vya upinzani wakienguliwa pasipokuwa na hoja za msingi.

Ukweli ni kwamba chama tawala kimetumia mapungufu yaliyopo kwenye Katiba kuteua makada wake kuwa watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, huku wakinadi amani kwenye majukwaa ya siasa.

Tatizo kuu linaanzia kwenye Tume ya Taifa yaUchaguzi. Tume hii sio huru na haitendi haki kwa vyama vyote. Nasema kama sio huru kwa sababu tunaona namna inavyopendelea chama tawala na kuwakandamiza wapinzani.

Matendo ambayo wanafanyiwa watanzania wenzetu waliopo nje ya CCM yanaumiza sana moyo, huku kila siku wafanyakazi wa NEC wakizidi kuonyesha namna ndoa yao na chama tawala ilivyohai na tamu.
Hali hii inaashiria kwamba NEC na chama tawala wana nia ya kuviua vyama vya upinzania nchini Tanzania.

Kwa mfano Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, aliposema hadhari “watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hataki bla! Blah!”
Mkurugenzi huyo aliyasema hayo alipokuwa anazungumnzia kumuandikia barua mgombea Urais wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu ili kutoa maelezo dhidi ya tuhuma za uongo na kukashfu wagombea wenzake.

Binafsi najiuliza toka lini Refa akawa Kocha kwa wakati mmoja uwanjani kwa maana anachokifanya Mkurugenzi ni kampeni.

Ninachoshangaa zaidi ni namna Tume ya Uchaguzi kama Refa huru imegeuka waziwazi na kuvitaka vyama viwe na sera za namna gani katika uchaguzi huu.

Mambo haya yanaleta GIZA kwenye demokrasia na uchaguzi huu umetandwa na giza nene.
Watanzania tulio wengi hatuamini tena kama hii tume inaweza kusimamia na kutetea demokrasia katika nchi yetu.

Inatia uchungu sana na kuumiza kuona namna nchi hii inavyoendeshwa bila usawa. Binafsi najiulizaga sana haya yanayoendelea katika hii nchi ndiyo matunda ya Baba wa taifa kupigania UHURU?

Hatuwezi kusema nchi hii ni huru wakati katika nchi moja kuna watu wanaoishi peponi na wengine wanaishi jehanamu. Nchi hihi kuna watanzania wanateseka na kunyimwa haki zao hadharani alafu wapo ambao wanafurahia maisha.

Nadhani maana ya uhuru katika nchi hii inapotea kwa kasi, kwasababu matendo ambayo wakoloni walikuwa wanawafanyia wazee wetu ndiyo hayo hayo ambayo sasa sisi wenyewe tunafanyiana bila hata ya woga. Inasikitisha sana!

Pamoja na mambo hayo yote ya kusikitisha na kuvunja moyo kuendelea kutokea nchini, bado naamini nguvu ipo mikonomi mwa watanzania na tukihitaji uhuru wa kweli tutaupata.
Ngugu zangu naomba mukumbuke kuwa haki haiombwi haki inapiganiwa.

Nadhani kila mmoja wetu anakubali kwamba matatizo mengi yameletwa na Katiba iliyopo. Uchaguzi huu kama zilivyokuwa chaguzi zilizopita umeonyesha dhahiri umuhimu wa katiba mpya.

Tanzania inahitaji katiba mpya hii ndio dawa ambayo itaweza kutenganisha serikali pamoja na chama tawala. Taifa likiendelea na katiba hii hata siku ikatokea CCM ni chama cha upinzani nacho kitalalamika sana. Tunahitaji Katiba ambayo itaondoa malalamiko kwa vyama vyote.

Nchi hii ni yetu sote na lazima tupiganie maendeleo ya watu wote bila kujali dini, rangi ya ngozi wala kabila. Watanzania yatupa sana tuungane kwa pamoja kukemea uovu hata kama Katiba yetu inamapungufu tusikubali wenye mamlaka kufanya kinyume na katiba.

Itoshe kusema kwamba tarehe 28 Oktoba usikose kwenda kupiga kura kwani kura yako moja italeta mabadiliko makubwa sana katika kile unachokiamini pamoja na nchi yetu.
Acha kupoteza muda bure,kulalamika hakusaidii.
 
Mimi naamini tunapaswa kufanya zaidi ya kupiga kura tu. Ni wazi wazi kabisa sasa kuwa NEC wanaitafutia CCM ushindi wa hila. Nawaambia watanzania tusipoingia mtaani kwa maandamano makubwa hakuna haki yoyote tutakayopata. Tushinikize tume huru isiyoteuliwa na rais.
Anza wewe kuingia barabarani unasema wakati wewe umekaa nyuma ya keyboard.
 
Mimi naamini tunapaswa kufanya zaidi ya kupiga kura tu. Ni wazi wazi kabisa sasa kuwa NEC wanaitafutia CCM ushindi wa hila. Nawaambia watanzania tusipoingia mtaani kwa maandamano makubwa hakuna haki yoyote tutakayopata. Tushinikize tume huru isiyoteuliwa na rais.
Tume haiwezi kuwa huru bila kushirikisha vyama vya upinzani 'HASA KWENYE KUHESABU KURA KWA UWAZI' ulishaona wapi mbwa anaung'ata mkia wake,mbwa hata awe mkali vipi hawezi kuung'ata mkia wake. 'Selfimage and gesture can tell the true colours of NEC leadership '
 
2434814_ERFcWLLW4AIVOAq.jpg
2434814_ERFcWLLW4AIVOAq.jpg
TANGANYIKA NA ZANZIBAR.jpg
i cant breath JPM.jpg

Haya ndiyo yanayotushawishi tusiichague CCM
 
Back
Top Bottom