bibilia imeeleza jambo hili kwa uwiano sawa kabisa,ni hatari sana mtu kutoa argument bila referal.
Kunena kwa lugha ni kusema kwa lugha nyingine sawasawa na Roho wa Mungu alivyokuijilia.
NOTE;a/ Kuna kunena kwa lugha kama kipawa/karama.
1kor 14:2~maana yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu,bali husema na Mungu,maana hakuna asikiaye,lakini anena mambo ya siri katika roho yake.
KUNA MAMBO YA SIRI AMBAYO WATU HATA WEWE MWENYEWE(mwili wako) HUPASWI kuyaelewa unaposema na Mungu wako,sawasawa na andiko hilo hapo juu.
b/kuna kunena kwa lugha kwa kila aaminiye.
mark16:17-na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio.kwa jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya.
NI MAAGIZO YA YESU MWENYEWE KWA KILA AMWAMINIYE YESU.
Katika maagizo yale hakuna sehemu amesisitiza kuwa watakapokuwa wakinena kwa lugha mpya watatakiwa pia wafasri.kumbuka hilo!
ILA KATIKA UWIANO WA MAANDIKO,maandiko sehemu nyingine yanasema kufasiri hasa katika mafundisho ya kitume,sio kwamba yanapingana lahasha!
kumbuka.Rum 8:26,27 ~ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu,kwa maana hatujui kuomba itupasavyo.
ELEWA LEO.KAMA ROHO MTAKATIFU akitaka ufasri huwezi kumzuia na kama haoni sababu huwezi kumulazimisha maana yeye ndio anajua udhaifu wako katika kuomba,na mara nyingi kufasri huja hasa pale unapowaombea wengine ili pale ROHO wa MUNGU anapotaka kuwasaidia wengine kupitia maombi hayo wapate kuelewa na kusikia kile MUngu anataka akione au anataka wakifanye,au watubu,au wabadili mwenendo n.k sawa na mapenzi yake juu ya hao unaowaombea kupitia ROho mt.
Sijaandika kibibilia mkuu. nimeandika kijamii kwa uwiiano sawa. ila ngoja nitoe maoni yangu kutoka katika maelezo yako.
1:Kunena kwa Lugha Mpya, sio siri ni tukio halisi na lilirekodiwa katika kitabu kitakatifu bibilia. Matendo 2.
katika tukio hilo kuna facts kadhaa.
* Mitume walinena kwa lugha mpya ambayo ilidhibitishwa na waliosikia kuwa lugha halisi za kibinadamu ambazo zinaongelewa na watu wamataifa mengine. Hakukuwa na Lugha hizi zisizofahamika.
Ushahidi wa Vitendo unanguvu kuliko ushahidi wa maelezo yanayohitaji tafsiri.
mfano ukiandikiwa habari mtoto wako kanywa sumu kisha akaanza kutoa mapovu na details za tukio zima ni tofauti na mtu kuelezea kifo cha sumu kwa ujumla. Somo zuli tunalichukua pentecoste kwa mitume. Lugha zao zilieleweka.
*Hakuna ufanano wowote kati ya mazoezi au program za kanisa zinazopelekea waumini kunena kwa lugha zisizofahamika na kile kilichotokea wakati wa mitume.
*Kwa mujibu wa tafiti ya Scientific study of Religion mtu akielekea kunena kwa lugha mpya kabla ya hapo huwa katika hali ya juu ya Emmotional instability (trance) tofauti na mitume walikuwa katika high SPIRITUAL STABILITY.
Mwisho.
Binafsi nimewahi kuhudhuria katika mkutano wa injili ulioendeshwa na mtu wa kuaminiwa sana nchini. mke wake alituongoza katika utaratibu wa kuvuviwa na huyo roho aneneshaye, (binafsi niliacha kufuata maelekezo yake kwa sababu yalikuwa kinyume na bibilia). Alituamuru tutaje neno Yesu au Mungu mfurulizo harakaharaka hadi utaona unavuviwa na kutamka maneno usiyoyajua.nilikataa kwa sababu mbili...
1) Zoezi hilo lilikuwa kinyume na amri za Mungu (usilitaje jina la bwana Mungu wako Bure).
2) Zoezi hilo linapingana na matukio yote ya kwenye bibilia yanayozungumzia kunena kwa Lugha. kwangu niliona ni mifumo miwili kinzani.
KUHUSU MAONI YAKO;
1 Wakorintho 14, inatoa maelezo ya kutosha kuhusu mada hii. Japo wakorintho hiyo ili tuielewe vizuri ni vizuri kujua mazingira ya mji huo,
ni vizuri ujua nini kilipelekea Paulo awaandikie hayo. Ili kujenga jukwaa zuri la kujengea hoja.
MAMBO KADHAA...
1:Mji wa Korintho ulianzishwa na Kaisali Julius, mji huo ulikuwa ni mji mkubwa kabisa wa kibiashara na makao makuu ya jimbo la Achaia. Ulikuwa ni kitovu cha miungu mingi ya kipagani na kila aina ya ibada za kishetani pia. Hivyo kanisa la Korintho liikuwa na changamoto kubwa sana ya kuingiza mambo yasiyofaa kutoka kwa upagani unaowazunguka.Na kuna uwezekano mkubwa kuingia kwa upagani katika kanisa ilikuwa sababu ya uandishi wa Barua yake kuwakumbusha misingi.
2:Kwa Sababu Korintho ilikuwa HUB ya kisiasa na kbiashara, Jiji hilo lilikuwa na population ya watu wa Lugha mbalimbali. Na kwa maneno mengine Kanisa lilihitaji Kalama ya Lugha (Zinazoeleweka kwa wageni) ili kuhudumia watu wa kila kabila.
Kwa haya hiyo inaonekana kulikuwa na tatizo ambalo LIPO SASA, watu kudhani kunena kwa Lugha kunakufanya uwe bora. Dhumuni la Kunena kwa Lugha ni KUHUBIRI INJILI na KUJENGANA sio Kuonyesha ubora wa Muumini.
Naamini Paulo anazungumzia LUGHA inayoeleweka Sio Zile ambazo anayenena haelewi, wanasosikia hawaelewi nadhani hata Malaika nao hawaelewi.
##########################
kwenye maelezo yako.
a) Sioni kama hapo paulo anazungumzia lugha hizi tunazozisikia zisizoeleweka hata kwa msemaji. Kwa msingi wa hoja yangu pale juu, wakolinto kwa mazingira waliyokuwapo wengi wa waumini walikuwa na ujuzi wa Lugha Mbalimbali na kama haitoshi Bado wapo waliovuviwa na Lugha mpya kama mitume (matendo 2).
Hivyo Wewe Ukiongea Kiingereza kanisa la kijijini ambalo hawajui hata kiswahili humjengi mtu. Utajijenga wewe ambaye unakijua na unajua unaongea nini. Ndiyo maana mambo hayo Mtume anashauri Ujinenee peke yako ukiwa sirini au basi kama umewiwa sana unene kiingereza kwa wasukuma na wasukuma watafsiriwe ili wajengwe na wao. Vinginevyo wewe utakuwa kituko au kama mjinga mbele ya wasikilizaji wako.
b) Hoja ya marko 16:17 inajibiwa na bibilia yenyewe sio hiki tunachokiona. Walioambiwa walinena kwa hiyo Lugha mpya tofauti na waliyozoea na kukulia. Waliowasikiliza Walielewa maana dhumuni ya Lugha ni Mawasiliano. Ntamshangaa Mungu kama atawasiliana na mtu kwenye kadamnasi kwa Lugha ambayo huyo anayeongea haielewi, kadamnasi nayo haieewi. Au yeye anaielwe ila wasikilizaji hawaelewi. Huo ndio msingi wa kukemea tabia hizo paulo.
c) Waliponena kwa Lugha mpya, mitume kwa sababu walikuwa wengi na waliosikiliza mashahidi walisema tumewasikia wakinena kwa Lugha zetu wenyewe mambo makuu ya Mungu. Hiyo siamini kama Lugha walizonena ndio hizi mpya tunazozisikia na kutozielewa japo nachelea kusema hizo sio lugha bali ni Sauti, maana Lugha ni medium ya mawasiliano, na kama hakuna kuwasiliana au uelewa kati ya wahusika inaua maana ya lugha.
d)Roho kutuombea hakuna uhusiano na Kunena kwa Lugha mpya. Kuugua kusikotamkika hakuna uhusiano na kuugua kunakotamkika tunakokuona kwenye nyumba za ibada. Yale matamshi yanatamkika mkuu ila huo mstari unazungumzia mambo yasiyotamkika, Lakini pia Roho ndiye anayekuombea sio wewe. kwa hiyo hapo anahusika roho sio hao wanaoongea.
Yawezekana tumekuwa tofauti kutokana na asili ya mafundisho.
Lakini ukisoma vizuri hiyo 1 wakorinto 14, Sio tu inapinga bali inakataza mengi ambayo tunafanya sasa. Na kama Lugha ni kalama basi ni kosa kubwa kutaka kanisa zima linene kwa Lugha maana utakuwa unalazimisha mwili wote uwe sikio.
karibu kwa maoni na changamoto mkui.