OK,Naomba turudi hapa
1kor14:14~maana nikiomba kwa lugha,roho yangu huomba,lakini akili hazina matunda.
Tazama vizuri mstari huo,anaomba kwa lugha meaningly kwa Roho wa Mungu ila pia na roho yake inaomba.
Naomba nikunukuu kidogo mkuu
''Hivyo KUUGUA Kusikotamkika (gnoaring that cannot be uttered)''
gnoaring linatokana na neno gnoar,ok,ngoja tuchek maana ya neno hili
gnoar-a low, mournful sound uttered in pain or grief: the groans of dying soldiers.
ukiunganisha na nukuu yako hapo juu unaweza kuona utter imo ndani ya gnoar.
Lakini pia watalamu wa lugha wanasema synonomy ya utter ni pamoja na pronounce.
UKIAMBIWA HUWEZI KUPRONOUNCE NENO FLAN SI KWAMBA HUWEZI ILA HUTALIPATIA THE WAY TO BE PRONOUNCED.
Msisitizo mkubwa wa YESU kwa wanadamu wanaomwamini ni kuomba.swali.
kwanini tuombe kama Roho wa Mungu anatuombea.?
Man can do nothing without God,and God will do nothing without man.
Roho yoyote hapa duniani ikitaka iaffect physcal realm inatafuta mwili,bila mwili it is illegal si kwa Mungu si Shetani.KWANINI
Kwasababu Mungu hawezi kubreak his own law,alisema wakati anamuumba mtu,Let him have rullership and not us,
Shetani alitafuta physcal body to express his opnions kwa mwanadamu otherwise was illegal.
Nataka kwenda mbali sana huku,ngoja turudi hapa
Rum 8;16~Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu,
Umeiona hiyo fellowship,bila roho yako ambayo maskani yake ni mwili wako hapa duniani Roho wa Mungu hanamahali pa kutestfy.
Naomba nifunge huu mjadala kwa maoni yangu kuwa,biblia ni kitabu cha Mungu kumuhusu mwanadamu,kimeeleza mema na mabaya yaliyofanywa,yanayofanyika na yatakayofanywa na wanadamu.
Point yangu ni kuwa ukiona kitu kinafanyika kibaya na watu fulan usifikiri hawapo watu wanaoweza kukifanya kitu kile kile kwa utaratibu sawa unaotakiwa.
asante maelezo mkuu.
kwanza ninaomba nitoe tongotongo katika hili.
Tumejenga hoja vizuri huko juu kuwa.
Yesu alisema wanafunzi wake watanena Lugha mpya (Kwa maana ninayoisimamia mimi "Lugha mpya za Kibinadamu zilizokuwa hazifahamiki kwao kabla kama ishara ya Uwepo wa Roho mtakatifu''.
Tukasema pia, Hao walioambiwa, wakiwa jumla ya watu 120 unabii wa Yoeli (Roho mtakatifu kuwashukia) na Utabiri wa Yesu (Kunena Lugha mpya za Kibinadamu zilizoeleweka kwa wasikilizaji).
Tukakubaliana kuwa Ushushwaji wa roho mtakatifu utaambatana na Vipawa vyake au kalama. Na miongoni mwa kalama ilikuwa ni Kunena Kwa Lugha.
Na msingi au dhumuni la kalama ni Kulijenga na kulikuza kanisa. 1 Korintho 12:7 " Kwa faida ya wote''. Tena kwa ajili ya kueneza injili. Hakuna self-Centered Gift.
Na tunakubaliana kuwa Tukio la matendo 2 linasadifu takwa la umuhimu wa 1 korintho 12:7 .
:::::::::
Mtiririko hapo juu unaonyesha wazi, mgogoro Uliompelekea Mtume paulo kuandika 1 Wakorintho 14. ni watu kukiuka mtiririko huo mwema.
Kunyofoa kifungu katikati ya haya hiyo ili kutetea kinachoendelea ktk habari ya kunena sioni kama ni sawa.
Nadhani ni Busara takatifu kurudi kwenye mpango wa Mungu kwa mtiririko pale Juu.
Katika hilo mkuu nakoswa ushauri zaidi ya huo.
:::::::::
WARUMI
Naogopa na nashawishika kuamini kwamba, Watu walianza KUNENA KWA LUGHA HIZI Tunazozisikia maknisani, Kisha wakarudi Kuzitafutia uhalali kwenye BIBILIA.
Hii ni kwa sababu kubwa moja na nadhani utakubaliana na mimi kuwa haina utetezi ulionyooka zaidi ya utetezi unaokinzana au pishana mfano.
Je ni Lugha ya Mbinguni?
Je ni Lugha ya Malaika (1cor 13:1)?
Je ni Lugha ya Roho mtakatifu (warumi)?
Je ni Lugha ya mpya za kidini ambazo wanadamu wengine hawazielewi?
Vyote vitatu havina ushahidi wa wazi na wakivitendo katika maandiko zaidi ya kile kimoja ambacho kiko wazi na kinasomeka kama maji (mdo 2) Yaani Lugha mpya za wanadamu ambazo wagalilaya hao walikiwa hawazielewi kabla ya kueleweshwa kwa uwezo wa roho mtakatifu ili injili itapakae ktk kila Lugha. 1 Kor 14 yote imeandikwa ili tusifanye makosa waliofanya hao jamaa.
KUUGUA KUSIKO TAMKIKA.
1:Bibilia haijasema Roho akiyuombea, hiyo ni kalama ya Roho yaani kunena kwa Lugha.
Roho wa Mungu Kuwaombea wafuasi wa Yesu ni kitu kingine na Roho kuwashushia wafuasi wa Yesu uwezo wa Kunena Lugha mpya. ndio maana hapo juu nilieleza utetezi wako hauungani.
2:Haugui Roho, naugua mimi. Hashindwi kutamka roho, ninayeshindwa kutamka ni mimi. Gnoaring ni hali ya Uchungu kiasi cha kushindwa hata kutoa neno unabaki unaguguna tu, na wengine hufikia hatua ya kulia tu. Jambo hilo ambalo umeshindwa kuliwasilisha tunatiwa moyo na maandiko, Roho hutusaidia kutufikishia hizo hoja na haja kwa Mungu.
Sioni uhusiano wa kuunganisha tukio hilo na Kalama aliyopewa mwanadamu na Mungu ili kulijenga kanisa au kufaidisha watu. Kalama hawapewi Wote, wewe unaweza kupewa kalama Ya kunena kwa Lugha, mimi nisipewe hata chembe maana Roho ndiye anayegawa kama atakavyo hakuna wa kumshawishi.
Kwa fungu hilo Roho wa Mungu anawaombea wote wenye hiyo hali. Hata mimi ktk hrkati za maisha napitia changamoto ngumu hata kutamkika ktkt ya maombi naweza kutoa chozi tu au kuishiwa maneno, Sihitaji kalama ya Roho ya kunena kwa Lugha Bali Roho huniombea mwenyewe.
Swali: Kwa nini tuombe wakati roho anatuombea?
Jibu jepesi. Fungu hilo liko wazi anatuombea katika mazingira ambayo tunaugulia kiasi cha sisi wenyewe kushindwa hata kueleza hoja yestu katikati ya maombi. Huo ni udhaifu wa kibinadami unaojazwa na na Roho mkuu nje ya hapo. OMBENI BILA KUKOMBA Yesu aliliweka wazi hilo. Tuombe mkuu. Fungu hilo ni motisha wa kuomba na sio kinyonyanguvu ya Maombi na kichochea uzembe na utegevu wa Kuomba.
Kuomba ni kiwasiliana na Muumba wako. kwa mstari huo tunahakikishiwa waziwazi udhaifu wetu wa kibinadamu katikati ya kuwasiliana na mwenye enzi unazibwa kwa Roho kutusaidia.
Otherwise mkuu nakushukuru kwa michango na changamoto nzuri zinazojenga.
Nyongeza kidogo ila sio kwa umuhimu maana niliahidi.
Kwa Mujibu wa magombo yaliyogunduliwa, yenye maandishi na nukuu za wakristo wa karne ya kwanza inaonyesha wazi kuwa hao wakolrintho walikiwa hawaneni Lugha zisizoeleweka hizi za kikarismatiki bali ni Lugha zankibinadamu.
Irenaeus circa 185 A.D.
Clement of Alexandria circa 190 A.D.
hawa wote commentaries zao zinaungana na ninachokisema.
John Chrysostom 386 -398 AD wakristo wa karne ya tatu waliamini ninachokisema.
- Origen (185 to 254 AD);
- Eusebius (263 to 339 AD);
- Athanasius (293 to 373 AD);
- Gregory of Nazianzus (330 to 390 AD);
- Gregory of Nyssa (335 to 394+ AD);
- Hilary(300 – 367 AD);
- Jerome( 347 to 420 AD);
- Epiphanius(310/20 to 403);
- Augustine (354 to 430 AD);
- Theodoret( 393 to 457); and
- Gregory (540 to 604 AD).
Wote hawa mababu wa kikristo pia waliamini wakorinto walinena lugha za wanadamu sio hizi tata.
- Thomas Aquinas (famous Romanist Philosopher – 1225 to 1274 AD)
- Martin Luther (Protestant Reformation leader – 1483 to 1546)
- John Calvin (Protestant Reformation leader / Biblical commentator – 1509 to 1564)
- Matthew Henry (English non-conformist minister and Biblical commentator – 1662 to 1714)
- John Gill (English Particular Baptist minister and Biblical commentator – 1697 to 1771)
- Adam Clarke (British Arminian theologian and Biblical commentator – 1762 to 1832)
- Robert Jamieson (1802-1880); Andrew Robert Fausset; and David Brown (1803-1897): Authors of the famous “Jameison-Faussett-Brown commentary”
- John Nelson Darby (author of the Synopsis of the Books of the Bible and founder of the error of Dispensationalism – 1800 to 1882).
Wote hawa waliamini ninachokisema.
nadhani ushahidi kwa kisayansi usipoonekana na maana, ushahidi wa historia ya wakristo wenyewe inaweza kuongeza kina cha uelewa.
cc
zitto junior na wadau wengine.