Goba vs Kigamboni: Wapi ni pazuri zaidi?

Goba vs Kigamboni: Wapi ni pazuri zaidi?

Msomaji2

Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
17
Reaction score
38
Msaada wa kimawazo

Hivi kati ya Goba na Kigamboni, wapi pazuri kujenga na kuishi.

Naomba ushauri wapi kuna maeneo mazuri.

1. Bei za viwanja
2. Huduma za kijamii
3. Usalama
4. Wapi ni potential
5. Na mengineyo

Utofauti upoje ndo nataka kujua, buget ya plot sio issue sana
..
Natanguliza shukrani[emoji120]
 
Basing on my opinions Goba kupo sawa zaidi kuliko kigamboni . Goba kuna service zote pia karibu na mjini changamoto za foleni na usafiri ukiwa goba ni nafuu zaidi kuliko kigamboni.
Thank you, kwa maoni yako
 
Msaada wa kimawazo
...
Hivi kati ya Goba na kigamboni, wapi pazuri kujenga na kuishi.
Naomba ushauri wapi kuna maeneo mazuri
1. Bei za viwanja
2. Huduma za kijamii
3. Usalama
4. Wapi ni potential
5. Na mengineyo
...
Utofauti upoje ndo nataka kujua...buget ya plot sio issue sana
..
Natanguliza shukrani[emoji120]
Wewe unapenda sana Beach sasa Goba mpk Bichi na Kigambon mpk Bichi
Wapi jiran?
 
Msaada wa kimawazo
...
Hivi kati ya Goba na kigamboni, wapi pazuri kujenga na kuishi.
Naomba ushauri wapi kuna maeneo mazuri
1. Bei za viwanja
2. Huduma za kijamii
3. Usalama
4. Wapi ni potential
5. Na mengineyo
...
Utofauti upoje ndo nataka kujua...buget ya plot sio issue sana
..
Natanguliza shukrani[emoji120]
Nitachangia kama ulivyo-outline
1) Bei za viwanja Goba inaweza kuwa juu kidogo ukilinganisha na Kigamboni .
2) Huduma za Kijamii Goba ina access options nyingi kuliko Kigamboni kutokana kuzungukwa na maeneo jirani yaliyokwishajengeka kitambo kabla ya Goba ku-pick up.
3) Usalama ni subjective kutokana na eneo gani hasa katika maeneo yote mawil, mf; Geza viwanja vipya wana organised communities security ambazo wanachangia na zimepunguza sana uhalifu. Goba kuna baadhi ya maeneo hasa walipojenga vigogo kuna same communities.
4) Kigamboni ni Potential zaidi, cause still kuna maeneo mengi yapo wazi na yanafikika kiurahisi
5) Miundombinu ya Kigamboni ipo bora zaidi kulinganisha na Goba. Pia viwanja vingi vya Kigamboni ni flat kulinganisha na Goba ambako kuna miinuko mingi. Kuhusu umbali Kigamboni ipo karibu zaidi na mjini kuliko Goba. Changamoto ya Kigamboni ni lazima uvuke maji kwa kulipia na kuna njia 3 kuu za kuingia na moja ya zaidi ikitokea Kongowe.
All in all Kigamboni ni pazuri zaidi kwa kujenga na kuishi as kuna population kubwa already.
 
Yote ni maeneo ya makazi bora lakini Goba ipo centre na ina access zaidi ya vitu vyote ulivyovitaja kuliko kigamboni KWA SASA,

Goba barabara zake zipo connected na morogoro road na bagamoyo road ambazo ardhi yake ni hot cake kuliko kilwa road ambayo kwa kiasi kikubwa ndio imeizunguka kigamboni.

Kuhusu potential ya kigamboni bado haitabiriki lakini ninachojua itakuwa mji flani wenye kujitosheleza kila kitu tofauti na maeneo kama goba ambayo itaendelea kutegemea sehemu zingine za dar kupata service.
 
Back
Top Bottom