The very one thing i like about these God stuffs ni pale mwanadamu alipopigwa marufuku kuhoji kuhusu Mungu! Ni Mungu huyu huyu ambae tunaaminishwa kwamba anatupenda wanadamu na ametujaalia hili ama lile bado ni Mungu huyo huyo ambae anatupiga marufuku kumchimba na kumchimbua kwa mapana na marefu! Sie tunaoendaga msikitini tunaambiwa; NO, in fact, TUNATISHWA kwamba kuchimbua sana kuhusu Mungu ni KUFURU! Ada ya mwenye kukufuru na moto wa Jehanamu...leo hii kila mmoja anaogoapa kukufuru; anaogopa moto wa Jehanamu! Ukienda upande wa pili, wale wa kanisani; nako si salama hata kidogo! Huko ukichimbua chimbua kuhusu mambo na related stuffs utaambiwa, no, UTATISHWA kwamba UNA MAPEPO, unapaswa kuombewa!! Kila mmoja anaogopa kuonekana ana mapepo, ambao bila shaka hawa nao hawatauona uzima wa milele! Ni Mungu mwenyewe ndie alitoa agizo kwamba tusimchimbechimbe au na hawa mawakala wake wanaokula kupitia jina lake! IKiwa ni Mungu mwenyewe ndie alitoa AGIZO, ni kwanini basi hakutaka tutumie uwezo aliotupatia ili tuweze kumchimba kisawa sawa? Anaogopa nini? Au ni hawa mawakala wake ndio wanatukataza kuchimbachimba kuhusu Mungu? Kama ndio, wanaogopa tutagundua nini? Ni kwamba wana mashaka juu ya uwezekano wa kuendelea uwapo wa mkate wao, au?