Mungu ni mawazo yaliyopo kichwani mwako wala hayupo
Na hizo ni hadithi waliosemezana watu wa kale na ndio utakuja kuona huyo mungu anapewa sifa kubwa wakati hakuna anachokijua
Kwakuwa mungu ametungwa ndio maana wapo wengi sana
Mkuu,
Kuna Post nimeitoa hapo juu kuchangia swami la Da Hustla ningependa nichangie katika point pale kuwa sifa mojawapo ya Mungu Muumba ni kuwa lazima ajidhihirishe katika hoja za kiakili, kisayansi na kiroho.
Sasa hebu fuatilia Post yangu hii kisha uone kuwa zao la Mungu muumba sio zao la mawazo yaliyopo kichwani mwa mtu bali uhalisia kutegemeana na Mungu yupi unayemuabudu.
Natanguliza kujenga hoja kwa aya ndani ya Qur'an kisha nitoe maelezo kwa ufupi.
Mungu anasema katika Surat At-Talaaq aya ya 12.
"
Mwenyezi Mungu nu yule ambaye amezuimba mbingu Saba, na Ardhi kwa mfano wa hizo. Amir zake zinashuka baina Yao, ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba mwenyezi mungu amekizunguka kila kitu kukijua vilivyo kwa elimu yake. (quran 65:12)
Ufafanuzi:
Hapo tumeambiwa Mungu kaumba mbingu saba. Kuna tafsiri mbili hapa na mimi nitatoa moja tu.
Mbingu saba kwa matabaka (Atmosperic layers)
1. Troposphere
2. Stratosphere
3. Ozone Layer
4. Mesosphere
5. Ionosphere
6.Thermosphere
7. Exosphere
Hizo ni major spheres ingawa wanasayansi wamejaribu kuzi-subdivide kama stratopause au tropopause, belts ,nk
Ndani ya hizo layers kuna amri nyingi sana (Commands) kama upepo (kuvuma au kutulia), kupwa na kujaa kwa bahari, kimbunga, photosynthesis, mvua (formation of rains), joto, baridi, Masika, kiangazi, radi, mawingu ya kawaida au ya mvua, mawingu kwenda kasi au kawaida,nk. Na hiyo ni katika Troposphere tu. sijakwambia Ozone layer, repulsion of meteors, x-rays, gamma rays. Nasi humo katika layers tunapata manufaa makubwa sana ya kurusha satellites, kupata mawimbi ya sauti, Simu, radio, TVs, rockets zinapita nk.
Aya inasema; "Na ameumba Ardhi kwa mfano wa hizo (Mbingu Saba)":
Hebu nazo tuzione kama kweli zipo saba.
core.
1. Inner Core (Solid)
2. Outer core (Liquid)
Mantle
3. Methosphere
4. Esthenosphere
5. Lisosphere
Crust
6. Continental crust
7. Oceanic crust
Sijakwambia Amri zinazotoka humo pia kama kupwa na kujaa kwa bahari, aina mbalimbali za udongo, miamba,uoto mbalimbali, madini, maji ya visima, ladha za maji mbalimbali, volcano, landsildes, nk, nk, nk
hizo zote ni amri zinazotoka kwa Allah Muumba. Nasi tunapata faida kubwa sana humo na Maisha yanaenda.
Na katika hali zote hizo hakuna mwanasayansi aliyetengeneza au kuumba na wala hawezi kubadilisha chochote Zaidi ya kukielezea tu. Cause and effect remain to al-Mighty God and leaves scientists to explain.
Sasa vyovyote watakavyoelezea, wakipatia sawa, wakikosea Mungu kishasema na kufanya. Naye ndiye aliekizunguka kila kitu kwa Elimu (Ujuzi) yake.
Conclusion: Mungu kasema kafanya, na akasema Kuna amri. Mengi tunayashuhudia na mengine sayansi imethibitisha, akili pia imekubali. Kilichobaki hapa ni roho kuitikia wito kuwa kweli aliyeyafanya haya si mwingine ila ni Mungu Muumba mwenye uwezo wa kufanya, kutoa amri na kuvilinda.
Kwa hiyo wazo la Mungu Muumba au Mwenyezi Mungu sio zao la akili au mawazo. Labda unaongelea neno Mungu kwa tafsiri ya wingi wa miungu.