Godbless Lema afutiwa mashitaka ya uchochezi huko Singida

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426


Waliomshitaki wameshindwa kuthibitisha mashtaka yao jambo lililopelekea Mahakama kuamua kumwachia huru .

Ikumbukwe kwamba Mh Lema aliweka hadharani orodha ya watu waliouawa kinyama mkoani Singida kutokana na kuiunga mkono Chadema , hicho ndio kikawa chanzo cha kukamatwa na kushitakiwa .

Kutokana na Lema kuachiwa huru ni wazi sasa kwamba yote aliyoyaongea yalikuwa KWELI TUPU .

Mungu ibariki Chadema .
 
Bora alitafuta hifadhi mapema. Angekuwa yupo humu nchini, huenda ungekuta yuko mahabusu mpaka muda huu na hiyo kesi isingefutwa.

Jicho la tatu: Waliomua Mawazo wamehukumiwa kifo, na Lema leo kesi yake imefutwa, huku Sugu nae hoteli yake ikisalimika kuvunjwa. Si ajabu tukasikia na kesi za Lissu zimefutwa.

Je, si kuwa tuhuma zilizopelekwa ICC zinachangia maamuzi haya?

Nawaza tu.
 
Hili linamaana gani ikiwa anayewekwa huru hayupo nchini na yupo "uhamishoni"?

Alafu, hiyo Kesi iliendaje yeye hayupo au mawakili wake walikuwepo? Kwann zile kesi za Lisu haziendeshwi namna hiyo akiwa hayupo?
 
Hili linamaana gani ikiwa anayewekwa huru hayupo nchini na yupo "uhamishoni"?

Alafu, hiyo Kesi iliendaje yeye hayupo au mawakili wake walikuwepo? Kwann zile kesi za Lisu haziendeshwi namna hiyo akiwa hayupo?
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania anaitwa Kilangi ni vema ukamcheki atoe ufafanuzi
 
ukweli mtupu .
 
Wengine tunahoji kwanini aliamua kutafuta hifadhi,majibu tunazidi kuthibitisha mashtaka yakikuwa wa kubambikiwa kwakuhesabika kama mmoja wa wnaosemwa kukwamisha maendeleo badala ya kuchochea maendeleo.
 
Ni moja ya njia za kupunguza sehemu ya makosa yaliyotendwa na wahusika,ili kupunguza makalu ya kesi zidhi ya wote wanaohusika.
 
kulikuwa na maana gani sasa ya kufungua hizo kesi, hiyo ni kupoteza muda na fedha za walipa kodi
 
Ni kweli!Inaelekea kuna mabadiliko fulani yanatokea lakini nahisi hawataki ionekane kuwa wanabadilka.
Nahisi kuna pressure either within au from outside!
Suala la wabunge wa viti maalum wa Chadema litatuongezea mwanga.
 
Safi kabisa, sasa kibao kigeuzwe kwa Wasaliti waliomtonya mpaka akasepa.
 
Mahakama zetu ziko huru na hakiii. Hongera zake mzee lemaa, kwa kutendewaa hakii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…