- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu salama?
Nmekutana nahii picha na nmeona watu wanasema kuwa si ya mwaka huu 2025. Uhalisia ukoje JamiiCheck?
Nmekutana nahii picha na nmeona watu wanasema kuwa si ya mwaka huu 2025. Uhalisia ukoje JamiiCheck?
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), ambaye mnamo tarehe 23 Machi 2025 alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Oparesheni ya 'No Reforms No Election' ukiwa ni mwanzo wa ziara ya mikutano ya hadhara nchi nzima iliyopangwa kufanywa na viongozi wa chama hicho.
Aidha katika muendelezo wa mikutano hiyo Mnamo tarehe 27, Machi 2025, Lissu alifanya mkutano wa hadhara Tunduma mkoani Songwe ambapo pamoja na mambo mengine alieleza umuhimu wa mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu 2025 ili kuimarisha uwazi, huru na haki.
Madai.
Kumekuwapo na picha inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kuwa ni kutoka mkutano wa hadhara wa Lissu uliofanyika Tunduma mkoani Songwe tarehe 27, Machi 2025.
Uhalisia wa picha husika.
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search umebaini kuwa picha hiyo ilichapishwa mtandaoni kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 19 Agosti, 2020 wakati wa kampeni za Urais, ambapo Lissu alikuwa ni mgombea kupitia CHADEMA. Rejea picha hizo zilichapishwa hapa, hapa, hapa na hapa zilizochapishwa kwa nyakati tofauti.
Hivyo matumizi ya picha hiyo kurejelea mikutano ya hivi karibuni ni kupotosha uhalisia.
Aidha hizi ni sehemu ya picha zilizopigwa katika mkutano wa Lissu wa tarehe 27, Machi 2025 Tunduma mkoani Songwe. tazama hapa na hapa.
Tazama hapa mkutano wa Tundu Lissu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2020 mjini Tunduma.
View: https://youtu.be/f1RXCY1BHV0?si=IhxLUd1RkCYgnqwp