Kuna watu wanabeza ombi la Lema na kulifanya kisiasa.
Iko hivi, Kuna siku mwanafamilia yako atapotea Kama Ben Saanane, atapigwa Risasi Kama Lissu, atapotezwa Kama Azory na utahangaika pasipo majibu, utalia pasiwe na wa kukufuata machozi.
Utafuatilia kwenye kila taasisi hutapewa ushirikiano uliotegemea. Utatamani kukaa matanga lakini utasema je akiwa bado yu hai itakuaje.
Hivyo kabla ya kubeza kuweka siasa jiulize hili linamanufaa kwa umma?
Pili tutambue mojawapo ya kazi ya serikali ni kulinda raia wake na Mali zao popote walipo hata nje ya mipaka. Sasa anapotokea kapotea mtu au kuuwawa pasipo kujulikana lazima serikali ichunguze na kuwakamata wahusika.
Sasa kupotea kwa Ben na Azory Kuna Mambo mengi yamesemwa, kupigwa kwa Lissu Risasi Kuna mengi yamesemwa. Familia zao zinataka majibu na watanzania tunataka majibu.
Kuna waliokotwa beach na mtoni watanzania wanataka majibu wale ni kina Nani na waliuwawa na kina Nani?
Watanzania wengi wamepotea hasa huko Rufiji na Mkuranga watanzania wanataka kujua walipo.
Lakini pia Kuna watu walitekwa Mohomed Dewj, Roma na wengine watanzania wanataka majibu kina Nani walikua wanafanya utekaji ule? Je wameshadhibitiwa?
Vijana wa CCM na all pro CCM, Kuna wengi mlikua mnamshabikia Sabaya na kusema alikua anamshughulikia Mbowe, kumbe alikua anafanya yaliyo kinyume na kiapo chake Sasa hivi mnamkimbia.