Godbless Lema amuonya Millard Ayo kwa kuonesha unyama wa Polisi wa Kenya na kuficha unyama wa Polisi wa Tanzania

Hawa wa huku kwetu wana fujo sana sasa dawa yao ni kususia kutangaza habari zao....huyo ayo atangaze tu ya Kenya mpaka wale wa hapa Bongo waone wivu.
 
Chama kina gazeti - Tanzania Daima, kina online TV, na Kubenea na Komu wana gazeti pia, nina uhakika hivyo vyombo vya habari vingetosha kututangazia yale ambayo wengine hawayatangazi.

Recently kila chombo cha habari kimeshikwa pabaya na serikali, hivyo MillardAyo kama mwanahabari na mtu ambaye maisha yake anayaendesha kutokana na utoaji wake wa habari, lazima achuje taarifa ili kutoripot mambo yatakayomtia matatizoni dhidi ya Serikali.
 

Tz daima si imeondoka na Komu? Au?
 
Haujai kisoda
 
Anzisha chakwako uonyeshe unachotaka tuone ... sio kila mtu Ng’ombe wa kufata mnachotaka nyinyi upinzani uchwara
 
Naona unamwaga povu mpaka linatokea puani!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila tuongee ukweli Lema siku hizi amekua anaongea sana,mengine hayana hata maana wale wadau wa twitter nadhani wataelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna muda naonaga hawa wapinzani nao hawana akili kabisa..

Huyu Lema badala apigie kelele uhuru wa habari in General kwani hakuna chombo chochote cha habari kinachoweza kutoa habari ambazo hazitoipendeza serikali,yeye anamu-attack Millard pekee..huu ni uzwazwa

Kwenye kila taaluma kuna Ethics zake lakini kuna muda Ethical dillema zinatokea..ndo kama hivi..Je Millard aposti hizo habari then afungiwe au aachane nazo atoe taarifa nyingine?
 
Mbona yeye apost anamlalamikia Millard Ayo?
 
Msahuri Lema amwambie Mbowe atunze hela za ruzuku ya miezi 5 tu uone kama hamjaanzisha kituo kama cha Ayo ili miwe mnatqngaza mnachotaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…