Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Godbless Lema ameandika kupitia mtandao wa X (zamani Twitter) amewataka Jambo na Millard Ayo wasiwe na hofu ya kutoa ushahidi wa kweli endapo Jamhuri itawahitaji, akisisitiza kuwa ukweli ndio kinga ya kwanza ya haki na kesi zinazohusu dhamiri ya taifa haziwezi kuachwa zikanyamazishwa.
"Jambo na Millard Ayo msiogope kutoa ushahidi wa kweli kama Jamhuri itawataka. Msiweke wala kukubali masharti ya kificho, kwani ukweli ni kinga ya kwanza ya haki. Hizi kesi siyo za mtu mmoja. Hizi ni kesi za dhamiri ya taifa. Kesho itakuwa ngumu kwa kila mmoja wetu iwapo leo tutanyamaza na kuacha wema na haki vikae kimya katika siku hizi za giza."
"Mpango dhidi ya Mkti Lissu ni mchafu na wenye nia ya kuua matumaini ya wananchi kabisa. Lakini historia imetuonyesha: mara nyingi pale dhuluma inapofika kilele, ndipo wokovu wa Mungu huonekana wazi. Ukiona dhambi ikijisifu na kuonekana kushinda, fahamu mshahara wake hauko mbali"