GE2025 Godbless Lema: Jambo na Millard Ayo msiogope kutoa ushahidi wa kweli kama Jamhuri itawataka. Mpango dhidi ya Lissu ni mchafu na unaua matumaini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Godbless Lema ameandika kupitia mtandao wa X (zamani Twitter) amewataka Jambo na Millard Ayo wasiwe na hofu ya kutoa ushahidi wa kweli endapo Jamhuri itawahitaji, akisisitiza kuwa ukweli ndio kinga ya kwanza ya haki na kesi zinazohusu dhamiri ya taifa haziwezi kuachwa zikanyamazishwa.

"Jambo na Millard Ayo msiogope kutoa ushahidi wa kweli kama Jamhuri itawataka. Msiweke wala kukubali masharti ya kificho, kwani ukweli ni kinga ya kwanza ya haki. Hizi kesi siyo za mtu mmoja. Hizi ni kesi za dhamiri ya taifa. Kesho itakuwa ngumu kwa kila mmoja wetu iwapo leo tutanyamaza na kuacha wema na haki vikae kimya katika siku hizi za giza."

"Mpango dhidi ya Mkti Lissu ni mchafu na wenye nia ya kuua matumaini ya wananchi kabisa. Lakini historia imetuonyesha: mara nyingi pale dhuluma inapofika kilele, ndipo wokovu wa Mungu huonekana wazi. Ukiona dhambi ikijisifu na kuonekana kushinda, fahamu mshahara wake hauko mbali"

​
 
polepole kawaambukiza chawa wa lissu nao eti wanatumia CODE sasa hapo nani kamwelewaanazungumzia nini?
 
Millard Ayo ametumia miaka mingi kujenga brand yake na amefika hapo alipo hapo kwa bidii zake.

Ikiwa Serikali inataka kumtumia itakuwa inafanya makosa wamuache Kijana awe independent
 
Lema sio mjumbe wa Kamati kuu hatambuliwi na msajili hawana haja ya kumsikiliza ushauri wake iwe Ayo wala Jambo Tv au yeyote
 
Nchimbi alishasema, waandish wa habari wengi ni ccm,..
Kwenye hili Mungu muweza atende miujiza lakini tusitegemee hao machawa watutetee.
 
Nabii Godbless katika moja na mbili.
 
Si washasema waandishi wengi wa habari ni chama cha kijani, hivyo wakitaka kuwatumia wanawatumia tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…