Pre GE2025 Godbless Lema kwa heshima aliyojijengea kwenye Taifa hili hawezi kwenda CCM ila haridhishwi na Uongozi wa kaka yake Freeman Mbowe

Pre GE2025 Godbless Lema kwa heshima aliyojijengea kwenye Taifa hili hawezi kwenda CCM ila haridhishwi na Uongozi wa kaka yake Freeman Mbowe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lema anatofauti za wazi kati yake na Katibu wake wa Kanda Bw AMANI Golugwa akimtuhumu kuwa ni fisadi mkubwa ndani ya CHADEMA,

Amani ambae ni swaiba mkubwa wa Freeman Mbowe wa muda mrefu anatajwa kumpigia kampeni za kuchaguliwa tena kwa rafiki yake hiyo aliyedumu madarakani kwa zaidi ya Miaka 30.

Lema kama ilivyo kwa Lissu, Heche na Mnyika hawataki kusikia Freeman Mbowe akirejea madarakani kwani wanaamini sababu ya watu kuuwawa ndani ya chama, kutekwa ndani ya chama ni matokeo ya uongozi wake dhaifu unaojificha kwenye kichaka Cha maridhiano na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amani Golugwa na Freeman Mbowe hawana Cha kupoteza ukizingatia Amani ataendelea kutafuna ruzuku yoyote itakayomfikia na Mbowe atarejeshwa Bunge kwa namna yoyote iwavyo hapa ndipo shida inapoanzia.

Kama Freeman Mbowe atarejea madarakani CHADEMA tutegemee Lemma, Lissu, Mnyika na Heche kuiaga CHADEMA na amakurudi CCM au kuhamia kwenye chama kingine Cha Upinzani.

Soma hii pia Kuelekea 2025 - Vigogo wa CHADEMA Arusha wasema tusishangae Lema akimfata Msigwa, wadai Lema hufanya vikao vya siri na Gambo, Makonda na Msigwa

CCM wanatumia kila aina ya mbinu kuibomoa CHADEMA kabla ya 2025 maana wanajua hiyo ndio salama yao.. Lakini wasichojua CHADEMA ni mpango wa Mungu baba aliye Hai.. Watashindana lakini hawatashinda
Na zito ndio injinia mkuu?! Nimeumia sana kupata habari hii.
 
Leo tarehe 31 Jan, 2025, Lissu ni Mwenyekiti mpya CHADEMA, Mnyika, Katibu Mkuu, Amani Golugwa, N/Katibu Mkuu bara, Heche, Makamu, na Lema , mjumbe wa kamati kuu.
 
Back
Top Bottom