Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Uandikishaji kwenye Daftari la Wapigakura wa Serikali za Mitaa umeanza rasmi leo, tarehe 11 Oktoba, 2024, na utaendelea hadi Oktoba 20, 2024. Hatua hii inampa fursa kila Mwananchi mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. So ni vizuri kutumia siku hizi kumi kujisajili ili kila mmoja aweze kutimiza haki yake ya kikatiba.
Lema, ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Arusha Mjini, alidai kuwa tamasha hilo linaweza kuwa na athari kwa zoezi la uandikishaji. Na kueleza wasiwasi wake kwamba tamasha hilo linaweza kuwakwamisha baadhi ya wananchi wasijiandikishe, na hivyo kushindwa kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga kura ifikapo Novemba 27.
Pia, Soma:
+ Godbless Lema: Kanuni za Uchaguzi 2024 ni za Kihuni, Hatuwezi Kususa, Kamati Kuu Imeazimia Kupambana na Kushinda Uchaguzi
+ Huyu Nabii Geordavie ana utajiri kiasi gani? Ampa Paul Makonda Land Rover zaidi ya 10 huko jijini Arusha!
+ Team Land Rover wapita Mwenge kwa Mbwembwe kuelekea Arusha kwa Makonda kwenye Land Rover Festival
Hata hivyo, jana huko Arusha, Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, alitoa onyo kwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha John Kayombo kuhusu kufanyika kwa tamasha la Land Rover Festival ambalo litafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Oktoba Katikati ya zoezi la uandikishaji.+ Godbless Lema: Kanuni za Uchaguzi 2024 ni za Kihuni, Hatuwezi Kususa, Kamati Kuu Imeazimia Kupambana na Kushinda Uchaguzi
+ Huyu Nabii Geordavie ana utajiri kiasi gani? Ampa Paul Makonda Land Rover zaidi ya 10 huko jijini Arusha!
+ Team Land Rover wapita Mwenge kwa Mbwembwe kuelekea Arusha kwa Makonda kwenye Land Rover Festival