Mtanzania atakayetaka kuichangia CHADEMA atakuwa na matatizo makubwa sana kichwani mwake. Ni bora pesa hizo mtu unayejitambua uwapelekee yatima na wajane huko au watu wenye mahitaji maalumu .
Kwa sababu CHADEMA wamekuwa watu wa kuomba michango miaka na miaka lakini matokeo ya michango hiyo huwa ni giza totoro. Chama kinashindwa hata kulipia kodi ya ofisi huku mikoani au hata kujenga tu ofisi za chama.
Kwa sasa chama kinapokea Riziki ya takribani Million 107. Lakini kilipewa kwa mkupuo zaidi ga Billion 2.7 kama Ruzuku. Pesa zote haieleweki zimekwenda wapi na zimefanya shughuli gani. Ni aibu mpaka leo chama kimeshindwa kuanzisha hata Kituo cha redio au Tv . Matokeo yake tuliona akina lissu waking'ang'ania kwenye Tv za watu za Wasafi FM eti wanataka kufanyiwa mahojiano.
Chama hakina kitega uchumi cha aina yoyote ile .yaani hata biashara ya kuuza sindano tu nguo CHADEMA imeshindwa kubuni.
Sasa michango ndio muarobaini wa shida za CHADEMA? Ndio chanzo cha mapato? Ndio njia ya kukifanya chama kujitegemee? Ndio akili za viongozi wa CHADEMA zilipoishia hapo? Chama cha miaka zaidi ya 30 kinataka kujiendesha kwa michango? Hivi huu siyo udumavu wa akili kweli?