Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Siku ya jana aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini kupitia akaunti yake ya X aliahidi kwamba siku ya leo Tarehe 14 January 2024 atakuwa anazungumza na wanahabari.
Wengi wameshuku kuwa huenda Lema atazungumzia kuhusu Uchaguzi wa CHADEMA na kuainisha ni mgombea gani ya Freeman Mbowe au Tundu Lissu anamuunga mkono.
Kaa karibu na Jamii Forums kupata updates zote
======================================================
- Godbless Lema amesema kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu kwenye nafasi ya Uenyekiti CHADEMA na amemuomba Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe apumzike
Lissu amekuwa Makamu Mwenyekiti, mnadhimu wa Bunge, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, wanaosema hawezi kuwa Mwenyekiti wanataka nani awe?
Kuna watu wanasema Lissu asiwe Mwenyekiti kwasababu hana pesa, sasa niwaambie katika wakati ambao chama kinapaswa kupata kiongozi asiye na hela ni sasa ili wajumbe wajue kuwa chama hakipaswi kuendeshwa kwa pesa za mtu mmoja bali mobilization kutoka kwa watu. CHADEMA inabidi kitafute namba ya ku-rise fund. Kuna watu waliingia kwenye uongozi bila kuwa na pesa"
- Aidha Godbless Lema amesema kuwa hatogombea Ubunge wa jimbo la Arusha Mjini kwenye Uchaguzi wa mwaka 2025
View: https://www.youtube.com/live/n4jGmCXtOsc?si=QELvyU3Ewhqvx9gA