Wakuu,
Siku ya jana aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini kupitia akaunti yake ya X aliahidi kwamba siku ya leo Tarehe 14 January 2024 atakuwa anazungumza na wanahabari.
Wengi wameshuku kuwa huenda Lema atazungumzia kuhusu Uchaguzi wa CHADEMA na kuainisha ni mgombea gani ya Freeman Mbowe au Tundu Lissu anamuunga mkono.
Kaa karibu na Jamii Forums kupata updates zote
======================================================
"Mimi Mbowe ni kaka yangu, tunajuana. Yeye ni Mchaga na mmachame kama mimi, na familia zetu zinafahamiana, ila kwa uchaguzi ujao wa Mwenyekiti namuomba amuachie Tundu Lissu.
Lissu amekuwa Makamu Mwenyekiti, mnadhimu wa Bunge, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, wanaosema hawezi kuwa Mwenyekiti wanataka nani awe?
Kuna watu wanasema Lissu asiwe Mwenyekiti kwasababu hana pesa, sasa niwaambie katika wakati ambao chama kinapaswa kupata kiongozi asiye na hela ni sasa ili wajumbe wajue kuwa chama hakipaswi kuendeshwa kwa pesa za mtu mmoja bali mobilization kutoka kwa watu. CHADEMA inabidi kitafute namba ya ku-rise fund. Kuna watu waliingia kwenye uongozi bila kuwa na pesa"
View: https://www.youtube.com/live/n4jGmCXtOsc?si=QELvyU3Ewhqvx9gA