Pre GE2025 Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huwa watu mnawezaje kua wanafiki?? Yaan unakuja kuaje.

Mfano, Yote Lema aloongea, lkn wewe unatoka kusema, Watu walitaka kumng'oa Mbowe?.


Huwa ni Ujinga na matope ndio yamejaa kichwan au
 
Wamachame wabinafsi sana,hawawapendi hata wachaga wa jamii zingine,pale njia panda machame,barabara ya arusha,kuna maduka ya vibanda ni wamachame tupu,hadi boda,ukienda mchaga wa jamii nyingine unaibiwa vitu vyako vyote,unaweza usiuze hata 100.
ukipeleka daladala yako machame to moshi mjini,hupati hata abiria mmoja kama sio mmachame..
Ni kweli Machame kuna huo upumbavu, na hata Kibosho pia
 
Jacob Zuma alimshinda Thabo Mbeki kwenye Urais wa ANC.

Wanaoamini Lisu ndio anakubalika wafunge midomo wawaache wajumbe wamchaguwe wanayemtaka.

Haya mambo ya kuachiana madaraka mngeyafanya mapema kwenye vikao vya kamati kuu na siyo unachukuwa fomu halafu unasema uachiwe ebo!
alimshindaje bila mdomo
 
Tatizo la Lisu kichwa chake hakijatulia.

Mbowe naye kachoka kwakweli sina tatizo naye apumzike tu.

Chadema inahitaji damu mpya ila wahusika walikosea kutoandaa warithi mapema.

Viongozi wetu wapunguze ubinafsi, nchi ni yetu sote.

Mtu huwezi kaa sehemu moja milele, kupeana nafasi iwe utamaduni wetu wa kudumu.

Hakuna mtu anaweza jimilikishia kitu milele.
Leo stroke umenena
 
Lema ni msaliti. Huyu ni mchaga aliyelogwa na mnyampaa
Kwa hiyo wewe akili ndogo na chawa wa Samia unataka Lema amuunge mkono Mbowe kisa ni mchagga. Wewe angalia ya chama chenu hicho ambacho mwenyekiti ni mfalme ambaye anapitishwa kwa shangwe na nderemo na machawa wake. Bure kabisa.
 
Wakuu,

Siku ya jana aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini kupitia akaunti yake ya X aliahidi kwamba siku ya leo Tarehe 14 January 2024 atakuwa anazungumza na wanahabari.

Wengi wameshuku kuwa huenda Lema atazungumzia kuhusu Uchaguzi wa CHADEMA na kuainisha ni mgombea gani ya Freeman Mbowe au Tundu Lissu anamuunga mkono.

Kaa karibu na Jamii Forums kupata updates zote

======================================================

  • Godbless Lema amesema kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu kwenye nafasi ya Uenyekiti CHADEMA na amemuomba Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe apumzike
"Mimi Mbowe ni kaka yangu, tunajuana. Yeye ni Mchaga na mmachame kama mimi, na familia zetu zinafahamiana, ila kwa uchaguzi ujao wa Mwenyekiti namuomba amuachie Tundu Lissu.

Lissu amekuwa Makamu Mwenyekiti, mnadhimu wa Bunge, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, wanaosema hawezi kuwa Mwenyekiti wanataka nani awe?

Kuna watu wanasema Lissu asiwe Mwenyekiti kwasababu hana pesa, sasa niwaambie katika wakati ambao chama kinapaswa kupata kiongozi asiye na hela ni sasa ili wajumbe wajue kuwa chama hakipaswi kuendeshwa kwa pesa za mtu mmoja bali mobilization kutoka kwa watu. CHADEMA inabidi kitafute namba ya ku-rise fund. Kuna watu waliingia kwenye uongozi bila kuwa na pesa"


  • Aidha Godbless Lema amesema kuwa hatogombea Ubunge wa jimbo la Arusha Mjini kwenye Uchaguzi wa mwaka 2025



View: https://www.youtube.com/live/n4jGmCXtOsc?si=QELvyU3Ewhqvx9gA

Mwenyekiti Freeman Mbowe,azingatie sana ushauri huu wa Lema,huyu sasa ni nabii na ushauri huu ni ushauri wa kinabii!
P
 
Back
Top Bottom