Godbless Lema ndiye mwenyekiti ajaye wa CHADEMA

Godbless Lema ndiye mwenyekiti ajaye wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Makupa

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
6,822
Reaction score
4,034
Nimekuwa nafuatailia siasa za hiki Chama takriban miaka ishirini iliyopita. Kama sikosei hiki chama nafasi ya Mwenyekiti imewahi kuwa na wenyeviti watatu ambao wawili kati yao ni mtu na Mkwe wake yaani Freeman Mbowe na Mzee Edwin Mtei.

Kutokana na kelele nyingi saana toka ndani ya chama kutaka awepo mwenyekiti mwingine asietokana na uridhi wa kindugu, Mwenyekiti ambaye kwa sasa yupo mahabusu amekuwa na mawasiliano ya karibu saana na baadhi ya viongozi wa kanda wa chama kwa nia ya kuhakikisha ya kwamba mrithi wake anatokana na safu wa viongozi wa kanda waliopo. Msingi haswa wa kutaka viongozi wa kanda ni kutaka kuhakikisha ya kuwa mheshimiwa Lissu ambae ni Makamu Mwenyekiti hataweza kumrithi Mheshimiwa Mbowe kwenye uachaguzi ujao wa chama.

Wadadisi wa maswala ya uchaguzi wanaamini ya kwamba kwa viongozi wa Kanda waliopo kwa sasa, Mrithi halisi na ambae aataweza kuendeleza dhana ya chama (chgga kwanza) ni Mheshimiwa Godbless ambae amekuwa active saana kwenye mitandao ya kijamii kwa nia ya kuhakikisha ya kwamba anaonekana na vijana wa chama kuwa ni jasiri na SHUPAVU hivyo anaweza kuwa mtu sahihi kumrithi kaka mheshimwa Mbowe ambae ni binadmu yake LEMA.

Nawasilisha wakuu
 
Wakimuweka mwenyekiti kutoka kaskazini watajifuta katika ramani za siasa za Tanzania.

Ukweli unaoujua, ndio utakaokuweka huru. Kwa sasa ardhi inahitaji uongozi, kuliko kitu chochote. Candidate yeyote atakayekuwa na sura ya utaifa na uzalendo, wananzengo wanampa. Maana kusema ukweli wamechoka. Sasa ushauri wangu kwa hawa makamanda ambao inaonekana wamekuwa katika ligi kwa miaka mingi, wanahitaji kujiimarisha ili wakidhi vigezo vinavyohitajika.

1. Wanahitaji kuondoka dhana ya jumuiya ya mahala ama utamaduni mmoja. Badala yake wachukue dhana ya Mwalimu Nyerere ya kuunganisha na kuwa na taifa moja lisilo na ubaguzi.

2. Wakubali na watambue kwamba matunda ya vita kama vile athari zake huwa ni kwa manufaa ama hasara ya taifa zima. Kwa msingi huo, wasijione kwamba wao wanastahiki keki kubwa zaidi ya uhuru kwa kuwa wamedhikika ama wamepambana mstari wa mbele, bali wajue uhuru wa kila eneo ni haki ya watu wote.

3. Ili kutimiza hayo, wathibitishe kwamba hawatakuwa watu wa visasi kama wataliban wa afghanistani ambao hatima yake ni kusababisha chuki, uchungu na vurugu zisizokoma.

4. Wahakikishe, ( hili ni la lazima), uongozi wa juu unagawanywa kwa watu mchanganyiko kktoka sehemu mbali mbali za nchi na tamaduni tofauti. Kuanzia ngazi ya juu, idara na kamatimbali mbali.

5. Waonyeshe uwezo na mwelekeo bora kuliko yaliyopo sasa.

Kwa kuendeleza mfumo wa kaskazini, bavicha, bawacha, taifa, sijui nini na nini kila mahala wakuu wa kaskazini, wengine wanatupiwa tupiwa tu kama mapambo, hapana. Hatufiki.
 
Ukweli unaoujua, ndio utakaokuweka huru. Kwa sasa ardhi inahitaji uongozi, kuliko kitu chochote. Candidate yeyote atakayekuwa na sura ya utaifa na uzalendo, wananzengo wanampa...
Hiki chama ni sikio la kufa mkuu ,kuhusu viongozi toka kanda ya kaskazini hawoni wala kusikia ,naamimi kabisa hiki chama ndio kingestahili kuwa mshirika wa serikali kule Zanzibar ,ila baada mareheme Seif kuwapa masharti kuwa ni lazima moja wa viongozi wakuu wa kitaifa atoke Zanzibar wahafidhina wa chama wakagoma .Matokea yake leo ACT wana nguvu kwenye siasa a nchi kuliko CDM
 
Waache CDM na mambo yao, CDM ikifa wewe utapata hasara gani?
 
Mkuu hifadhi huu Uzi ,subiri tuone mwakani 2023,hutaamini
Bora atoke tu kaskazini mradi kama ni mtu shupavu. Siyo hawa waunga juhudi mkono.

Kilichofanywa na katibu Dr Mashinji, na aliyegombea uenyekiti mara ya mwisho , yule mbunge alierudishwa bungeni na Ndugai baada ya kujiuzulu. Bora mtu strong hata kama ni wa Ukerewe . Siyo waunga juhudi
 
Tatizo kubwa ndani ya CHADEMA wenye njaa wengi sana,wale wenye misimamo ndo wanafaa kupewa kijiti Cha uenyekiti.
Lema,Heche,Mbilinyi,Msigwa na Mnyika.tofauti na hapo yatakuwa yaleyale ya akina Zitto
 
Nimekuwa nafuatailia siasa za hiki Chama takribani miaka ishirini iliyopita. Kama sikosei hiki chama nafasi ya Mwenyekiti imewahi kuwa na wenyeviti watatu ambao wawili kati yao ni mtu na Mkwe wake yaani Freeman Mbowe na Mzee Edwin Mtei...

Nawasilisha wakuu
Shughulìkèni nà MATUNGURI si Chadema ilisha kufa?
 
achana na mwenyekiti Taifa, Kwa sasa kuna vita kali sana inayokwenda chini kwa chini juu ya Mwenyekiti mpya wa BAWACHA.

Yule dada wa Kipemba itambidi tu akae pembeni pale.
 
Nimekuwa nafuatailia siasa za hiki Chama takribani miaka ishirini iliyopita. Kama sikosei hiki chama nafasi ya Mwenyekiti imewahi kuwa na wenyeviti watatu ambao wawili kati yao ni mtu na Mkwe wake yaani Freeman Mbowe na Mzee Edwin Mtei.

Kutokana na kelele nyingi saana toka ndani ya chama kutaka awepo mwenyekiti mwingine asietokana na uridhi wa kindugu, Mwenyekiti ambaye kwa sasa yupo mahabusu amekuwa na mawasiliano ya karibu saana na baadhi ya viongozi wa kanda wa chama kwa nia ya kuhakikisha ya kwamba mrithi wake anatokana na safu wa viongozi wa kanda waliopo. Msingi haswa wa kutaka viongozi wa kanda ni kutaka kuhakikisha ya kuwa mheshimiwa Lissu ambae ni Makamu Mwenyekiti hataweza kumrithi Mheshimiwa Mbowe kwenye uachaguzi ujao wa chama.

Wadadisi wa maswala ya uchaguzi wanaamini ya kwamba kwa viongozi wa Kanda waliopo kwa sasa, Mrithi halisi na ambae aataweza kuendeleza dhana ya chama (chgga kwanza) ni Mheshimiwa Godbless ambae amekuwa active saana kwenye mitandao ya kijamii kwa nia ya kuhakikisha ya kwamba anaonekana na vijana wa chama kuwa ni jasiri na SHUPAVU hivyo anaweza kuwa mtu sahihi kumrithi kaka mheshimwa Mbowe ambae ni binadmu yake LEMA.

Nawasilisha wakuu
Mataputapu haya
 
Mwenyekiti ni Freeman A. Mbowe acheni chokochoko za kutafuta madaraka...ikumbukwe tu, sumu haijaribiwi kwa kulambwa !
 
Mwenyekiti ni Freeman A. Mbowe acheni chokochoko za kutafuta madaraka...ikumbukwe tu, sumu haijaribiwi kwa kulambwa !

Msigwa anafaa.
Nako kusini kupate mtu. Angalau kusawazisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom