Ukweli unaoujua, ndio utakaokuweka huru. Kwa sasa ardhi inahitaji uongozi, kuliko kitu chochote. Candidate yeyote atakayekuwa na sura ya utaifa na uzalendo, wananzengo wanampa. Maana kusema ukweli wamechoka. Sasa ushauri wangu kwa hawa makamanda ambao inaonekana wamekuwa katika ligi kwa miaka mingi, wanahitaji kujiimarisha ili wakidhi vigezo vinavyohitajika.
1. Wanahitaji kuondoka dhana ya jumuiya ya mahala ama utamaduni mmoja. Badala yake wachukue dhana ya Mwalimu Nyerere ya kuunganisha na kuwa na taifa moja lisilo na ubaguzi.
2. Wakubali na watambue kwamba matunda ya vita kama vile athari zake huwa ni kwa manufaa ama hasara ya taifa zima. Kwa msingi huo, wasijione kwamba wao wanastahiki keki kubwa zaidi ya uhuru kwa kuwa wamedhikika ama wamepambana mstari wa mbele, bali wajue uhuru wa kila eneo ni haki ya watu wote.
3. Ili kutimiza hayo, wathibitishe kwamba hawatakuwa watu wa visasi kama wataliban wa afghanistani ambao hatima yake ni kusababisha chuki, uchungu na vurugu zisizokoma.
4. Wahakikishe, ( hili ni la lazima), uongozi wa juu unagawanywa kwa watu mchanganyiko kktoka sehemu mbali mbali za nchi na tamaduni tofauti. Kuanzia ngazi ya juu, idara na kamatimbali mbali.
5. Waonyeshe uwezo na mwelekeo bora kuliko yaliyopo sasa.
Kwa kuendeleza mfumo wa kaskazini, bavicha, bawacha, taifa, sijui nini na nini kila mahala wakuu wa kaskazini, wengine wanatupiwa tupiwa tu kama mapambo, hapana. Hatufiki.