Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Katika ukurasa wake wa X(Twitter) Godbless Lema kaandika,
"Baba Askofu (picha ya Askofu Malasusa) Bwana Yesu asifiwe sana. Pole na kazi ya Mungu. Huku Arusha tunaendelea vizuri kiasi na watu wanaendelea kusubiri TAMKO la Kanisa unaloliongoza wewe juu ya ukatili mkali huko NGORONGORO na Utekaji na utesaji dhidi ya raia. Msalimie sana YESU."
Hiki ni kiburi.
Namshauri Lema kwa ukurasa huo huo aombe radhi kwa kuwaona watumishi wa Kanisa kuwa political sparring partners.
Mbaya zaidi kulifedhesha na kudhihaki Jina lipitalo majina yoye, YESU.
Asipofanya hivyo hizo salamu anazozitafuta atazipata, na si muda mrefu.