Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Godbless Lema ametangaza ujio wa uzinduzi wa kampeni ya kidigitali ya Chama hicho utakaofanyika February 27,2025.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo February 25,2025, Lema amesema
“Tarehe 27 tuna tukio muhimu Chama chetu kinakwenda kuzindua, Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Kamati ya Fedha ya Chama ambacho Chama kiliitengeneza tulipokuwa Bagamoyo, tunaenda kuzindua mkakati wetu wa kidigitali, ni mkakati ambao wenzetu watashangaa kwasababu tumewaacha mbali sana akina Mzee Wasira, akina Mzee Nchimbi hawawezi kufanana na think tank yetu katika kufikiri mambo ambayo tutakwenda kuzindua kuanzia tarehe 27 saa 12 jioni hadi saa nne usiku”
“Kesho Wakurugenzi Viongozi wetu wa Habari watawasambazia ujumbe kwamba jambo hilo litafanyika ukumbi gani, tunaomba Waandishi mkaribie na mkiweza kwenda Live kuanzia mwanzo wa tukio hadi mwisho mtakuwa mmefanya vizuri sana, hili tukio litafuatiliwa Dunia nzima”
“Tunazindua tukio maalum la kufanya kampeni kidigitali na mambo mengine ambayo mtaona siku hiyo, Mwenyekiti wetu Tundu Lissu atakuwa Mgeni rasmi, mwaliko huu ni wa Wananchama wote Nchi nzima”
“Baada ya uzinduzi wa kampeni kutakuwa na shughuli nyingine za kisiasa na kuitangaza hii movement, siku hiyo Mwenyekiti wetu wa Chama Taifa anaweza kuwagusia kidogo mikakati yetu mingine ya Kimataifa, kwahiyo ninawakaribisha Waandishi, Wana CHADEMA, namkaribisha hata Nchimbi au Wasira kama hivi wanaviangaliaga kama atakuwa hajalala wakati huo, nakaribisha kila Mtu kwamba tutakuwa na tukio tareh 27”