Godfrey Malisa: Nitakwenda mahakamani kupinga kuvunjwa kwa katiba ya CCM na ya nchi kwa yaliyotokea Dodoma

Godfrey Malisa: Nitakwenda mahakamani kupinga kuvunjwa kwa katiba ya CCM na ya nchi kwa yaliyotokea Dodoma

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Mwana CCM GODFREY MALISA ameamua kusema ukweli.

"Sasa hivi tayari inafahamika kwamba Chama cha Mapinduzi katika Mkutano wake Mkuu kilipitisha kwa kauli moja na kumtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM, jambo hili nilipolisikia sikuamini kwamba tumefikia hapa kwanini?, kwasababu CCM ni chama makini, ni chama kinachoheshimu demokrasia, ni chama kinachozingatia demokrasia na katiba ya nchi, haijawahi katika historia ya chama cha mapinduzi kufanyika haya yaliyofanyika leo (tarehe 19/1/2025), kitu cha ajabu kabisa, ninasikitika kwamba tunawezaje kufika mahali hapa kwa wazi wazi Chama kinacho heshimu demokrasia kuwanyima Wanachama wanaotaka kugombea nafasi ya Urais wa nchi kwa mujibu wa katiba ya CCM na kwa mujibu wa Katiba ya Nchi.."



1. Kwa mahakama za Juma hupati lolote, I am sorry for this statement

2. Naogopa ya Kibao!
 
Angeenda mahakamani kimya kimya tu angooneka yupo serious na akifanyacho.

Hili la kutoa tangazo ni igizo tu kama la Hashimu Rungwe kuandaa pilau kwa wapiga kura....

Wajinga bado hawataisha bongo.
 
Ataokotwa kwenye fukwe za Ziwa Tanganyika au pengine Hatutamsikia tena.
 
Wajumbe wamempitisha dkt Samia Suluhu Hasana kuwa mgombea pekee kupitia CCM, hakuna zaidi ya Samia, mzee Malisa acha kupoteza muda wako bure.
Hakuna mwana CCM yeyote ambaye yuko tayari kugombea zaidi ya Samia.
kama una wivu na chuki kunywa sumu ufeeee.
Samia mitano tenaaaaaa
 
Back
Top Bottom