Godfrey Polepole awataja wahusika wa mauaji ya Oktoba 29. Ashauri Serikali isimalize pesa kwenye Tume ya Jaji Lila

Godfrey Polepole awataja wahusika wa mauaji ya Oktoba 29. Ashauri Serikali isimalize pesa kwenye Tume ya Jaji Lila

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
7,748
Reaction score
10,288
Ujumbe huu hapašŸ‘‡

Nukuu ya alichokisema Godfrey Polepole
"Ningependa kusema mamlaka za Tanzania zimuachilie huru Balozi Humphrey Polepole. Hilo ni la kwanza.

La pili, nataka kumwambia Mama Samia Suluhu Hassan, Mama Samia usipoteze pesa ambazo ni kodi za Watanzania kwa ajili ya kuwalipa makamishna ambao umewateua leo hii kwa takribani muda wa miezi mitano kwa ajili ya kuifanya kazi ya kufanya uchunguzi ya wakina nani ambao walihusika kwenye matukio ya kabla na baada ya tarehe 29.

Mimi nitapenda kukufahamisha wahusika wakuu kadhaa ambao watakupatia majibu ya matukio ya kabla na baada ya Oktoba 29, 2025.

Mtu wa kwanza kabisa ambaye mimi ninakuambia sasa Mama Samia atakusaidia kupata majibu na usipoteze hizo fedha za Watanzania, mtu wa kwanza ni yule aliyekata intaneti kuanzia siku ile ya tarehe 29 mpaka kwa mfululizo wa zaidi ya siku nne. Yule ukimpata, atakwambia kwa nini alizima intaneti, alikuwa anaficha nini katika ulimwengu mzima ama duniani taarifa zisitoke kwa wakati. Sasa yule ukimpata, atakupa majibu kwa nini alizima mtandao wa intaneti.

Mtu wa pili ambaye atakupatia majibu yaliyostahili ni afisa wako wa polisi ZCO anayetambulika naye kwa jina la Faustine Jackson Mafwele. Huyu bwana, yeye alideclare, alitambua pingu zilizomfunga David Jumbe, msaidizi binafsi wa Mheshimiwa Tundu Antiphas Lissu. Alizitambua pingu zile baada ya ndugu Jumbe kuwa ametekwa. Kwa hiyo Faustine Mafwele akatambua pingu zile kwamba anazifahamu ni pingu ngumu sana. Kwa hiyo huyu naye ukimpata, atakuelezea vizuri ni akina nani ambao walihusika katika kufanya utekaji, ikihusisha pamoja na utekaji wa ndugu David Jumbe.

Mtu wa tatu ambaye atakusaidia kuweza kujua matukio hayo kabla na baada ni mkuu wako wa mkoa anayetambulika naye kwa jina la Albert Chalamila. Huyu ndiye mkuu ama ndiye mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Dar es Salaam. Sasa huyu naye ukikaa naye chini ukaongea naye vizuri, atakwambia ni akina nani wanaofanya matukio ya kihalifu katika mkoa wa Dar es Salaam.

Mtu wa nne ambaye atakusaidia jambo hili, muite kaa naye karibu, ni IGP wako Camillus Wambura. Huyu atakusaidia kuweza kujua ni akina nani walioruhusu polisi wapewe silaha AK-47 kwenda kuwamiminia marisasi raia wasiokuwa na hatia. Polisi walipiga risasi raia wasiokuwa na hatia. Kwa hiyo Camillus Wambura atakwambia ni nani aliyewaruhusu polisi kuchukua silaha za kivita na kwenda kuwapiga marisasi raia wasiokuwa na hatia. Na huyu pia atakwambia ni akina nani ambao waliwalipa polisi ili wakawapige risasi za moto raia.

Kwa hiyo kwa kufanya hayo Mama Samia Suluhu Hassan, utaokoa kiasi kikubwa sana cha fedha ambazo ungetumia kuwalipa hao makamishna. Kwa kuchukua rekodi kutoka kwa hawa watu niliyokutajia, utapata majibu yaliyokuwa genuine kabisa na utaweza kujua unaanzia wapi na kuweza kushughulika na nani.
Kwa hiyo mimi nikutakie majukumu mema na ufuatiliaji mzuri wa mambo haya. Na kwa kusema hivyo, mimi niwatakie wakati mwema Watanzania."
 
Mama Samia usipoteze pesa ambazo ni kodi za Watanzania kwa ajili ya kuwalipa makamishna ambao umewateua leo hii kwa takribani muda wa miezi mitano
Sahihi,
Ni ufujaji wa fedha za Watanganyika kwa mambo yasiyo na maana
 
Mhusika mkuu wa mauaji ni CIC kwani mauji yalitekelezwa na majeshi ya ulinzi na usalama.
 
Huyo dogo anazunguka sana, anayeunda tume ndio mtu wa kwanza na wanajua kila kitu ila hizi tume kiini macho tu.
Mimi mwenyewe nimeshangaa anamnyooshea kidole mbwa wakati mwenye mbwa, aliyemtuma mbwa, anamjua?
 
Mimi mwenyewe nimeshangaa anamnyooshea kidole mbwa wakati mwenye mbwa, aliyemtuma mbwa, anamjua?
Huyu dogo kunguru muoga, mwenye mbwa kwasasa anacheza na akili za watanzania kuunda tume juu ya tume ili wajipange upya 2030

Nilisema CCM wanatugeuza chapati wanatupindua pindua wanavyotaka wao
 
Watanzania wote matako yetu! Upumbavu mtupu! Tunamwunga mkono muuaji?
 
Back
Top Bottom