Godlisten Malisa akamatwa tena na Jeshi la Polisi na kusafirishwa mkoani Kilimanjaro

Godlisten Malisa akamatwa tena na Jeshi la Polisi na kusafirishwa mkoani Kilimanjaro

Huyu mchaga ana dharau sana, alianza kutoa vimeseji vya kutukana viongozi kwa dharau kubwa, yaani bado hajasema.

Hajui kwamba kuna post alitoa akimsingizia Waziri kuhusika na kumficha muuwaji huko Rombo. Watu wakamkaushia tu, sasa ataenda kumenya karanga kwenye mtondoo huko Gereza la Karanga. Na jimbo analolitaka atalipata akiwa segere matata, hukumu 2025 August 2025
Mkuu kumbe!!!
 
Huyu jamaa watamsumbua sana.
Kama vipi ajiondokee TZ..
 
Viongozi na wafuasi wa CDM wanakinga yakutokamatwa na jeshi la Polisi.

Nimewaza tu maana nimeona kila akikamatwa mfuasi au kiongozi wa CDM tayari ni kama tunakimbilia kuhusisha na mambo ya siasa.

Tutambue tu hawa nao ni raia tu kama sisi wana tabia na maisha yao nje ya hizi siasa.
 
Kesi namba 11805/2024 inayomkabili aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob na Godlisten Malisa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Saalam limeahirishwa hadi tarehe 04 Julai 2024 ambapo usikilizwaji wa awali wa shauri hilo utaanza.

Baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Jeshi la Polisi limemkamata Godlisten Malisa kwa kile walichodai ana shitaka jipya mkoani Kilimanjaro. Asubuhi hii Jeshi hilo limeanza safari ya kumpeleka Mkoani Kilimanjaro.

Pia soma
- Mauaji ya Robert Mushi ndugu wa aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob polisi wanahusika?

- Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

- Utata sakata la ndugu wa Boniface Jacob: Kupotea mpaka kukutwa mochwari ya polisi, Amana wapigilia msumari!

- Boniface Jacob na Godlisten Malissa Wafikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

- Hatimaye Malissa na Boniface Jackob waachiwa kwa dhamana
walimchochea nani na nani kachocheka
 
Trump ana makosa ya kutaka kupindua matokeo ya Urais pamoja kuiba nyaraka za siri za serikali ya Marekani lakini hajawahi kukamatwa uchunguzi wa hizi tuhuma zake ukifanyika, sasa huyu Malisa ana makosa gani makubwa zaidi ya haya??

Unajua sifa ya kuwa Polisi Tanzania? Ukilijua hilo, huwezi kushangaa.
 
Kesi namba 11805/2024 inayomkabili aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob na Godlisten Malisa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Saalam limeahirishwa hadi tarehe 04 Julai 2024 ambapo usikilizwaji wa awali wa shauri hilo utaanza.

Baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Jeshi la Polisi limemkamata Godlisten Malisa kwa kile walichodai ana shitaka jipya mkoani Kilimanjaro. Asubuhi hii Jeshi hilo limeanza safari ya kumpeleka Mkoani Kilimanjaro.

Pia soma
- Mauaji ya Robert Mushi ndugu wa aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob polisi wanahusika?

- Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

- Utata sakata la ndugu wa Boniface Jacob: Kupotea mpaka kukutwa mochwari ya polisi, Amana wapigilia msumari!

- Boniface Jacob na Godlisten Malissa Wafikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

- Hatimaye Malissa na Boniface Jackob waachiwa kwa dhamana

Sababu ya Malisa kupelekwa Kilimanjaro soma:

- Adolf Mkenda atajwa kuwa chanzo cha Godlisten Malissa kukamatwa tena

- Aliyemchoma Mwanamke visu 25 na kumsababisha Kifo afariki dunia akiwa chini ya ulinzi
#Updates
Usiku huu @MalisaGJ_ amefikishwa Moshi mjini, na Jeshi la Polisi limempeleka moja kwa moja ofisi ya RCO. Wakili Peter Kidumbuyo ameambatana na Malisa katika mahojiano hayo.
 
Back
Top Bottom