Godlisten Malisa: Ili tuweze kusafirisha umeme sisi wenyewe kwa tija inabidi tujenge vituo vya kupozea njiani

Godlisten Malisa: Ili tuweze kusafirisha umeme sisi wenyewe kwa tija inabidi tujenge vituo vya kupozea njiani

Comment ya kwanza kakudanganya, ila nikueleze serikali ilishatoa maelezo nadhani hufatilii.
Tanzania ni mwanachama wa
southern africa power
Eastern Africa power
Kuna miundombinu ya moja kwa moja kama kenya tz interconnect na ule tz zambia interconnect.
Tanzania ina njia kuu zinazotoka iringa, shinyanga na mbeya, ambazo zinaunganishwa na njia za kimataifa, ili kusafirisha kwa wenzetu majirani,
Ila nikuibie siri baada ya yote. Tanzania ipo kwenye mradi wa backbone transmission line.
Hizo njia zikitumika kutoa umeme Rufiji kwenda Arusha na Kilimanjaro nguzo zinaungua?
Yaani watu wa Ethiopia wao wanazalisha umeme kwa kutumia mchanga ambao TANESCO hawawezi kuwatuma wataalam wao wakajifunze namna ya kuzalisha umeme ambo ata ikipotea bado wanabaki na faida.
 
PINGAMIZI DHIDI YA HOJA YA MALISA KUHUSU UAMUZI WA TANZANIA KUHEMEA UMEME UGHAIBUNI: KAWADANGANYE WATU WALIOSOMA UNGWINI

View attachment 3269288
Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko

Katika pingamizi hili napendekeza kwamba, kadiri jukumu la kuzalisha na kusambaza umeme kwa kutumia tekinolojia ya kisasa linavyohusika, uamuzi wa serikali ya Tanzania kuhemea umeme kutoka ughaibuni, hapa katika zama za "post-Stigler's Gorge," ni ushahidi tosha kwamba serikali haikutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa wakati, na sasa inahaha kuokoa jahazi.

Kimsingi, maelezo ya Malisa kuhusu nishati ya umeme yamenikumbusha Mwalimu wangu wa Fizikia, Dr. Kiwanga, Idara ya Fizikia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alinifundisha Kanuni ya Ohm kuhusu usafirishaji wa umeme, yaani Ohms Law. Kanuni hii inasema kwamba:

(1) V=IR;

(2) R=(r*L)/A;

(3) I=(V/R) kutokana na (1);

(4) P=I*I*R;

(5) P= (I*I*r*L)/A;

(6) P=(V*V)/R kutokana na (3) na (4);

(7) P=(V*V*A)/(r*L) kutokana na (2) na (6).

Ambapo:
  • V=Volti/Voltage
  • I=Mkondo wa umeme/Current
  • R=Ukinzani/Resistance
  • P=Nishati ya joto inayozalishwa na umeme mkondoni/Dissipated Power
  • r=Kiini-ukinzani/Resisitivity
  • A=Eneo mkingamo katika waya wa umeme/cross-sectional area
Kimantiki, kuna mahitimisho mawili kutokana na formula hizi.

Mosi, kutokana na formula namba (5) ni wazi kwamba, kadiri umbali wa kusafirisha umeme unavyoongezeka nguvu yake inayopotea inaongezeka.

Yaani, “dissipated power is directly proportional to distance and current.”

Hii maana yake ni kwamba, ili tuweze kusafirisha “umeme wa mkondo-geu” kutoka bwawa la Nyerere au Mtera hadi Arusha bila kupotea sana, inabidi kujenga, sio vituo vya kupozea umeme wa mkondo-geu njiani (step-down transformer substations) kama Malisa anavyodai kimakosa, bali tunapaswa kujenga vituo vya kukuzia umeme (step-up transformer substations).

Na pili, kutokana na formula namba (7) ni wazi kwamba, kadiri umbali wa kusafirisha umeme unavyoongezeka nguvu yake inayopotea inapungua.

Yaani, “dissipated power is directly proportional to voltage and inversely proportional to distance.”

FomuLa hii inahusiana na tekinolojia ya kusafirisha umeme wa mkondo-mnyoofu ambao hauna uhusiano wowote na transfoma-pozo wala transfoma-chocheo.

Tekinolojia hii inaitwA “High Voltage Direct Current (HVDC) Transmission Lines.”

Malisa hajaongelea kitu kuhusu mkono huu wa mjadala kwa makusudi, maana unafichua uzembe wa serikali.

Tanzania inahitaji kuwekeza zaidi katika tekinolojia ya HVDC.

Ukweli ni kwamba HDVC za masafa marefu zinaweza kupunguza upotevu wa umeme kwa sababu kadiri umbali unavyoongezeka upotevu wa umeme unapungua kwa mujibu wa fomula namba (7) hapo juu.

Kwa hiyo, uamuzi wa Tanzania kuhemea umeme kutoka ughaibuni ni Ushahidi kwamba Wizara ya Nishati haikutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa wakati, na sasa inahaha kuokoa jahazi.

Na mpaka hapo hakuna "ufafanuzi wa ufafanuzi" utakaoweza kunibadilisha mawazo isipokuwa maelezo ya kwanini serikali ilipuuzia tekinolojia ya HDVC.

Na ninamwomba Malisa ajitokeze na kujibu pingamizi langu.
Hawezi maana kama mimi nimeelewa kwa shida sana mchaga yule alivyo na kichwa kigumu Sidhani.
 
By Malisa GJ,

Kwanza, ieleweke kuwa hili si jambo geni. Hii si mara ya kwanza kununua umeme nje ya nchi. Tunanunua umeme kutoka Zambia kwa ajili ya mkoa wa Rukwa, kutoka Uganda kwa ajili ya mkoa wa Kagera, na kutoka Kenya kwa ajili ya wilaya ya Mkinga, Tanga.

Pili, watanzania tunahoji kwanini tununue umeme nje wakati tuliambiwa bwawa la Nyerere likikamilika tutakuwa na umeme wa kutosha na tutaweza kuuza nje. Je, tulidanganywa?

Ili kujibu swali hilo ni muhimu kujua hali ya uzalishaji wa umeme nchini na vyanzo vyake. Vyanzo vya umeme wa maji (hydroelectric power plants) tulivyonavyo vina uwezo ufuatao:
  • Kidatu inazalisha 204 MW
  • Kihansi 180 MW
  • Mtera 80 MW
  • Hale (Tanga) 68 MW
  • Rusumo 80 MW
  • Julius Nyerere 2,115 MW
  • Nyumba ya Mungu 8 MW

Kwa hiyo, kupitia vyanzo vya maji tuna uwezo wa kuzalisha 2,735 MW. Mahitaji ya umeme nchini yanakadiriwa kuwa 2,200 MW. Hii ina maana kwamba tuna ziada ya karibu 500 MW ambazo tunaweza kuuza nje. Kwa hiyo hatujadanganywa. Umeme wa kuuza nje upo.

Sasa, kwanini tununue umeme nje wakati ndani tuna ziada? Jibu ni kwamba usafirishaji wa umeme unasababisha upotevu njiani. Kusafirisha umeme si sawa na kusafirisha mbaazi. Ukitoa mbaazi Moshi zikiwa 50Kgs, zikifika Dar zitakua hizohizo 50Kgs. Lakini kwa Umeme ni tofauti. Kadri unavyosafirisha umbali mrefu, ndivyo unavyopotea.

Je, kati ya Ethiopia na bwawa la Mwalimu Nyerere, wapi mbali? Kama tunahofia umeme ukisafirishwa kutoka bwawa la Nyerere hadi Arusha utapotea, je unaotoka Ethiopia si utapotea zaidi?

Jibu ni kwamba Tanzania haitahusika na usafirishaji wa umeme huo kutoka Ethiopia. Sisi tutahusika baada ya kuupokea Namanga. Kwa hiyo, kama ni usafirishaji, sisi tutaanzia Namanga kwenda Arusha. Kwahiyo pale Namanga tukipokea 100MWs tutazifikisha Arusha bila kupotea maana ni karibu.

Kwa lugha rahisi, ni sawa na kuwa na chanzo kipya cha umeme Namanga. Kwa hiyo ni ukweli kwamba kusafirisha umeme kutoka Namanga kwenda Arusha hakutakuwa na upotevu mkubwa njiani kama kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere kwenda Arusha. Hii ni logic ya kawaida ambayo hata mtoto mdogo anaelewa.

Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Ili tuweze kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere au Mtera hadi Arusha bila kupotea sana, inabidi tujenge vituo vya kupoozea njiani (substations) kama ile ya Lemuguru iliyopo Mateves Arusha, ambayo ilianza kujengwa 2019 imekamilika 2024 (miaka mitano) kwa gharama ya karibu bilioni 20. Kwa hiyo kuna suala la muda na gharama.

Je, umeme wa ziada unaozalishwa Tanzania utaenda wapi? Jibu ni kwamba Utauzwa nje ya nchi. Tayari Tanzania imesaini hati ya makubaliano (MoU) na Zambia na Rwanda kuziuzia umeme.

Je, kusafirisha umeme kwenda nchi hizo hakutafanya upotee njiani? Jibu ni kwamba umeme huo utauzwa kutoka vyanzo vya karibu, hivyo hakutakuwa na upotevu mkubwa. Kwa mfano, Rwanda watauziwa umeme kutoka Rusumo na Zambia watapokea umeme kutoka Kihansi ambapo upotevu hauwezi kuwa mkubwa kama kuutoa umeme Kihansi kwenda Arusha au Rusumo kwenda Arusha.

Utaratibu wa kuuziana umeme baina ya nchi na nchi sio jambo geni. Nchi za Afrika Mashariki zimeanzisha Eastern Africa Power Pool (EAPP) ili kuratibu biashara ya umeme na uunganishaji wa gridi kati ya nchi hizo.

Nchi za Ulaya wanayo European Network of Transmission System Operators for Electricity (ENTSO-E) ambayo inaunganisha nchi 35 za Ulaya. Kupitia ENTSO-E nchi inaweza kuuza na kununua umeme kutoka nchi jirani. Kwa mfano, Ujerumani inanunua umeme kutoka Ufaransa, Denmark, na Norway jumla ya 30,000 MW. Lakini Ujerumani hiyohiyo inauza umeme kwa Ufaransa, Austria, na Uholanzi ambao ni 60,000 MW.

Unaweza kujiuliza, kama Ujerumani inaweza kuzalisha umeme na kuuza nje ya nchi, kwanini tena inunue? Jibu ni kwamba inapunguza upotevu wa kusafirisha umeme kwa umbali mrefu ndani ya nchi. Kuliko kutoa umeme Munich na kuusafirisha hadi Humburg (kilomita karibu 800) ni bora wakanunua umeme Dernmark wakapeleka Humburg, halafu ule wanaozalisha Munich ukatumika miji ya jirani na mwingine wakauzia Austria.

Na Tanzania ndicho tulichofanya. Kuliko kutoa umeme Rusumo kuupeleka Kyela, ni bora ule wa Rusumo utumike Kigoma, Kagera, na Geita, halafu unaobaki tuwauzie Rwanda na Burundi. Halafu tununue umeme kutoka Malawi tupeleke Kyela. Tukifanya hivyo tutakua tumeokoa gharama za usafirishaji na upotevu wa umeme njiani.!

Hoja ya Malisa juu ya umbali wa kusafirisha umeme na gharama zake kwa kudai kuwa eti hatuhusiki kwenye gharama za usafirishaji kwa kuwa tunaupokelea Namanga, ni sawa na mteja anayekaa Dar anayedhani kuwa akinunua mahindi hapo sokoni kariakoo hahusiki na fact kuwa yamesafirishwa kutoka Iringa, na yeye kama mteja atahusika tu kulipia gharama ya usafirishaji katika bei atakayouziwa!.
 
Sio mtaalamu wa umeme lakini namna ulivyoeleza nimeelewa mno na nimeshawishika , kama taifa hili halijakuweka kitengo chochote Cha usimamizi au ushauri nikiri kabisa taifa limetukosea sana sisi WATANZANIA
 
Hizo njia zikitumika kutoa umeme Rufiji kwenda Arusha na Kilimanjaro nguzo zinaungua?
Yaani watu wa Ethiopia wao wanazalisha umeme kwa kutumia mchanga ambao TANESCO hawawezi kuwatuma wataalam wao wakajifunze namna ya kuzalisha umeme ambo ata ikipotea bado wanabaki na faida.
Sikushikii dude, kama umesoma sana, unaona ni sawa na wewe ni electrical engineer umewazidi walioamua kufanya hivo. Mimi ni nani nikubishie. Sawa nimekuelewa engineer, jamaa wezi sana. Kuna agenda wanasukuma.
 
Uvivu wa kufanya vitu vipya, uvivu wa kufanya vitu vya kesho isio lnekana miaka 50 mbele.. kama kujenga kituo kimoja ni bilion 20 vinne bilion 80 kama nchi tunakoswa hela kama hiyo? Kusema inachukua muda muda gani? JPM alituonesha tukiwa serious vitu tulivyozoea kuchukua muda vinakuwa havichukui muda huo tunao amainishwa (usimamizi). Mimi sion haja ya kununua umeme bora tujenge hivyo vituo hadi Arusha ili sisi tuwauzie hizo nchi huko Mipakani.
 
Wakimaliza kufanya hivyo waruhusu watu binafsi pia kuwauzia umeme wa ziada tunaozalisha majumbani, maofisini na viwandani.
Uwepo wa mini-grids na energy markets, Ndiyo njia pekee na rahisi kutokomeza tatizo la umeme nchini Tanganyika
 
aisee Ethiopia wako vizuri sana

Sasa mkuu sisi tunanunua kutoka Kenya au kutoka Ethiopia ?
 
Hapa huyu anatetea kitu kinachoenda kanda yao, ingekuwa kinaenda kanda tofauti angekuja na all sort of analysis kuonesha mradi wa kununua nje haufai. Nilishangaa sana kipindi cha nyuma kila miradi ilikuwa inapopolewa ati ni maendeleo ya vitu na si ya watu. Ila daraja la mto wami ule mradi haukupopolewa, guess why?
I thought like you..
 
Kuna jambo kubwa sana la maana ambalo halizungumzwi. Ujerumani akiuza au akinunua umeme Ufaransa anatumia Euro. Pesa ambayo nchi zote zinatumia. Sisi tukinunua umeme Ethiopia tutalipa kwa dola. MW100 zitagharimu karibu dola milioni 70 kwa mwaka. Bora kupoteza MW17 wakati wa kusafirisha kuliko kutoa hizo dola ambazo zingesaidia kununua vitu vya maana zaidi kama vifaa tiba, madawa, machine, kulipa deni la ujenzi wa bwawa la Nyerere nk nk.
 
Kuna jambo kubwa sana la maana ambalo halizungumzwi. Ujerumani akiuza au akinunua umeme Ufaransa anatumia Euro. Pesa ambayo nchi zote zinatumia. Sisi tukinunua umeme Ethiopia tutalipa kwa dola. MW100 zitagharimu karibu dola milioni 70 kwa mwaka. Bora kupoteza MW17 wakati wa kusafirisha kuliko kutoa hizo dola ambazo zingesaidia kununua vitu vya maana zaidi kama vifaa tiba, madawa, machine, kulipa deni la ujenzi wa bwawa la Nyerere nk nk.

Wewe akili kubwa!
Yaani BIG BRAIN.
Utakuwa umesoma special school.
Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom