DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Anaandika Mwanasiasa na mwanaharakati Godlisten Malisa.......
"CRDB Bank imetoa maua na tuzo ya pole kwa The Voice Bar Kinyerezi, inayodaiwa kuharibiwa kutokana na ghasia za Oktoba 29. Ni jambo jema kuwajali wateja wenu kwa kiwango hiki, na kwa hilo nawapongeza.
Lakini je, vipi kuhusu mamia ya Watanzania waliouawa kikatili? Mnadhani miongoni mwao hakuna wateja wenu? Bila shaka walikuwepo, tena wengi. Hao mmewapelekea maua? Mmewapa tuzo za faraja? Je mmetoa hata taarifa rasmi ya kuwapa pole?
Kumbukeni, The Voice imepoteza mali, lakini wapo wateja wenu waliopoteza uhai. Hamtawaona tena. Pengine mmoja wao angekuwa Mwekezaji wa kesho, angekuja kufungua The Voice kila mkoa. Lakini sasa wametoweka milele.
Sisemi mmekosea kuwapa pole The Voice. Mmefanya vema. Lakini si sahihi kuishia hapo. Mlipaswa kutoa pole kwa wateja wenu wote na kwa Watanzania kwa ujumla. Mauaji haya ya kikatili yamegusa karibu kila familia. Kama hujampoteza ndugu, umempoteza rafiki, au classmate, au muumini mwenzako kanisani/msikitini, au mfanyakazi mwenzako. Kwa kifupi kila mtu ameguswa.
Ni jambo la aibu kukaa kimya bila kusema lolote, halafu mnakimbilia kutoa pole kwa chupa za konyagi zilizovunjwa. Mnatuma ujumbe gani kwa wateja wenu? Kwamba mnajali zaidi mali kuliko utu?
Biblia inasema Uhai wa mtu ni bora kuliko mali (Mathayo 6:25). Na tena: “Mtu akipata mali zote za ulimwengu, akapoteza nafsi yake, atafaidika nini?” (Marko 8:36). Maneno haya yanatufundisha zawadi ya uhai ni takatifu na tunapaswa kuilinda kwa nguvu zote.
Kumbukeni mali hupotea na hupatikana tena, lakini uhai ukipotea haurudi. Mlichokifanya kimepunguza imani ya wateja wenu; wengi watajihisi hata wakipata majanga, benki yao inaweza kukaa kimya.
Falsafa yenu ni “The Bank that Listens" - benki inayosikiliza wateja. Sasa mbona hamjasikiliza kilio cha wateja wenu? Mito ya uchungu inatiririsha damu na machozi yao, na ninyi mmekaa kimya? Mnashindwa hata kutoa pole?
Kama kweli mnajali, ombeni radhi. Toeni pole kwa watanzania wote na familia zilizopoteza wapendwa wao. Onesheni kwa vitendo kwamba utu ni zaidi ya mali, ni zaidi ya fedha, ni zaidi ya chochote. Dalai Lama alisema "Utu ni nguzo ya maisha; lakini mali ni kivuli kinachopita"