Godoro gani la quality ya juu kuepusha maumivu ya mgongo?

Godoro gani la quality ya juu kuepusha maumivu ya mgongo?

Magodoro mengi mtaani ni fake- aende kwenye duka la kampuni husuka, comfy vita raha wapo mlimani, qfl nenda kariakoo kwa wahindi. Ukitaka kujua godoro fake ukiona godoro ni pale unaambiwa godoro la 5 kwa 6 na kuendelea la inch 8 and over linabebwa kwa pik pik. Density ya godoro oruginal kama hilo huwez kukunja hata mara mbili ukabebq kwenye boda
Kuna magooro huwa yanakuja yamekunjwa kutoka Kiwandan
 
ni kweli hata mimi nilinunua magodoro ya dodoma kiwandani kwao kabisa .Tena nilinunua mawili inch 6 kwa sita inch 12 na la watoto AISEE magodoro yale yana bonyea yanaacha shimo,yanaumiza mgongo balaa yani una amka umechoka sana na unaamka ukiwa unaumwa.KUMBE nikaja nikaambiwa magodoro ya dodom mazuri QFL sio dodoma kumbe kuna utofauti kati ya magodoro ya dodoma na QFL.

Kwa hasira nikaenda kununua magodoro yanayoitwa primiamu.Haya kwa kweli ni mazuri sema bei yake imechangamka kidogo.
ulinunua wapi na bei ni sh ngapi please share hapa mkuu?
 
Chukua TUF FOAM ulale kama upo kwenye mtumbwi
 
Kuna magodoro ni kituko.
Mnalala wawili hamjaguusana ila mkipitiwa na usingizi mnajikuta wote mshatumbukia kati afu pembeni limenyanyuka kila pande utadhani linasubiri mafuriko muondoke maana ni mtubwi kabisaa
 
Wakuu naomba msaada natafuta godoro zuri 6*6 inch 12 u 14 ambalo litanifanya nikilala nione nimelala sehemu nzuri na salama mnoo kwa mwili wangu, kuepusha maumivu ya mgongo, gharama ya godoro ilo lisizidi 1M (Shilingi milion 1). Natanguliza shukrani zangu kwenu naomba kupata ushauri wenu
Epuka kulalia Mto (pillow) inapunguza sana maumivu ya mgongo , mimi mwenyewe ni shuhuda wa hili.
 
Nilikuwa naumia mgongo kwa mda mrefu kwa kutumia haya magoro manene ..nikawa na maumivu sugu kila wakati.
Nilienda field nilipiga miezi 3,yote hyo nililalia vgoro vile vya wanafunzi..
Maumivu yalikata baada ya mwezi nikawa mzima kabisa,
Niliporudi home niliachana na hayo manene natumia kigoro kidogo vya 50000 vile.
Ukiwa na 5x6 nunua viwili visambaze kama nikitandani au chini.
Utakuja nishukuru.
 
Back
Top Bottom