Simba jana ilicheza kandanda safi sana dhidi ya Lipuli kwa muda wote wa mchezo. Nawashauri Simba kuwa waanze kumtafuta kipa badala ya Manula. Lile goli la jana siyo goli la kufungwa kipa kama Manula. Dosari kubwa la Manula ni kimo chake. Manula ni mfupi kwa kimo na kwa goli la jana kama kipa angekuwa ni kipa mrefu lile goli lisingeingia kwenye nyavu. Simba tafuteni kipa mrefu na mahiri hasa wakati huu wa dirisha dogo.