Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Kauli ya Serikali kwamba “goli la mama lipo… safari hii tutavunja rekodi” imeamsha mjadala mzito miongoni mwa wadau wa soka nchini. Wakati fainali za AFCON zikikaribia Desemba 21, 2025, matumaini yanapandishwa juu kupitia kauli tamu, zawadi nono na misafara ya wajumbe. Lakini swali la msingi linabaki pale pale: je, tunajenga soka au tunajenga kampeni?
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema mipango yote iko tayari, kambini Misri hali ni nzuri na Taifa Stars iko tayari kwenda Morocco. Serikali pia imepanga kupeleka wawakilishi kutoka miji itakayohusika na AFCON 2027 ili “kujifunza”. Haya yote ni mazuri kwenye makaratasi, lakini uhalisia wa uwanja unasema jambo jingine.
Historia haidanganyi. Kila tunapokaribia mashindano makubwa, simulizi huwa zilezile: ahadi, zawadi, goli la mama, na malengo ya “kuvunja rekodi”. Mwisho wa safari tunarudi kichwa chini—bila kombe, bila heshima, bila chochote cha kujivunia. Tatizo si ukosefu wa ari, bali ni ukosefu wa mkakati wa muda mrefu.
Badala ya kuelekeza nguvu kubwa kwenye kusaka vipaji mashuleni, kuimarisha ligi za vijana, kuweka miundombinu ya kisasa, na kuwa na sera thabiti ya maendeleo ya soka, tumekwama kwenye kampeni za kisiasa na hamasa za muda mfupi. Goli la mama haliwezi kufunga magoli uwanjani. Zawadi haziwezi kubadili mbinu za kocha wala kuongeza ubora wa kiufundi wa wachezaji.
Kuvunja rekodi hakupatikani kwa kauli, bali kwa uwekezaji makini, nidhamu na mipango inayoanza chini kabisa. Kama kweli tunataka AFCON iwe zaidi ya matembezi, basi ni wakati wa kuacha maigizo na kuwekeza kwenye msingi wa soka. La sivyo, Desemba imefika, filimbi ya mwisho itapulizwa, nasi tutarudi nyumbani kama kawaida—kichwa chini, visingizio juu.
KUMBUKENI: MKIFUNGWA NYIE NI TIMU YA WATANZANIA ILA MKISHINDA NYIE NI WATOTO WA MAMA!