Goli la Simba dhidi ya Azam ASFC 2021

Goli la Simba dhidi ya Azam ASFC 2021

Mkuu upo sahihi kabisa anaesimamisha mchezo no muamuz na anaeanzisha mchezo no muamuzi Simba walianzisha bila filimbi ya muamuzi Cha ajabu atamuamuzi alikurupuka kukimbia kuangalia mpira ulioingia golini na kuita mpira Kati ni upuuzi wa muamuzi asiyejua kazi yake au kunakitu kilikua kinaendelea kichwani kwake.
Acha utopolo mkuu kasome kanuni,
 
Kumbe nimegundua kwa nini utopolo kila siku wanalalamika wanaonewa tatizo ni kwamba hawajui mpira. Leo wangekuwa wao polisi wangepata kazi ya kulinda usalama.
Wewe ni mpumbavu refa ndiye fala hakutakiwa kuwa sehemu ya malumbano kutoa maelekezo kwa wachezaji maana yake mpira umesimama

Kama ulifatilia ile gemu azam walipata faulo na walianza haraka na alikataa na kurudisha mpira kwanini?

Angalia tofauti na wenzetu refa anakuwa hayupo kwenye maongezi na wachezaji ndio magoli yanaruhusiwa
 
Mkuu umetisha

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Watu ni wabishi sana.. inabidi uwape evidence zote. Wakatae tu kwasababu ya utopolo wao
20210626_190453.jpg
 
Mchezo wa jana Azam hakutendewa haki. Ule ni uonevu mkubwa.
 
Wewe ni mpumbavu refa ndiye fala hakutakiwa kuwa sehemu ya malumbano kutoa maelekezo kwa wachezaji maana yake mpira umesimama

Kama ulifatilia ile gemu azam walipata faulo na walianza haraka na alikataa na kurudisha mpira kwanini?

Angalia tofauti na wenzetu refa anakuwa hayupo kwenye maongezi na wachezaji ndio magoli yanaruhusiwa
Acheni mihemko
 
Lile bao hakuna kosa kwa upande wa Simba wala Mwamuzi, ni akili kubwa ya Wachezaji wa Simba kwenye hatua kama zile

Rejea Simba dhidi ya Nkana kwenye Klabu bingwa Afrika, move ya faulo ilikuwa kama ile, Wachezaji wa Nkana walipoteza concentration, Simba wakawahi kuweka (Quick thinking).

Azam au Mtu yoyote ambaye ni Mwanasoka ajue inapotokea faulo yoyote lazima kwanza ukazibe mpira, zibeni mpira huku wengine wanaongea na Mwamuzi.

Wenzetu Ulaya ile mali hata akichezewa faulo anawahi kuidaka kwanza ikae eneo lake, wengine kwenye ukuta na wengine wanakaa karibu na mpira.

Sasa Azam wengine wapo kwa Mwamuzi na wengine wanajipanga, wakaacha mpira kwa Simba, ni akili ya haraka Simba wakaitumia kufunga lile bao, hizo ndio akili za Wazoefu.

Kilichotokea ni kuendelea kujifunza, kukomaa na kujua nini kinahitajika kwa wakati gani.​

View attachment 1830891
Kosa alilolifanya refa ni kujadili na wachezaji wa azam, refa angekuwa haongei na wachezaji waliofungwa lile goli ni halali
 
Faulo ilipulizwa.Maana yake mchezo umesimama.

Ili mchezo uendelee lazima refarii aruhusu tena.

Mazingira yale ya mpira hata kama ni kwiki thinking'i siyo sahihi.

Ingekuwa refarii haongei na mtu sawa.

Ila mchezaji mmojawapo wa Azam yupo na refarii,wanaongea.

Hata kama kanuni zinaruhusu jambo hili siyo sahihi.

Kipyenga kipulizwe.

Pale ni karibu na goli,ukuta uwekwe

Wenye faida na pigo wapige mpira.

Mazingira ya namna ile yanatengeneza maamuzi yasiyo sahihi kwa waamuzi,wengine wanaweza kuzuia ile 'move' ya mpira na kuamuru upigwe tena.

Wengine wakaacha lililoanza liendelee.Yaani tunaruhusu maamuzi ya 'utashi' badala ya maamuzi ya sheria.
Endelea kutazama video nyingi za soka la ulaya kuna siku utaliona goli au magoli kama lile.
 
Kosa alilolifanya refa ni kujadili na wachezaji wa azam, refa angekuwa haongei na wachezaji waliofungwa lile goli ni halali
Wachezaji wa azam walionyesha kutokomaa kimataifa na uchovu uliwaingia. Hakuna kosa kwa Morrison kuanzisha faulo haraka haraka.
 
Wachezaji wa azam walionyesha kutokomaa kimataifa na uchovu uliwaingia. Hakuna kosa kwa Morrison kuanzisha faulo haraka haraka.
Sheria inasema timu iliyochezewa faulo inaweza kuanzisha mpira haraka ikiwa tu wachezaji waliofanya faulo wako yadi 10 kutoka mpira ulipo
 
Iangalie vizuri clip iliyotupiwa kwenye uzi huu. Hii clip ni ya mechi nyingi. Kuna mechi moja wachezaji walikuwa wanamzonga mwamuzi na free kik ikapigwa refa akakubali goli na mpira ukawekwa kati. Kuna nyingine golikipa alikuwa ameegemea goli ili aanze kuwapanga wachezaji wake na fasta free kik ikapigwa akabaki ameegemea goli wakati nyavu zinatikisika!!
Aliyekwambia refa hakosei ni nani?
 
Kwa kawaida kama kuna faulo lazima refa ahakikishe wachezaji wa pande zote wamejipanga na ndipo apulize kipenga. Kitendo cha leo cha refa akiwa bado anazungumza na wachezaji wa Azam halafu kabla hajaruhusu mpira upigwe mchezaji wa Simba anaanzisha mpira na kufunga. Binafsi ule ni uonevu mkubwa na kama ni ushindi basi refa ndo amewapa Simba ushindi. TFF wapeni adhabu marefa kama wale ikiwa ni kuwafungia maisha. Kweli inauma. Poleni sana Azama ule ulikuwa ushindi wenu.
Neno "kwa kawaida " unamaanisha Nini? Ni sheria au mazoea?
 
Sheria inasema timu iliyochezewa faulo inaweza kuanzisha mpira haraka ikiwa tu wachezaji waliofanya faulo wako yadi 10 kutoka mpira ulipo
Inasema hivyo lakini sio utekelezaji halisi. Real Madrid walifunga goli kama la jana. Thierry Henry aliwafunga Chelsea goli kama lile. Mpira ni kujiongeza.
 
Mkuu kuna vitu unachanganya, hapa refa alikuwa haongei na wachezaji wa sevila, wakati kwa upande wa kwetu huku refa alikuwa anaongea na wachezaji wa azam
Waendelee kuongea na refa pia siku nyingine
 
Back
Top Bottom