.
Usitulilie badae!!
Mie kumsingi naamini Mpendazoe kachemsha. Ninazo sababu:-
Hofu yangu ni moja. Inawezekana Mpendazoe alikuwa anatishwa kimya kimya na dola na vitisho vyenyewe alikuwa anajua vitamdhuru. Akaona akimbie.
- Alitakiwa kuupinga ufisadi akiwa ndani ya CCM. Nje ni kujimaliza kisiasa.
- Mtu yeyote anayegombea ubunge huwa ana dhamira mbili. Moja ni kuwa na nafasi ya kupata kipato zaidi (kwa maana ya mshahara zaidi, heshima zaidi kwa kuitwa mheshimiwa na cheo zaidi ikiwa atapewa uwaziri au mamlaka mengine) na mbili ni "kuwatumikia wananchi". Sasa ku sacrifice haki ya kikatiba ya zaidi shilingi 40m/= kwa muda aliotumia kuwatumikia wananchi ni kuchemsha. Labda huko alikoenda amepata zaidi ya hizo (kitu ambacho kitakuwa ni rushwa).
- Kama alikuwa na dhamira halisi ya kuhama chama ili baadae aendelee kuwatumikia wanachi kwa kugombea tena ubunge akapata angehamia chama kingine cha kudumu, na sio kwenda kwenye chama ambacho hana uhakika kama kitapata isajili wa kudumu.
- Akumbuke mbunge sio kada wa chama. Makada wa chama wana wafuasi ndani ya chama husika. Chama huteua wanachama wake ili wakiwalishe katika uchaguzi fulani kulingana na upepo unavyovuma kwenye jimbo hilo la uchanguzi. Na moja ya sharti la kuteuliwa kugombea ni kuikitumikia, kukishabikia na kukubaliana na maamuzi yote ya chama. Ndio maana kina Wasira waliweza kuhama chama na waliporudi wakpokelewa kwa mikono miwili. Ni upepo tu. Kwa bahati mbaya hana influence ya kuwafanya wana Kishapu kuhamia CCJ. Heri Dan Makanga na UDP vs CCM kule Baridi enzi hizo.
- Kajifunga goli. atasononeka. atabaki peke yake.
- Kachemsha ile mbaya. Kimsingi huo ndio mwisho wake kisiasa.
Nani awalilie, kwa lipi? Huyo anatapatapa tu. Tumeshaona wengi na mwisho wao unaeleweka, historia ipo, cha ajabu hawajifunzi. Akina Mrema na kundi lake, na baadae Njelu Kasaka, si tunawaona mitaani wanalialia tu hovyo? Huyu ndiye atakakuja kulialia tu kama wenzie wanaolialia sasa hivi.
Total miscalculation. Hadi huruma!
Unataka kusema wanaokumbatia ufisadi na wanachama cha majambazi hao ndio wanajua kufanya calculation zao vizuri?
hehehe kwa hiyo ubunge siyo uongozi and wajumbe wa shina ndo misingi ya uongozi?Wameshasema eti hakuwahi kuongoza hata shina. Shem on them.
Hata kidogo. Lakini hii ya huyu kakosea move. Ni kama mko kwenye mechi halafu mchezaji mmojawapo anaamua kuondoka uwanjani na kuhamia kwenye jukwaa la washangiliaji.
Nani awalilie, kwa lipi? Huyo anatapatapa tu. Tumeshaona wengi na mwisho wao unaeleweka, historia ipo, cha ajabu hawajifunzi. Akina Mrema na kundi lake, na baadae Njelu Kasaka, si tunawaona mitaani wanalialia tu hovyo? Huyu ndiye atakakuja kulialia tu kama wenzie wanaolialia sasa hivi.
Total miscalculation. Hadi huruma!
Hata kidogo. Lakini hii ya huyu kakosea move. Ni kama mko kwenye mechi halafu mchezaji mmojawapo anaamua kuondoka uwanjani na kuhamia kwenye jukwaa la washangiliaji.
Unachojua wewe ni move tu na ulaji unaoweza kupatikana uki-move toka hapa kwenda kule. Wenzio wanawaza zaidi ya hapo. Wanawaza mustakabali wa nchi. Wanawaza nchi watakayoachiwa wajukuu zetu. Kwa maana nzima ni kwamba watu kama Mpendazoe wanawaza mustakabali wa nchi wala si ubunge wa kesho kutwa.
Mechi gani inayochezwa ndani ya CCM hivi sasa itakayoleta manufaa kwa taifa?
Hataki umaarufu, kwa hiyo anataka nini? Kama hataki umaarufu mbona kaitisha mkutano wa waandishi wa habari kuwajuza kuhusu kuhama kwake? Umaarufu anautaka sana, na anataka agombee tena huko Kishapu. Ingekuwa hataki umaarufu, angesubiri muda wake uishe wa ubunge kipindi hiki, halafu asigombee, aende huko CCJ kimyakimya, habari tungezipata tu bila yeye kuitisha mkutano.
Sasa habari ya ubunge tena ndio asahau, maana hiyo CCJ itapata usajili wa kudumu baada ya uchaguzi mkuu, labda mwaka ujao au hata baadaye.
Amefulia
'Mechi' inawakilisha msimamo wa alichokuwa anakipigania akiwa bungeni huko. Kwa hiyo timu yake ni wale wote waliokuwa upande mmoja katika mpambano huo. Huko alikoenda hataweza kuendeleza mapambano, ni kakundi tu ka washangiliaji, hakuna impact. Yuko nje ya ulingo sasa, atakuwa mlalamishi tu, wale ambao lugha za mitaani tunawaita 'bush lawyers'. Katika hili mafisadi ndio wameshinda, ndio maana nasema kajifunga goli mwenyewe halafu akahamia jukwaa la washangiliaji.
You are far too naive about politics to argue with 'true' politicians. Wewe naona hata hujui haki za kikatiba za Mtanzania, ungeliyajua hayo wala usingelijaribu kumsakama Mpendazoe. Hata kama wewe unaona hakuna impact why worry, let Mpendazoe worry about it. Nje ya ulingo gani wakati kuna vyama vingi nchini?
Amefulia kwa sababu hicho anachodai anapigania hatafanikiwa katika hiyo CCJ. Na kwa style aliyotoka nayo, kajinyima kabisa ukumbi wa kuendeleza mapambano. Kwa hiyo amefulia
Ukumbi upi wa mapambano unaodai kajinyima? Mapambano yako mitaani kuwaelimisha wananchi kama wewe wajue hali za kikatiba. Vitisho na vikwazo havisaidii, mara nyingi ndio vinavyochochoea mapambano.
Harakati za Makamba na UVCCM kusafishana na kutishiana zinatakiwa zioneshwe na majasiri wengine kama Mpendazoe, watoke na kujiunga upinzani bila woga wa kifilisiwa na chama tawala, upinzani upate nguvu na CCM iwe chama cha Upinzani