Goli ni Goli; la Mpendazoe nalo Goli!

Goli ni Goli; la Mpendazoe nalo Goli!

.
Usitulilie badae!!

Nani awalilie, kwa lipi? Huyo anatapatapa tu. Tumeshaona wengi na mwisho wao unaeleweka, historia ipo, cha ajabu hawajifunzi. Akina Mrema na kundi lake, na baadae Njelu Kasaka, si tunawaona mitaani wanalialia tu hovyo? Huyu ndiye atakakuja kulialia tu kama wenzie wanaolialia sasa hivi.

Total miscalculation. Hadi huruma!
 
Mie kumsingi naamini Mpendazoe kachemsha. Ninazo sababu:-

  1. Alitakiwa kuupinga ufisadi akiwa ndani ya CCM. Nje ni kujimaliza kisiasa.
  2. Mtu yeyote anayegombea ubunge huwa ana dhamira mbili. Moja ni kuwa na nafasi ya kupata kipato zaidi (kwa maana ya mshahara zaidi, heshima zaidi kwa kuitwa mheshimiwa na cheo zaidi ikiwa atapewa uwaziri au mamlaka mengine) na mbili ni "kuwatumikia wananchi". Sasa ku sacrifice haki ya kikatiba ya zaidi shilingi 40m/= kwa muda aliotumia kuwatumikia wananchi ni kuchemsha. Labda huko alikoenda amepata zaidi ya hizo (kitu ambacho kitakuwa ni rushwa).
  3. Kama alikuwa na dhamira halisi ya kuhama chama ili baadae aendelee kuwatumikia wanachi kwa kugombea tena ubunge akapata angehamia chama kingine cha kudumu, na sio kwenda kwenye chama ambacho hana uhakika kama kitapata isajili wa kudumu.
  4. Akumbuke mbunge sio kada wa chama. Makada wa chama wana wafuasi ndani ya chama husika. Chama huteua wanachama wake ili wakiwalishe katika uchaguzi fulani kulingana na upepo unavyovuma kwenye jimbo hilo la uchanguzi. Na moja ya sharti la kuteuliwa kugombea ni kuikitumikia, kukishabikia na kukubaliana na maamuzi yote ya chama. Ndio maana kina Wasira waliweza kuhama chama na waliporudi wakpokelewa kwa mikono miwili. Ni upepo tu. Kwa bahati mbaya hana influence ya kuwafanya wana Kishapu kuhamia CCJ. Heri Dan Makanga na UDP vs CCM kule Baridi enzi hizo.
  5. Kajifunga goli. atasononeka. atabaki peke yake.
  6. Kachemsha ile mbaya. Kimsingi huo ndio mwisho wake kisiasa.
Hofu yangu ni moja. Inawezekana Mpendazoe alikuwa anatishwa kimya kimya na dola na vitisho vyenyewe alikuwa anajua vitamdhuru. Akaona akimbie.

...akili ya wana ccm wengi ni ya kama huyu kufikiria ugali wa leo tu hawjui kuangalia mbele! kwani ubunge tu ndio kazi ya maana ya kutumikia wananchi??? na lazima awe mbunge uchaguzi ujao??? anaweza kugombea hata baada ya miaka 10 ijayo provided Mungu anampa uzima!!
...hakuna ajuae yale yatatokea kwenye uchaguzi ujao hata ya kesho tu! isipokuwa Mungu! nini maana ya kumwambia mtu kachemsha au kafulia?
MAWAZO NA MIPANGO YA MPUMBAVVU INAFIKIRIA MLO NA MASLAHI BINAFSI YA MUDA MFUPI,...Bali mawazo ya mwerevu yanafikiria mambo yadumuyo na yanayohusu wengine! HILI NI SOMO ZURI KWA WATANZANIA WENYE AKILI SAWASAWA KUTOKA KWA MPENDAZOE!!
 
Nani awalilie, kwa lipi? Huyo anatapatapa tu. Tumeshaona wengi na mwisho wao unaeleweka, historia ipo, cha ajabu hawajifunzi. Akina Mrema na kundi lake, na baadae Njelu Kasaka, si tunawaona mitaani wanalialia tu hovyo? Huyu ndiye atakakuja kulialia tu kama wenzie wanaolialia sasa hivi.

Total miscalculation. Hadi huruma!

Unataka kusema wanaokumbatia ufisadi na wanachama cha majambazi hao ndio wanajua kufanya calculation zao vizuri?
 
mpendazoe ni cheche ndogo kwenye petrol - tufumbue macho
 
Mkuu MM umemsikia Tambwe Hiza alivyomkandia yaani anatufanya watanzania tumesahau kuwa hayo aliyo dai Mpendazoe ndio ambayo Tambwe alikuwa anapigia kelele alipokuwa CUF lakini sasa yuko huko haoini shida. Lakini hajui kati yao Mpendazoe ni jasiri kuliko yeye kwa sababu yeye ametoka kubovu na yeye amekimbilia kubovu.
 
Unataka kusema wanaokumbatia ufisadi na wanachama cha majambazi hao ndio wanajua kufanya calculation zao vizuri?

Hata kidogo. Lakini hii ya huyu kakosea move. Ni kama mko kwenye mechi halafu mchezaji mmojawapo anaamua kuondoka uwanjani na kuhamia kwenye jukwaa la washangiliaji.
 
Hata kidogo. Lakini hii ya huyu kakosea move. Ni kama mko kwenye mechi halafu mchezaji mmojawapo anaamua kuondoka uwanjani na kuhamia kwenye jukwaa la washangiliaji.

Unachojua wewe ni move tu na ulaji unaoweza kupatikana uki-move toka hapa kwenda kule. Wenzio wanawaza zaidi ya hapo. Wanawaza mustakabali wa nchi. Wanawaza nchi watakayoachiwa wajukuu zetu. Kwa maana nzima ni kwamba watu kama Mpendazoe wanawaza mustakabali wa nchi wala si ubunge wa kesho kutwa.

Mechi gani inayochezwa ndani ya CCM hivi sasa itakayoleta manufaa kwa taifa?
 
Nani awalilie, kwa lipi? Huyo anatapatapa tu. Tumeshaona wengi na mwisho wao unaeleweka, historia ipo, cha ajabu hawajifunzi. Akina Mrema na kundi lake, na baadae Njelu Kasaka, si tunawaona mitaani wanalialia tu hovyo? Huyu ndiye atakakuja kulialia tu kama wenzie wanaolialia sasa hivi.

Total miscalculation. Hadi huruma!

Ni kweli, hawa wote "Akina Mpendazoe" watarudi tu na kulia mwangalie shujaa wao Mrema A. L. sasa amerudi na gia ya kuwachafulia akina 6 na wengineo, na kutaka wapewe haki zao za kukiacha Chama dume CCM na kukimbilia huko kwa "Mataifa".
 
Hata kidogo. Lakini hii ya huyu kakosea move. Ni kama mko kwenye mechi halafu mchezaji mmojawapo anaamua kuondoka uwanjani na kuhamia kwenye jukwaa la washangiliaji.

Unaweza kutoa mfano wa move sahihi kwa Mpendazoe?
 
Unachojua wewe ni move tu na ulaji unaoweza kupatikana uki-move toka hapa kwenda kule. Wenzio wanawaza zaidi ya hapo. Wanawaza mustakabali wa nchi. Wanawaza nchi watakayoachiwa wajukuu zetu. Kwa maana nzima ni kwamba watu kama Mpendazoe wanawaza mustakabali wa nchi wala si ubunge wa kesho kutwa.

Mechi gani inayochezwa ndani ya CCM hivi sasa itakayoleta manufaa kwa taifa?

'Mechi' inawakilisha msimamo wa alichokuwa anakipigania akiwa bungeni huko. Kwa hiyo timu yake ni wale wote waliokuwa upande mmoja katika mpambano huo. Huko alikoenda hataweza kuendeleza mapambano, ni kakundi tu ka washangiliaji, hakuna impact. Yuko nje ya ulingo sasa, atakuwa mlalamishi tu, wale ambao lugha za mitaani tunawaita 'bush lawyers'. Katika hili mafisadi ndio wameshinda, ndio maana nasema kajifunga goli mwenyewe halafu akahamia jukwaa la washangiliaji.
 
Hataki umaarufu, kwa hiyo anataka nini? Kama hataki umaarufu mbona kaitisha mkutano wa waandishi wa habari kuwajuza kuhusu kuhama kwake? Umaarufu anautaka sana, na anataka agombee tena huko Kishapu. Ingekuwa hataki umaarufu, angesubiri muda wake uishe wa ubunge kipindi hiki, halafu asigombee, aende huko CCJ kimyakimya, habari tungezipata tu bila yeye kuitisha mkutano.

Sasa habari ya ubunge tena ndio asahau, maana hiyo CCJ itapata usajili wa kudumu baada ya uchaguzi mkuu, labda mwaka ujao au hata baadaye.

Amefulia

Wakufulia ni wewe ambaye hujui politics zinavyokwenda, unasukumwa na hisia za kibinafsi tu! Hata kama itafanyika mizengwe ya kuchelewesha CCJ isipate usajili wa kudumu na ikapata usajili mwaka keshokutwa cha muhimu hapa ni kwamba Mpendazoe amesimama kuhesabiwa, sio mnafiki kama wengine wanaonung'unikia pembezoni. Amedhihirisha kwa vitendo kwamba hakubaliana na jinsi CCM inavyoendesha mambo yake. Ametimiza wajibu wake wa kidemokrasia hata kama wapo wanaotamani kumbinya kwa kitendo hicho.

Unadhani alikuwa hajui kwamba hayo ya CCJ kucheleweshwa kupata usajili yanaweza yakatokea?
 
Walikuwa wapi siku zote kusema maneno yote hayo? Kama alikuwa mzigo kwanini asitolewe chamani kipindi hicho yupo ndani ya CCM? Hatudanganyiki na hayo ni maneno yao kila unapotokea upinzani. Mwingine akijitoa watadai alikuwa ni mzigo ndani ya chama. Hivyo CCM kutakuwa kumejaa mizigo,kwanini tusichague upinzani jamani?
 
hata kama mpendazoe atarudi basi lazima kuna hatua itakuwa imepingwa na hao walafi lazima watakuwa wamejirekebisha japo kwa nukta ndogo
 
'Mechi' inawakilisha msimamo wa alichokuwa anakipigania akiwa bungeni huko. Kwa hiyo timu yake ni wale wote waliokuwa upande mmoja katika mpambano huo. Huko alikoenda hataweza kuendeleza mapambano, ni kakundi tu ka washangiliaji, hakuna impact. Yuko nje ya ulingo sasa, atakuwa mlalamishi tu, wale ambao lugha za mitaani tunawaita 'bush lawyers'. Katika hili mafisadi ndio wameshinda, ndio maana nasema kajifunga goli mwenyewe halafu akahamia jukwaa la washangiliaji.

You are far too naive about politics to argue with 'true' politicians. Wewe naona hata hujui haki za kikatiba za Mtanzania, ungeliyajua hayo wala usingelijaribu kumsakama Mpendazoe. Hata kama wewe unaona hakuna impact why worry, let Mpendazoe worry about it. Nje ya ulingo gani wakati kuna vyama vingi nchini?
 
Haki za kikatiba nazijua. Katiba inamruhusu mchezaji kuhama kutoka timu inayocheza ligi ya daraja la kwanza na kuhamia ya daraja la nne, au hata ya 'mchangani' ni haki yake, chaguo lake, hajavunja sheria. Na watu wanaitumia haki hiyohiyo kujididimiza na kudidimiza timu zao. Haki ya kikatiba haimzuii mtu kufulia kama anapenda hivyo, ima kwa kujua ama kutokujua. Kwa hiyo bado Mpendazoe amefulia, na of course ni haki yake pia.
 
Amefulia kwa sababu hicho anachodai anapigania hatafanikiwa katika hiyo CCJ. Na kwa style aliyotoka nayo, kajinyima kabisa ukumbi wa kuendeleza mapambano. Kwa hiyo amefulia

Ukumbi upi wa mapambano unaodai kajinyima? Mapambano yako mitaani kuwaelimisha wananchi kama wewe wajue hali za kikatiba. Vitisho na vikwazo havisaidii, mara nyingi ndio vinavyochochoea mapambano.
 
Ukumbi upi wa mapambano unaodai kajinyima? Mapambano yako mitaani kuwaelimisha wananchi kama wewe wajue hali za kikatiba. Vitisho na vikwazo havisaidii, mara nyingi ndio vinavyochochoea mapambano.

Mtaani atafanya nini zaidi ya kunung'unika tu na kulalama kila kukicha? Malalamiko na manung'uniko ya mitaani ni shughuli inayowafaa wale wasiokuwa na uwezo wa kufika hapo alipokuwa amefika. Amewaangusha wapiga kura wake.
 
Harakati za Makamba na UVCCM kusafishana na kutishiana zinatakiwa zioneshwe na majasiri wengine kama Mpendazoe, watoke na kujiunga upinzani bila woga wa kifilisiwa na chama tawala, upinzani upate nguvu na CCM iwe chama cha Upinzani

You have a point here. Chama kisichotaka kukubali makosa yake bila shaka kinaweza kutumia mbinu mbalimbali chafu kuwadhuru kwa njia moja ama nyingine wale wanaotoka. Kama waasisi wa Taifa hili waliweza kujitoa muhanga dhidi ya vitisho vya Wakoloni wazalendo wenye uchungu na nchi yao watashindwaje kujitoa muhanga? Mpendazoe kadhihirisha kwamba hana roho ya kuku!
 
Back
Top Bottom