Golikipa Beno Kakolanya ni moja kati ya maduka ya Home shopping center (GSM)

Golikipa Beno Kakolanya ni moja kati ya maduka ya Home shopping center (GSM)

Haina salamu! Moja kwa moja kwenye uzi

Hivi benchi la ufundi la timu ya simba linaruhusu vipi hili duka la GSM kuendelea kuidakia timu yetu??!!! Hawa wachezaji tunaowasajili kutokea Yanga si wa kuwamini hata kidogo!

Ukiangalia magoli yote mawili ya jana yaliyofungwa na Fiston kaamka mayele utagundua kuwa kuna kauzembe cha makusudi kilichofanywa na hilo duka la GSM pale golini. Goli kipa wa kimataifa huwezi akafungwa goli za kinamna ile, yaani kipa anashindwa kunyoosha mikono yake kudaka kashuti kadhaifu kama kile tena kashuti cha chinichini kama kile....!!

Haya maduka huwa yanapokea tu maelekezo kutoka kwa waajiri wao wa zamani ili tu yafungishe na mwisho wa siku yanaenda kuchukua (yanaingiziwa) donge nono.

Ni kipindi sasa simba itafute golikipa wa kiwango cha juu kutoka nje ya tanzania maana hawa wazawa wanaendekeza sana matumbo yao kuliko maslahi ya timu.

Wasalam
Mara Inonga! Mara kocha Matola, mara kocha mzungu baada ya kumtoa Chama! Na sasa ni Kakolanya!!

Hii ni moja ya dalili ya kuvurugwa bila shaka!!!
 
Sasa si Bora tumsajili mandonga kama kila ikipigwa Shuti imo kisa mabeki wamefanya makosa.
 
kweli kabisa,magoli yote ni uzembe wa mabeki Enonga na Otara
goli la kwanza Mayele kapenyezewa pasi halafu akapiga kwenye angle la pembeni hata ingekuwa Mendy kufuata ni ngumu ,ya pili kapiga kwenye mwanya wa mabeki kalenga angle vile vile ya chini,magoli yote ya Mayele huwa halengi kipa ni pembeni ,pale lawama ni uzembe wa mabeki
 
Jeneza fc a.k.a KARIA FC 😂

TUTAWANYOOSHAAAAA NA MSOMARI WENU
 
Uzuri magoli ya namna ile Mayele amemfunga hata Kipa wenu namba 1.
Nakukumbusha tu goal la 2 Mayele alimgeuza inonga mbele na nyuma akampiga tobo mpira ukajaa nyavuni
 
Back
Top Bottom