POTOSHI Golugwa amesema wananchi wamepiga kelele wanataka waruhusiwe kulima bangi?

POTOSHI Golugwa amesema wananchi wamepiga kelele wanataka waruhusiwe kulima bangi?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2

1764254065380.png
 
Tunachokijua
Amani Golugwa ni naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye aliteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho kutumikia nafasi hiyo, Tundu Lissu na kuthibitishwa na baraza kuu mnamo tarehe 22, Januari 2025.

Tarehe 27, Novemba 2025, Golugwa alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo hotuba yake ilirushwa mbashara kupitia 'Channel' ya chama hicho, CHADEMA MEDIA TV kwenye mtandao wa YouTube.

Kumekuwepo na video iliyochapishwa katika mtandao wa TikTok kupitia ukurasa unaotumia jina la 'Kizota Wa Depo' ikimuonesha Golugwa akisema 'wananchi wamepiga kelele wanataka waruhusiwe kulima bangi'


Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?


Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia marejeo ya video umejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa kwa kukata na kuunganisha vipande isivyostahili hatimaye kubadili ujumbe halisi uliotolewa na Golugwa.

Katika video halisi Golugwa ameisihi serikali kusikiliza kile ambacho wanakihitaji akisema,

"Ninaisihi serikali ni lazima isikilize wananchi wanachokitaka kwa sababu ni jambo jema. Wananchi hawajapiga kelele wanataka waruhusiwe kulima bangi, wananchi hawajapiga kelele wanataka waruhusiwe wawe wanasafirisha mirungi. Wananchi wamepiga kelele wamesema wanataka 'reforms' (mabadiliko) ili wawe na chaguzi huru za haki ambazo zitawapa taifa lao viongozi wanaowapenda na watakuwa na amani"
​
Back
Top Bottom