Jeshi la kukodiwa la kutoka Romania, wameona moto uliukuwa unatembezwa na M23 na RDF, na kuamua kujisalimisha kwa UN, ambapo, waliombewa kuingiwa Rwanda kwa mipango ya kusafirishwa na kurudi kwa Romania
View attachment 3218136View attachment 3218133
The Rwandan-backed M23 rebels have released captured Romanian mercenaries who were fighting with the Congolese army. As they passed a border, they were chastised by Willy Ngoma, who tapped them mockingly one by one.
news.sky.com
Hizi nchi za kiafrika zinaongozwa na wezi na mafisadi wakubwa .
Wanajeshi wa Kongo kwa hili walitakiwa wamto rais mpumbavu madarakani waweke demokrasia ya kweli au wakae meza moja na waasi waweke utawala wa majimbo ufanye kazi ipasavyo sio utawala wa majimbo kama halafu kila kitu kinasimamiwa na Serikali kuu .
Rais anayetawala nchi yenye madini na kila kitu anashindwa kuajiri wanajeshi na kuwalipa mishahara mizuri. Ni mpumbavu sana huyo Rais anayeirushia Lawama Rwanda wakati hafai hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji . Kwa nini asitoe baadhi ya maeneo yenye dhahabu yanasimamiwa na Jeshi kwa ajili ya kuliwezesha badala yake anawalinda Wezi kutoka Ulaya kwa gharama kubwa . Bora angekaa na Kagame wanajipanga namna ya kutoa huduma kwa watu wa mashariki kwa Kongo na kuweka uhuru kwa wananchi kuishi wanapotaka bila kuulizwa . Yaani wafute pumbavu wa nchi za kiafrika kufungiana mipaka na kudhibiti watu kuhamia sehemu nyingine wanakoona kuna fursa .
Huu ujinga pia upo nchi za Afrika Mashariki watawala wanafunga sheria za kuzuia hata watu kupita kwenda nchi nyingine kama Afrika kusini . Watanzania wanawazuia waethiopia kupita kwenda Afrika kusini . Lakini Afrika kusini haiwakatazi kwenda huko . Huu ni kama uchawi kwa binadamu . Mtu anapita na kujificha kwenye Tanker la mafuta ili aende zake Afrika kusini akatafute riziki lakini mchana kutwa anashindwa kwa gharama kubwa na kupelekwa gerezani kwa gharama ya kodi za watanzania .
Kwa nini asipewe masharti ya kwenda Huko anakokwenda tuu na sio kukaa nchini . Huko ndio wawakatae . Kama Afrika Kusini wangewakataa wasingeenda . Wanaenda kwa sababu wanawapokea .
Sasa sisi kinachotuwashia ni nini ?
Tanzania kama tungekuwa na Watawala wapenda haki tulipaswa tuwasaidie M23 na sio kuwasadia mawakala wa Mabeberu waliojificha kwenye starehe Kinshasa. Nchi yenye wetu zaidi ya mil.100 haina jeshi na rasilimali zinapotosha kuilisha ulaya kwa Karne tano leo tunakwenda kuwasadia kuwaua waafrika wenzao . Tuna akili kweli au ni uhuni wa kutafuta pesa kwa malipo ya Majizi yaliyojificha chini ya UN kulinda utoroshaji na wizi wa madini .
Ikumbukwe kuwa watawala wengi wa duniani ni mawakala wa shetani wapo tayari kugawa na kuuza kila kitu kwa wazungu alimradi wakae madarakani na magari ya kifahari na misafara na ving'ora bila kujali kuwa hao wazungu wanatorosha mpaka waanyama kama wanavyofanya huku kwetu . Kisha Jeshi na polisi wanakaa kimya na usalama wa Taifa na Tanapa lakini wanawabambikia keshi akina Dr. Slaa ili wafie gerezani .Yaani nchi za kiafrika Usalama wa nchi ni madaraka ya mtu mmoja na familia yake . Yaani eti Mgeni kutoka Omani ndiye usalama wa nchi hata kama anapora na kuuza kila kitu kwa wageni bado dola linatumia nguvu kubwa kuhakikisha anatawala hata kama Katiba imetoa fursa kwa wananchi kumkataa kwa sababu ya matendo yake ya wizi na ufisadi na kuuza rasilimali za umma kwa wageni bila huruma kwa kutegemea kuwa dola itamlinda katika uhalifu wake huo wa kuteketeza taifa kiuchumi huku yeye akizidi kuwa bilionea kwa muda mfupi .
Waafrika tumuunge mkono Kagame ,Museveni na M23 ili wazungu wakimbie pale Goma na Afrika kwa ujumla .
Hawa wazungu ndio wanaoleta silaha za kuua waafrika wenzetu .
Mfano uchaguzi unaokuja hapa Kongo ya CCM mabomu ,silaha na risasi na magari ya washawasha yatanunuliwa kwa wingi kama vile suala la uchaguzi ni suala la Vita na uhalifu mkubwa lakini kumbe ni mafisadi yanayolinda ufisadi wao na kusalia madarakani kwa nguvu .
Sasa kama uchaguzi ni vita na vurugu ni bora usifanyike . Kama ukifanyika ni vita na kuuana na kutokana sasa huo uchaguzi ni wa nini ?
Uchaguzi tunaziona waangalizi huru kutoka nje lakini tunataka tuwafurahishe hao hao kwamba tuna demokrasia ya vyama vingi kinafiki.
No Election iwe ni kwa vitendo . Hakuna haja ya kufanya uchaguzi unaoacha wetu na vilema na vifo na watu wengi kufungwa gerezani ni bora nchi nzima wakamatwe wawekwe gerezani siku hiyo ya uchaguzi . Nchi itakua salama zaidi maana CCM watakua wanaendelea na wabunge na madiwani wao waliopatikana kihuni mwaka 2020.