Gone Too Soon: RIP JF Member.....Chetuntu!!!

Gone Too Soon: RIP JF Member.....Chetuntu!!!

1091610.jpg
 
Nimesikitishwa na kupatwa majonzi makuu juu ya kuondokewa na mwenzetu tuliyempenda sana.
Kuna wakati ninajiuliza kama kweli Mungu yupo fair (LoL hata sie Mods tunaulizwa sana hilo swali), lakini kifo kinabakia FUMBO lisilo na majibu wala ufumbuzi zaidi ya Mungu pekee. Kazi yake hatuikosoi kamwe kwani ndiye ajuaye hatima zetu woote kwa wakati wake.

JF na timu yote tunatoa pole za dhati na kuwaombea subira wafiwa pamoja na sisi ktk kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Apumzike kwa amani, na Warehemiwe wafiwa.

DC, i had the same feeling, mara nyingi huwa kuna signs nyingi tu na hatuzisomi

I have met this lady ila kwenye kazi na sikujua kumbe ndiye chetuntu

AND YOU KNOW WHAT?? SHE WAS SERVING PEOPLE IN NEED, KAZI YA WITO

NA MUNGU KAPENDA UA LAKE

what a sad day today

Hivi vifo wakati wa kujifungua vinahuzunisha sana...Mwaka jana tulimpoteza mfanayakazi mwenzetu ambaye alitoka damu nyingi baada ya kufanyiwa operation. Wakati mume wake anatolewa damu yeye akaaga dunia...na pia mtoto alifariki...It was so traumatic kiasi kwamba huwa sipendi kumuona mume wake na watoto 2 aliowaacha hai...Hata daktari aliyemfanyia operation alichanganyikiwa!!

Nasikia dini nyingine zinaamini kuwa kuzaa ni nusu ya kufa........Kama kweli hili tungelikumbuka siku zote basi tungewaheshimu mama zetu waliotuzaa na wake zetu waliotupatia watoto!!

Ngoja nikapumzike kwanza...I have been deeply touched......!!

Babu DC!
 
Mungu ampe makazi mema katika makazi mema ya peponi -amen

Aspirin, Kimey na wana JF wengine tuwe pole na msiba.

Tumetoka kwa Mola na kwake ni marejeo yetu
 
Kwa nini aliamua kuandika hayo hapo (blue)???

Masikini ameishia njiani (just missed a step) kabla ya kufika hiyo ward ya mavuno na furaha!!

I am speechless!!

Ndo alikokuwa anafanyia kazi.
Alikuwa anafanya kazi kwenye kambi ya wakimbizi huko Kasulu. Na alikuwa akiwahudumia watoto kwenye Paedriatique ward. Ndo maana akaichagua hiyo kama Loc. yake.
 
Hivi vifo wakati wa kujifungua vinahuzunisha sana...Mwaka jana tulimpoteza mfanayakazi mwenzetu ambaye alitoka damu nyingi baada ya kufanyiwa operation. Wakati mume wake anatolewa damu yeye akaaga dunia...na pia mtoto alifariki...It was so traumatic kiasi kwamba huwa sipendi kumuona mume wake na watoto 2 aliowaacha hai...Hata daktari aliyemfanyia operation alichanganyikiwa!!

Nasikia dini nyingine zinaamini kuwa kuzaa ni nusu ya kufa........Kama kweli hili tungelikumbuka siku zote basi tungewaheshimu mama zetu waliotuzaa na wake zetu waliotupatia watoto!!

Ngoja nikapumzike kwanza...I have been deeply touched......!!

Babu DC!
Mwacheni MAMA AITWE MAMA!
 
We acha tu mimi huyu dada ni mtu wa pili yaani ninaowafahamu kabisa ndani ya mwezi huu mmoja wamefariki kisa uzazi, nimechoka kabisa hapa wamama tuna tabu ni Mungu tu aingilie kati.

Pole sana Maty,

Hili suala linaumiza sana kwani vifo vingi vinavyotokana na uzazi vinazuilika endapo huduma zetu zingekuwa nzuri..........

Tuzidi kumwomba Mungu awape pumziko la milele na wakufatia dhambi zao kwani wamepoteza maisha wakati wakipigani uhai wa watoto wao. Pia tumwombe Mungu awanusuru wengine wanaosubiri kuifanya kazi hii muhimu ya kuujaza ulimwengu...!!

Babu DC!
 
Pole sana babu ODM........haswa kwa kitendo cha kumtafuta kwenye simu na baadae unapata taarifa ameshafariki daaahh inauma sana..........Mungu akupe faraja na wanaJF wote zaidi hasa familia yake
 
Pole sana babu ODM........haswa kwa kitendo cha kumtafuta kwenye simu na baadae unapata taarifa ameshafariki daaahh inauma sana..........Mungu akupe faraja na wanaJF wote zaidi hasa familia yake
Inauma sana aisee!
 
sasa utaratibu unakuwaje jamani? hatuendi hata kumpumzisha mwenzetu? au tunaomboleza tu humuhumu jamvini
 
Sote tu mavumbi na mavumbini tutarudi,..Mungu atutie nguvu wote walioguswa na hili.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani.
 
Back
Top Bottom