Good doctor!

Good doctor!

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Ilikuwa inakaribia saa sita na nusu usiku,nimetoka wash room tayar kwenda kulala,,,,mara mdogo wangu ananigongea mlango na kusema "broo chakula hakikai tumboni na kibaya Zaidi najisikia kutapika Mda wote lakini nikienda wash room hakuna kinachotoka hii Hali inaniumiza Sana".

Nikajisemea Moyoni huyu dogo nae muoga kweli WA kuumwa si avumilie Tu huenda dawa zinamkoroga tumboni ndio maana anajisikia hivyo,ukichukulia ana kama siku mbili tatu toka amalize dozi ya malaria. Nikamwambia "au labda dawa hizo zinakuchefua huenda mpaka kesho utakuwa Sawa" Kwa jinsi alivyokuwa anajisikia aliniambia " broo naomba nipeleke hospitali japo nikapate sindano ya kuzuia kutapika" daah nikimcheki namuona kabisa kwenda hospital ndio option iliyobakia,,,,,,wanasema damu nzito kuliko maji,Ila kama maji yangekuwa mazito kuliko damu ningemwambia broo jikaze twende kesho halafu ningezama rumu na kulala!

Basi Safar ya kwenda hospitali ikaanza,,,mara paap dokta huyu hapa! Dogo akajielezea kuwa amekunywa dozi siku mbili tatu zilizo pita lkn jioni Ile Hali imebadilika na chakula hakikai kabisa kabatini so anahitaji huduma ya kuzuia kutapika,,,,dokta akauliza maswali mawili matatu kujua historia ya tatizo,akaelezwa lakini Mimi na mdogo wangu tukaona kama dokta anazunguka Sana wkt Sisi tunataka sindano ya kuzuia kutapika,,,,mwisho wa siku dokta akasema inaelekea bado malaria ipo,nikamwambia lakini dokta, je si itahitajika baada ya wiki moja labda ndo kujua kama IPO au laa ukichukulia kamaliza dozi juzi Tu? Dokta akapozi Kwanza kama mtu ambaye anatusoma mawazo yetu na alikuwa mstaarabu Sana pamoja na Sisi sio wataalamu lkn tukajifanya kuchalenge utaalaamu! Akasema sasa kama dozi haijamsadia hata ukisubiri wiki moja ipite ndo utakuwa Una prove nini sasa? Kwa sauti ya upole na utulivu alitujibu.

Basi Kwa kawaida dogo vidonge huwa hapendi,so akachagua sindano Kwa siku tano akamaliza dozi na akawa freshi kabisa na msosi ulikuwa unakaa kabatini vizur kabisa na anaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Moral of the story :

Kwanza,,,, usidharau Jambo lolote hata likiwa dogo,,,,Mimi na bwana mdogo tulijua dawa zilikuwa zinamvuruga tumboni Tu so haikuwa ishu kubwa kivile,kumbe ugonjwa bado ulikuwa unamtafuna.

Pili,,,, Kwa kila Jambo waachie wenye ujuzi nalo,usileta bla bla bla za vijiweni,tuheshimu Utaalamu siku zote.

Ni hayo Tu!
 
Aliwahi kunisimulia rafiki yangu wakati bado mdogo mama yake aliumwa wakampeleka hospital hajitambui, kufika hospitali daktari akasema awekewe drip. Nurse akaandaa drip fulani, rafiki yangu kwasababu anajua mama yake ni diabetic akamkatalia nurse asiweke drip hio ndipo nurse akamuuliza kwanini akamwambia kwasababu mama yangu ana kisukari! Nurse akawa mpole, bila kuhoji yule mama alikuwa anakufa mapema kwa makosa ya nurse.
Kwahio si kila jambo ukubali tu kisa ni mtaalam kasema hata wao huwa wanapitiwa na wana mambo mengi kama binadamu wengine.
 
Nadhani hata huyo dogo pia alikua na utaalamu kuhusu hilo drip, labda amesomea mambo ya afya.

Sidhani kama "Aisha Chukua yote" wa Tandika anaweza kujua drip hili limebeba dawa aina gani na zinaweza kureact namna gani kwa mtu mwenye diabetes!
 
Alikuwa mdogo. Ni ile hali ya kujua status ya afya ya ndugu au mzazi wako. Mfano ukijua ndugu yako ana kisukari anaweza kuanguka ukawaambia watu mleteeni pipi au fanta tu akawa fresh.
 
Yeah, kwa kesi za namna hii ni sahihi. Hata mateja wanajua namna ya kuwasaidia wenzao wakizidisha.

Ila kuna sehemu ukiweka ujuaji lazima uyakanyage!
 
Aliwahi kunisimulia rafiki yangu wakati bado mdogo mama yake aliumwa wakampeleka hospital hajitambui, kufika hospitali daktari akasema awekewe drip. Nurse akaandaa drip fulani, rafiki yangu kwasababu anajua mama yake ni diabetic akamkatalia nurse asiweke drip hio ndipo nurse akamuuliza kwanini akamwambia kwasababu mama yangu ana kisukari! Nurse akawa mpole, bila kuhoji yule mama alikuwa anakufa mapema kwa makosa ya nurse.
Kwahio si kila jambo ukubali tu kisa ni mtaalam kasema hata wao huwa wanapitiwa na wana mambo mengi kama binadamu wengine.
Madaktari hawakataliwi ila wanaulizwa ili upewe sababu kwanini kamuandikia hivyo kama kapitiwa atajua na atakushukuru ila usikurupuke na elimu yako ya mtaani ukaanza kumprovoke doctor, mfano hapo kuna drip za aina nyingi , mgonjwa wakisukari kimepanda huduma ya kwnza ni drip ya NS ili kushusha maan ni maji tu, ila sio Drip zenye glucose, ss kama alimpa iyo ilikua sawa haina madhara, uyo mtaalamu amemvumilia uyo dogo
 
Alikuwa anampa yenye glucose.
 
Alikuwa mdogo. Ni ile hali ya kujua status ya afya ya ndugu au mzazi wako. Mfano ukijua ndugu yako ana kisukari anaweza kuanguka ukawaambia watu mleteeni pipi au fanta tu akawa fresh.
Kisukari gani umpe soda cha kupanda au kushuka? Hizi elimu mitaan hiz Mtawaua mam zenu nyieeee uje umpe soda akiwa na sukari yakupanda unialike msiban
 
Kwweli
Aliwahi kunisimulia rafiki yangu wakati bado mdogo mama yake aliumwa wakampeleka hospital hajitambui, kufika hospitali daktari akasema awekewe drip. Nurse akaandaa drip fulani, rafiki yangu kwasababu anajua mama yake ni diabetic akamkatalia nurse asiweke drip hio ndipo nurse akamuuliza kwanini akamwambia kwasababu mama yangu ana kisukari! Nurse akawa mpole, bila kuhoji yule mama alikuwa anakufa mapema kwa makosa ya nurse.
Kwahio si kila jambo ukubali tu kisa ni mtaalam kasema hata wao huwa wanapitiwa na wana mambo mengi kama binadamu wengin

Aliwahi kunisimulia rafiki yangu wakati bado mdogo mama yake aliumwa wakampeleka hospital hajitambui, kufika hospitali daktari akasema awekewe drip. Nurse akaandaa drip fulani, rafiki yangu kwasababu anajua mama yake ni diabetic akamkatalia nurse asiweke drip hio ndipo nurse akamuuliza kwanini akamwambia kwasababu mama yangu ana kisukari! Nurse akawa mpole, bila kuhoji yule mama alikuwa anakufa mapema kwa makosa ya nurse.
Kwahio si kila jambo ukubali tu kisa ni mtaalam kasema hata wao huwa wanapitiwa na wana mambo mengi kama binadamu wengine.
Kweli mkuu upo sahihi kabisa nao pia ni binadamu
 
Point sana big boy
 
Madaktari hawakataliwi ila wanaulizwa ili upewe sababu kwanini kamuandikia hivyo kama kapitiwa atajua na atakushukuru ila usikurupuke na elimu yako ya mtaani ukaanza kumprovoke doctor, mfano hapo kuna drip za aina nyingi , mgonjwa wakisukari kimepanda huduma ya kwnza ni drip ya NS ili kushusha maan ni maji tu, ila sio Drip zenye glucose, ss kama alimpa iyo ilikua sawa haina madhara, uyo mtaalamu amemvumilia uyo dogo
Na Hilo kumuuliza dokta kwanini kamuandikia dawa flani ni zuri ingawa Kwa madokta wa kibongo naona kama ukiwahoji hoji kama wana wanamind hivi,,,,Ila wazungu utakuta wanatoa maelezo vizur Kwa mgonjwa mpaka anaelewa
 
Nadhani hata huyo dogo pia alikua na utaalamu kuhusu hilo drip, labda amesomea mambo ya afya.

Sidhani kama "Aisha Chukua yote" wa Tandika anaweza kujua drip hili limebeba dawa aina gani na zinaweza kureact namna gani kwa mtu mwenye diabetes!
Mkuu ukinunua gari bovu lazima utakuwa fundi.
Huyo dogo alijua aina za drips kwasababu amekuwa na mgonjwa wa kisukari muda mrefu so amejifunza kupitia uzoefu huo labda.
 
Kisukari gani umpe soda cha kupanda au kushuka? Hizi elimu mitaan hiz Mtawaua mam zenu nyieeee uje umpe soda akiwa na sukari yakupanda unialike msiban
Usijifanye wewe ndio una akili pekee, mtu hadi afikie kumpa mgonjwa soda flani ujue wameshauriwa na daktari.
 
Kisukari gani umpe soda cha kupanda au kushuka? Hizi elimu mitaan hiz Mtawaua mam zenu nyieeee uje umpe soda akiwa na sukari yakupanda unialike msiban
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Aliwahi kunisimulia rafiki yangu wakati bado mdogo mama yake aliumwa wakampeleka hospital hajitambui, kufika hospitali daktari akasema awekewe drip. Nurse akaandaa drip fulani, rafiki yangu kwasababu anajua mama yake ni diabetic akamkatalia nurse asiweke drip hio ndipo nurse akamuuliza kwanini akamwambia kwasababu mama yangu ana kisukari! Nurse akawa mpole, bila kuhoji yule mama alikuwa anakufa mapema kwa makosa ya nurse.
Kwahio si kila jambo ukubali tu kisa ni mtaalam kasema hata wao huwa wanapitiwa na wana mambo mengi kama binadamu wengine.
D5 huwez mpa mtu bila kumpima sukari mkuu labda nurse alijisahau
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] we mwenyewe hujafafanua, kisukari kipi tunampa mgonjwa au mradi ana kisukari tumpe soda?
Nimesema mtu anaejua status ya ndugu yake. Sio random. Jaribuni kutuliza vichwa kabla ya kuvamia comments za watu.
 
Back
Top Bottom