Good news: Diamond athibitisha Wasafi Tower kukamilika 95%

Good news: Diamond athibitisha Wasafi Tower kukamilika 95%

Mbona maflaiova ya mfugale yalivyojaa maji kwa mvua ya siku moja mkaleta mapicha ya uk,germany ,us kwamba na wao madaraja yao yanajaa maji? kwani Domo ana tofauti gani na Dre au Meek Mill? Ungekuwa ushakaa USA ungeona ni watu wa kawaida sana hao....Kwani USA hakuna Homeless/Omba omba?
Unatia aibu wewe,

afu mtu mzima sasa[emoji41]
 
Mkuu namkubali diamond ila apo kusema kwamba ndo mwanamuziki anamiliki radio na television afrika sio kweli kuna mwanamuziki anaitwa salif keita yupo mali uko ana media house tangu miaka ya 90 na ana mpunga mrefu tu.
Na ndo msanii mwenye hela kuliko wote Africa kama sikosei
 
Celebrity worship syndrome ni ugonjwa wa akili ambapo mtu hutokea kumpenda mtu maarufu kupita kiasi.

(Kufatilia na kusifia/kupenda kila kitu anachofanya kwenye kazi yake na maisha binafsi.)

Thank you so much, nilihisi Huyu jamaa ana ugonjwa, Upi sasa ndo ilikuwa changamoto?
 
Kweli ambaye amepewa kapewa tuu, na huu msemo umejidhihirisha mbele yaDiamond Platinumz kuwa ndo msanii ana yejituma kwa bidii zote kuliko msanii yeyote hapa bongo.

Pia ndo msanii ambaye anamiliki TV na radio Africa nzima pekeake.

Pia ndo msanii ambaye Tv na radio yake kwa Mara ya kwanza vitakuwa vinapatikana kwenye miliki yake, na sio kama radiona Tv Kama clouds, efm na nyingine zinazotegemea leasing area ili kuoperate.

HAIL TO DIAMOND PLATINUMZ THE G. O. A. T[emoji122]
the g o a t hail hail hatari sana kufanya kazi kwa bidii zote na kujituma masonic rule 4
 
Non Sense!!!!!!! TCRA si wameweka wazi wamiliki na hisa za wasafi? Mbona unajitoa ufahamu? Mnaona JF wamejaa maburula kama nyinyi? Huyo msaniii wenu kupata vijishare vya wasafi mikelele mwaka mzima,je angekuwa na 100% share si tusingelala? Ebu mwambie awagugo kina Dre , Diddy ,Birdman walivyo na ma investment ya hatari halafu hawana YOWE hata kidogo!! Huyo msanii wenu ana utajiri wa kibongo tu.

Mzee mzima kumbe na wewe una mijilasi ya nguvu.
 
Mkuu unapresent vipi habari yako? Title wasafi tower ila content haina chochote kinachohusu wasafi tower
 
Unajuwa matukio kama haya yametokea sana nchi nyingi tu mtu ghafla kuibuka na pesa na miradi ikaja kuwa majanga. Kuwa na pesa sio dhambi na anaweza kuwa napesa tatizo linakuja hapa, inawezekana watu wanatakatisha pesa uwezekano ni mkubwa, kwa serikali makini na hii imetokea sana nchi nyingi tu. Ni kumwita ok na kufanya uchunguzi mdogo tuoneshe hisa zenu na pesa zilichangwa kupitia chanzo kipi? vyanzo vya pesa yako, mapato ya mwaka, matumizi ya mwaka, kodi za mwaka, na kujenga tower ina maana umeongeza mtaji umetokana na nini kuna maswali mengi na majibu yakitoka tunaweza kushika vichwa sasa je tuna vitengo maalumu vya kuangalia haya mambo na hapa sio Wasafi tu wako wengi tu. Huwezi mtu ghafla kaibuka tu hata mtaani kwako utasikia alikuwa hana kitu mwaka jana tu kaangusha nyumba hapa ananunua mpaka mtaa serikali kimya na watu wanaona sifa, kuwa tajiri sio dhambi ila utajiri umetokana na nini? Utakatishaji pesa ni tatizo kubwa duniani mara nyingi watu kuogopa mkono wa serikali wanawatumia hawa kuficha dhambi zao haiwezekani mtu mwingine ana share 51% halafu ajifiche halafu mtu kama babu tale kaweka sura mbele, kuna kitu hakijawekwa wazi hii ni kampuni kuna wenye share ni lazima itajwe thamani ya share na zimechangiwa kivipi sio kuleta number tu 51%, 45% haitoshi.
 
45% sio mchezo aisee kwa biashara kama ile.
Ndio maana kuna vitu vingi haviko wazi hata wale ma managers wake watatu wanasema wao sio wasindikazaji wana share sasa hatujui share zipi katika hiyo 45%? je 45% wanaongelea katika capital au profit? Mimi nadhani pale kuna jambo limejificha ni lazima waoneshe ok kampuni thamani yake 2 billion capital wewe ulichangia billion cash chanzo kipi mkopo au? na wale kina Tale share zao ni zipi katika nini maswali mengi mimi naamini kuna watu wanaficha pesa pale kama kichaka. nchi yoyote ukiweka kampuni yako public basi lazima ikaguliwe ilitokea huko India kampuni SAHARA siku alipoweka public kampuni zake mbili madudu yaliyotoka huko hatari.
 
Kwani kuwa na redio na Tv ndio utajiri, lazima tujuwe revenue-operating cost= profit hapo katika profit ndio upate returning kwanza ua uwekezaji sasa inategemea returning ni miaka mingapi mpaka watu waanze kula profit.
 
Inaonekana waswahili wengi wanaugua huu ugonjwa
Celebrity worship syndrome ni ugonjwa wa akili ambapo mtu hutokea kumpenda mtu maarufu kupita kiasi.

(Kufatilia na kusifia/kupenda kila kitu anachofanya kwenye kazi yake na maisha binafsi.)
 
Ndio maana kuna vitu vingi haviko wazi hata wale ma managers wake watatu wanasema wao sio wasindikazaji wana share sasa hatujui share zipi katika hiyo 45%? je 45% wanaongelea katika capital au profit? Mimi nadhani pale kuna jambo limejificha ni lazima waoneshe ok kampuni thamani yake 2 billion capital wewe ulichangia billion cash chanzo kipi mkopo au? na wale kina Tale share zao ni zipi katika nini maswali mengi mimi naamini kuna watu wanaficha pesa pale kama kichaka. nchi yoyote ukiweka kampuni yako public basi lazima ikaguliwe ilitokea huko India kampuni SAHARA siku alipoweka public kampuni zake mbili madudu yaliyotoka huko hatari.
Sallam sk na Babu tale Ni mamenager wa diamond kwenye upande wa label sio kwenye media na pia ujue sallam sk na Babu tale Ni waajiriwa tu wa diamond kwenye music only
 
Back
Top Bottom