Unajuwa matukio kama haya yametokea sana nchi nyingi tu mtu ghafla kuibuka na pesa na miradi ikaja kuwa majanga. Kuwa na pesa sio dhambi na anaweza kuwa napesa tatizo linakuja hapa, inawezekana watu wanatakatisha pesa uwezekano ni mkubwa, kwa serikali makini na hii imetokea sana nchi nyingi tu. Ni kumwita ok na kufanya uchunguzi mdogo tuoneshe hisa zenu na pesa zilichangwa kupitia chanzo kipi? vyanzo vya pesa yako, mapato ya mwaka, matumizi ya mwaka, kodi za mwaka, na kujenga tower ina maana umeongeza mtaji umetokana na nini kuna maswali mengi na majibu yakitoka tunaweza kushika vichwa sasa je tuna vitengo maalumu vya kuangalia haya mambo na hapa sio Wasafi tu wako wengi tu. Huwezi mtu ghafla kaibuka tu hata mtaani kwako utasikia alikuwa hana kitu mwaka jana tu kaangusha nyumba hapa ananunua mpaka mtaa serikali kimya na watu wanaona sifa, kuwa tajiri sio dhambi ila utajiri umetokana na nini? Utakatishaji pesa ni tatizo kubwa duniani mara nyingi watu kuogopa mkono wa serikali wanawatumia hawa kuficha dhambi zao haiwezekani mtu mwingine ana share 51% halafu ajifiche halafu mtu kama babu tale kaweka sura mbele, kuna kitu hakijawekwa wazi hii ni kampuni kuna wenye share ni lazima itajwe thamani ya share na zimechangiwa kivipi sio kuleta number tu 51%, 45% haitoshi.