GOOD NEWS: Ni Emmanuel OKWI ndani ya YANGA, asaini Miaka Miwili.

GOOD NEWS: Ni Emmanuel OKWI ndani ya YANGA, asaini Miaka Miwili.

Ni usajili mzuri kwa Yanga ingawaje Okwi niliyemshuhudia Chalenji kidogo kiwango chake kilikuwa chini ukilinganisha na misimu ya nyuma akiwa Simba SC...

Ngoja aje, anolewe na mwisho tumuone uwanjani atakuwa na lipi jipya...
 
Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nhcini Uganda
Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.

Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na
nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa
msimu wa 2015/2016.

Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo
mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati
ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.

Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji watano wa kimataifa
wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.

Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki
kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma
Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.

Baraka Kizuguto Afisa Habari – Young Africans SC
Disemba 15, 2013.

Huu ni uandishi wa kiubabaishaji, saa hizi ni saa 4 na dakika 37, halafu mtu anasema eti dirisha dogo limefungwa leo saa 6 usiku!
 
Naona waliowapiga tano mmewaamulia: mpaka sahivi mnao watatu, Yondani, Kaseja na Okwi.

Bado Julio, anapigiwa simu hapokei; akipokea tu utasikia kesho kuwa ametua jangwani kuwa kocha wa mipasho na saikolojia.
 
Dah Rage aisee mbona unatunyima raha mjini hapa!! Kwa nini unatufanyia hivi wana Simba wenzako haya bhana kina Chanogo si ndio mastaa wetu..... Dah hii habari sio nzuri hata kidogo kwetu
 
Yanga imara yanga imara....simba makopo simba makopo
 
Dah Rage aisee mbona unatunyima raha mjini hapa!! Kwa nini unatufanyia hivi wana Simba wenzako haya bhana kina Chanogo si ndio mastaa wetu..... Dah hii habari sio nzuri hata kidogo kwetu

Mmejiandaaje Wiki ijayo?
 
hiyo ni minor error, fact ni Okwi katua jangwani.

Hivi Yanga anaengoza kamati ya usajili ndio huyu Bin clebb? Kwakweli nikianzia na issue ya Mbuyu Twite mpaka Okwi, basi ukiona amemsogelea demu wako inabidi umuombe samahani akuachie maana kwa speed hii hakuna demu wa kuruka mbele yake kama akimtaka.
 
Tatizoow Simba na Yanga wanasajilii kwa kukomoana wala hawafuati Benchi la ufundi,,,wehu wote
 
kuchangia hapa i ngumu kwa sababu asiyeeleweka ni tapeli wetu Rage, kama unamfuatilia vizuri tangu wakati wa Asamoah, Mbuyu Twite na hata hawa wawili wa juzi utagundua unahitaji kutulia sana kuchangia kuhusu Okwi na Etoile
Mbona kama siwaelewi cos simba bado wanadai pesa yao hawa yanga hawajitaki wanataka kunyang'anywa point haya ngoja tuone africa sio tanzania cos wamezoea kupindisha sheria tff kama walivyofanya kwa twite,yondan na ngasa ngoja tuone inakuwaje na kama wakifanikiwa basi kuna tatizo tena kubwa la kiufundi simba maybe hawajui sheria au wanapotoshwa
 
kama wewe ni mpenzi wa Simba na Aseno basi wiki hii itakua imekuishia vibaya sana
 
uko akilini mwangu Watu8, huenda pia benchi limemshusha lakn bado ni mchezaji mzuri, kingine ni kwamba bado tunasajili kwa kumbukumbu, tizama Simba leo hii bado wanamzungumzia Oloya bila kujua kiwngo chake au hata usajili wa Berko ni kumbukumbu zaidi maana kwa kweli ameshuka sana nilivyomuona mazoezini, amegain weight
Ni usajili mzuri kwa Yanga ingawaje Okwi niliyemshuhudia Chalenji kidogo kiwango chake kilikuwa chini ukilinganisha na misimu ya nyuma akiwa Simba SC...

Ngoja aje, anolewe na mwisho tumuone uwanjani atakuwa na lipi jipya...
 
......Bin Kleb alisema lengo la Yanga SC ni kufanya vizuri katika Ligi ya Mbingwa Afrika mwakani na ndiyo maana wameamua kuimarisha timu kwa kusajili wachezaji wazuri.

hii nimeipenda sio eti unasajili mchezaji kulipa goli 5.................nawatakia kila la heri watani japo najua kama Rage si mbabaishaji basi Simba wana locus standi
 
Tatizoow Simba na Yanga wanasajilii kwa kukomoana wala hawafuati Benchi la ufundi,,,wehu wote

Mbona una hasira sana? Yanga ya sasa inaweza kucheza soka la kimataifa na si kitaifa.
 
Back
Top Bottom