Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nhcini Uganda
Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.
Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na
nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa
msimu wa 2015/2016.
Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo
mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati
ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.
Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji watano wa kimataifa
wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.
Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki
kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.
Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma
Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.
Baraka Kizuguto Afisa Habari Young Africans SC
Disemba 15, 2013.
Naona waliowapiga tano mmewaamulia: mpaka sahivi mnao watatu, Yondani, Kaseja na Okwi.
Huu ni uandishi wa kiubabaishaji, saa hizi ni saa 4 na dakika 37, halafu mtu anasema eti dirisha dogo limefungwa leo saa 6 usiku!
Bado Julio, anapigiwa simu hapokei; akipokea tu utasikia kesho kuwa ametua jangwani kuwa kocha wa mipasho na saikolojia.
hiyo ni minor error, fact ni Okwi katua jangwani.
Dah Rage aisee mbona unatunyima raha mjini hapa!! Kwa nini unatufanyia hivi wana Simba wenzako haya bhana kina Chanogo si ndio mastaa wetu..... Dah hii habari sio nzuri hata kidogo kwetu
hiyo ni minor error, fact ni Okwi katua jangwani.
Mbona kama siwaelewi cos simba bado wanadai pesa yao hawa yanga hawajitaki wanataka kunyang'anywa point haya ngoja tuone africa sio tanzania cos wamezoea kupindisha sheria tff kama walivyofanya kwa twite,yondan na ngasa ngoja tuone inakuwaje na kama wakifanikiwa basi kuna tatizo tena kubwa la kiufundi simba maybe hawajui sheria au wanapotoshwa
Ni usajili mzuri kwa Yanga ingawaje Okwi niliyemshuhudia Chalenji kidogo kiwango chake kilikuwa chini ukilinganisha na misimu ya nyuma akiwa Simba SC...
Ngoja aje, anolewe na mwisho tumuone uwanjani atakuwa na lipi jipya...
Tatizoow Simba na Yanga wanasajilii kwa kukomoana wala hawafuati Benchi la ufundi,,,wehu wote
Yuko nchini China huyo!Huu ni uandishi wa kiubabaishaji, saa hizi ni saa 4 na dakika 37, halafu mtu anasema eti dirisha dogo limefungwa leo saa 6 usiku!
Tatizoow Simba na Yanga wanasajilii kwa kukomoana wala hawafuati Benchi la ufundi,,,wehu wote