Goodluck Gozbert sio mwimbaji wa Gospel

Mkuu Chachasteven, Gozbert mimi mwenyewe nilikuwa namtilia mashaka sana mara niliposikia nyimbo zake kwa mara ya kwanza, lakini wimbo huu alioutoa ndio ulithibitisha kwamba huyo hakiki sio Mtumishi, yaani sio muimbaji wa Nyimbo za Injili bali huyo ni wale wanaoitwa wasanii wa nyimbo za injili, itoshe tu kutambua na hakuna haja ya kubishana hapa, naamini hata yeye mwenyewe analijua hilo, na anashangaa anapoona kuna watu wanamtetea, Kuimba Injili inataka Mtu uwe na Wito na pia Ushuhuda, sio kujiimbia tu kwa sababu unaweza kuimba, sijajua wewe msimamo wako kiimani ni upi, yawezekana unaweza kuwa unamtetea ukifurahi kuona jinsi anavyowapoteza watu wengi watakaochagua kumfuata, lakini kama wewe unatamani kuona watu wanapewa iliyo kweli kwenye Injili nadhani tusaidiane kuwakosoa watu kama Gozbert waache mara moja kusaidia wanaoutukana Ukristo kwa sababu ya style zao za Uimbaji, nakuhakikishia asipokemewa atakuja kufanya vituko sana kwenye aina hiyo ya uenezaji wa Injili.
 
umejibu kama goodluck, au manager wake! Umeeleza Vyema
 
Vigezo vya kujua huyu anaimba GOSPEL ni vip ?
 
Vigezo vya kujua huyu anaimba GOSPEL ni vip ?
Hili ni swali zuri sana, ila najua mleta uzi hawezi kulijibu kwa sababu hajafanya tafiti za kutosha juu ya malalamiko yake. Simlaumu, hata hivyo, kwa sababu ni haki ya kila mtu kuhoji ingawa maswali aliyonayo kayaweka kama mtazamo na hali halisi. Yaani hajataka kuuliza ila amekuja kutuambia Gozbert sio muimba Gospel na anataka tukubali. Kigezo alichokitumia sasa! Ni taabu tupu.

Pia hii ni mada ngumu na yenye mjadala mrefu sana, ila nitajitahidi kuifanya iwe fupi na inayoeleweka na nitapokea mapendekezo na nyongeza yeyote kutoka kwa mtu yeyote.

Kigezo cha kujua kwanini wimbo unaweza kuwa gospel na mwingine hauwezi kuwa gospel ni mashairi yanayoimbwa ndani ya wimbo husika na sio aina ya mdundo na vitendo vilivyoonekana kwenye video. Naamini kama mwenye wimbo amesambaza injili basi hiyo ni gospel music.

Uzuri wa Gospel ni kwamba imejigawa mara mbili, yaani kuna praise and worship, au kwa kiswahili, Kusifu na kuabudu au vyote kwa pamoja vikachanganywa kwenye wimbo mmoja. Kwa kutumia wimbo wa Gozbert huo wa nibadilishe ni ladha ya kuabudu. Kuwa mnyenyekevu na kuomba kwa Mungu. Mashairi yanajieleza vizuri... Nadhani mdundo ulitumika kwa maksudi kuweka hisia ya utambuzi kwa watu. Hakuna kilichotokea bahati mbaya. Na bahati nzuri hata biblia inatutaka tuseme ukweli na Gozbert alisema ukweli mule ndani. Shida ni kuwa tumekariri, hatutaki ku evolve. Hii ni 2020 watu bado wanataka tuishi kama 1950.. Inashangaza maana hata biblia zina matoleo mapya kila siku. Kwanini kwaya zisiwe na mfumo mpya?? 🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…