Goodluck Gozbert sio mwimbaji wa Gospel

Goodluck Gozbert sio mwimbaji wa Gospel

Inasikitisha sana, pamoja na kuwa teknolojia na intaneti vina faida lukuki kwa watumiaji, lakini hasara zake bado ni kubwa sana. Siku hizi mtu yeyote tu anaweza akabishana na mtu aliyekaa darasani kwa miaka hata 7 na mwenye uzoefu wa taaluma fulani kwa miaka zaidi ya 6+. Hatari tupu.
 
Yes technolojia imesaidia kuwaambia wasomi kuwa theory za darasani ni tofauti na uhalisia wa maisha...
Inasikitisha sana, pamoja na kuwa teknolojia na intaneti vina faida lukuki kwa watumiaji, lakini hasara zake bado ni kubwa sana. Siku hizi mtu yeyote tu anaweza akabishana na mtu aliyekaa darasani kwa miaka hata 7 na mwenye uzoefu wa taaluma fulani kwa miaka zaidi ya 6+. Hatari tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aijalishi upo kwenye imani gani ila kwa Miungu na mitume wote ujumbe ni mmoja tu "Mpende jirani yako kama nafsi yako"....Ukisema unampenda mtu bila matendo si kitu....Matendo ndiyo kipimo pekee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni swali zuri sana, ila najua mleta uzi hawezi kulijibu kwa sababu hajafanya tafiti za kutosha juu ya malalamiko yake. Simlaumu, hata hivyo, kwa sababu ni haki ya kila mtu kuhoji ingawa maswali aliyonayo kayaweka kama mtazamo na hali halisi. Yaani hajataka kuuliza ila amekuja kutuambia Gozbert sio muimba Gospel na anataka tukubali. Kigezo alichokitumia sasa! Ni taabu tupu.

Pia hii ni mada ngumu na yenye mjadala mrefu sana, ila nitajitahidi kuifanya iwe fupi na inayoeleweka na nitapokea mapendekezo na nyongeza yeyote kutoka kwa mtu yeyote.

Kigezo cha kujua kwanini wimbo unaweza kuwa gospel na mwingine hauwezi kuwa gospel ni mashairi yanayoimbwa ndani ya wimbo husika na sio aina ya mdundo na vitendo vilivyoonekana kwenye video. Naamini kama mwenye wimbo amesambaza injili basi hiyo ni gospel music.

Uzuri wa Gospel ni kwamba imejigawa mara mbili, yaani kuna praise and worship, au kwa kiswahili, Kusifu na kuabudu au vyote kwa pamoja vikachanganywa kwenye wimbo mmoja. Kwa kutumia wimbo wa Gozbert huo wa nibadilishe ni ladha ya kuabudu. Kuwa mnyenyekevu na kuomba kwa Mungu. Mashairi yanajieleza vizuri... Nadhani mdundo ulitumika kwa maksudi kuweka hisia ya utambuzi kwa watu. Hakuna kilichotokea bahati mbaya. Na bahati nzuri hata biblia inatutaka tuseme ukweli na Gozbert alisema ukweli mule ndani. Shida ni kuwa tumekariri, hatutaki ku evolve. Hii ni 2020 watu bado wanataka tuishi kama 1950.. Inashangaza maana hata biblia zina matoleo mapya kila siku. Kwanini kwaya zisiwe na mfumo mpya?? 🤔
Matoleo yapi hayo ya Biblia unayo refer ?, Neno la Mungu ni lilelile Jana, Leo, Kesho na hata milele,.
 
H

Hamna gospel pale clouds wanamdanganya akaimbe kwenye fiesta washabiki wameshika mibia mikononi wengine wanabakana,wamevaa vichupi tu gospel gani!..ni staili tu ya kupiga hela
Wamebakana? ushaidi upo?

hata kama wamebakana kwani neno la Mungu si limeletwa kwa ajili yao? au lililetwa kwa wasafi wa moyo? la hasha na watu hao duniani sidhani kama wapo neno lililetwa kwa wakosefu na wachafu wa moyo Gozbet kuiba fiestani sioni kama ni kosa maana wapo wanao furahia na kubarikiwa kwa uimbaji

Hao wanao bakana ni sawa na anae ingia kanisani/msikitini kutafuta demu alafu lawama umtupie Padri/shekh au Wanakwaya
 
[emoji23][emoji23][emoji23],,,"An expression of gospel"....Daaah!!
Troublemaker,
Lengo la mimi kumuomba jamaa akasikilize hiyo albamu ni kumrahisishia kuelewa muziki wa injili ni mpana kuliko anavyofikiria yeye. Wataalamu wa muziki wamekaa chini kuitafsiti hio albamu ni nyimbo za gospel licha ya midundo na rap system.

Staili ya uimbaji haijalishi. Kinachojalisha ni ujumbe unaoimba. Je unaakisi injili au unapinga. Kwa kipimo hicho cha ujumbe ndiyo maana halisi ya kuchuja ipi ni injili na ipi siyo injili.

Na wewe kasikilize hiyo albam halafu uje. Na kwa nyongeza kipindi Kanye anatoa hiyo albamu alisema haimbi tena nyimbo za kidunia, na hajabadilisha aina ya flow. Tofauti ni kwambwa anamsiu na kumuabudu Mungu (wake) kwa ku rap.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matoleo yapi hayo ya Biblia unayo refer ?, Neno la Mungu ni lilelile Jana, Leo, Kesho na hata milele,.
Tatizo haufuatilii. Unaleta hoja kwa mambo ambayo hauna uhakika nayo... Fuatilia kwanza, ndugu yangu.
 
Habari wana JF,
Moja kwa moja kwenye mada, kama tujuavyo neno Gospel maana yake ni Habari njema kwa watu wote (kutokana na imani ya kikristo). Na kuna waimbaji wengi (hatuwaiti wasanii maana hamna usanii kwenye dini) wanaimba kama njia ya kumtumikia Mungu.Wapo wengi kama kina Bahati Bukuku, Rose Muhando,Christina Shusho n.k

Mwanzo nilikuwa nasita kupinga kuwa Goodluck gozbert sio muimbaji wa Injili ila ni mziki wake ni wa Bongo flavour tu. Hili linajidhirisha vyema kupitia nyimbo yake ya 'Nibadilishe' ambayo ndani yake mahadhi ya nyimbo na style za kucheza hazitofautiani na zile za kina Harmonise, Diamond, Burna Boy n.k. Hii inaniaminisha kuwa huyu si muimbaji wa gospel bali anafanya Bongo flavour kwa kivuli cha dini. Kama hujaona wimbo huo...Angalia kwenye link hapa chini....



Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu, mbona akina boni mwitege na rose mhando walikuw wanaweka watu wanacheza viduku na bado mlikuwa mnawachukulia waimba gospel?
Mbona goespel ya bonny mwaitege iko kama takeu style ya mziki wa mr nice?
Mbona rose mhando gospel yake ilikuwa kama sebene za wakongo?
Gospel inabadirika kama ilivyo kwa mziki mwingine maana gospel ya miaka ya 80 iko tofauti na gospel wanayoimba akina bahat bukuku na wengine.
Goodlucky anaimba habari njema
 
Back
Top Bottom