Goodluck Gozbert unaelekea wapi?

Goodluck Gozbert unaelekea wapi?

Ni ngumu sana kwa wakristo kumuelewa Godluck Gozbert kwenye huu wimbo.
Wanazuga kuwa hawapendi Uchezaji na staili ya mavazi kwenye video, lakini kiukweli wanachukia zaidi mashairi ya wimbo.
Mkristo sio mtu anaetaka kuiimba "Nibadilishe", yaani akiri mbele ya watu kuwa yeye ndo ana matatizo, ana dhambi? ni mchungaji gani anaweza upenda huo wimbo? yaani unataka Kakobe au Gwajima, au Nkone, aimbe Mungu Nibadilishe na kuconfess dhambi zake za sirini mbele ya watu? Maana hicho ndicho anachoimba dogo.
Laiti kama dogo angeimba "Mbadilishe" na akawa anafocus kwenye nafsi ya tatu, " Kwanza umenyoa denge, unapenda sana michezo ya nywele......., Omba Ubadilishwe......" Wakristo wengi wangeupenda, regardless ya michezo na mavasi, kwa kuwa wangeutumia kwenye hata ushuhudiaji, na kusemana, maana wanapenda kuwasema sana wale wanaowaona sio wakamilifu.
Yaani kwa maneno machache angeimba nafsi ya tatu, wimbo ungekuwa wa ushuhudiaji, na wakusengenyana, na ndizo wakristo wengi wanazipenda, ila kaimba nafsi ya kwanza, umekuwa wimbo wa confession, ambao wakristo hawapendi kuconfess mbele za watu.
mmmmh....! Najaribu kukuelewa ila hao akina nkone, kakobe wanatoka wapi..? Hv unafuatilia injili yao..? Au umeamua tu kubwabwaja....! Waweza ukawa sawa lakini hyo ni kwa mtu asiyelijua vizuri neno la mungu / mwenye wokovu wa kuigiza
 
mmmmh....! Najaribu kukuelewa ila hao akina nkone, kakobe wanatoka wapi..? Hv unafuatilia injili yao..? Au umeamua tu kubwabwaja....! Waweza ukawa sawa lakini hyo ni kwa mtu asiyelijua vizuri neno la mungu / mwenye wokovu wa kuigiza
At least I gat someone kaongea something nltaka kuongea, sijui kama anaelewa alichokiandika
 
mmmmh....! Najaribu kukuelewa ila hao akina nkone, kakobe wanatoka wapi..? Hv unafuatilia injili yao..? Au umeamua tu kubwabwaja....! Waweza ukawa sawa lakini hyo ni kwa mtu asiyelijua vizuri neno la mungu / mwenye wokovu wa kuigiza
Amini nakuambia, ni rahisi kwa wewe kusimama madhahabuni kukubali umekosa, kuliko wachungaji na maaskafu.

usijaribu kunielewa, nielewe, ni hivi Wimbo wa Godluck Gozbert, ili uupende, unataka ujiimbe wewe kuwa u mkosaji, na aina za dhambi alizoziimba, sio dhambi ambazo hard core christians watapenda kujinasbu nazo. japo ukweli wanaujua wao wenyewe,

ila angeimba nafsi ya tatu, anamuimba yule, au hata nafsi ya pili, wewe. ungekuwa ni number one song kwenye mikutano ya injili sasa hivi.
 
Wakuu habari

Hivi hii nyimbo mpya aliyoitoa Goodluck Gozbert ni ya dini au maana sio kwa maudhui Yale kwa upande wa video na audio pia
Mkuu naamini umepagawa na mapigo ya kimuziki ya wimbo ule, nakushauri jaribu kufuatilia kwa makini mashairi ya wimbo ule ule utagundua jamaa wala hajachepuka amebaki njia kuu. Kukariri ndiyo kunakupa taabu jipe Exposure ya kusikiliza nyimbo "MAKOMA" uone jinsi watu wanavyoimba nyimbo za Injili katika njia iliyoboreshwa. Ni katika harakati za kuyatakatifuza ya Dunia.
 
Waungwana Hebu Tuusikie Na Huu.. Halafu Tuseme Mahadhi Yake! Upo Kwenye Rap Version!!

Huu Hapa [emoji116]


 
Labda kuvaa mashati ya vitenge makubwa kama Bony mwaitege au mashat ya zambarau na suruali pana za samawati,kijani na udhurungi[emoji5][emoji4]
Umesahau suti ya rangi ya hudhurungi over size na mashati ya pinki
 
Agent wa shetani
Watakuja na ushawishi mdhani wanamuabudu Mungu wa kweli
' Kizazi hiki hakitapita hata yote yatatimia'
Kuna nini cha ushetani kwenye hiyo video? Nielimisheni tafadhali
 
Hv watanzania mna matatizo gan?,hv mmeusikiliza wimbo vzuri? Jamaa anazungumzia kuhusu maovu yake na anataka bwana ambadilishe tatizo liko wap,mavazi, kucheza kunahusiana na nn na kumuabudu mungu?huo ni wimbo wa dini pure na ni bonge moja la wimbo for sure tuache kukariri mlitaka avae suruali pana na mashati ya kitenge ndo mjue kaimba dini?
Ukiwa mlokole unatakiwa kuwa mshamba, hatujazoea jamani
 
Huo wimbo hauna maadili ya kidini, hakuna ubunifu wowote kiufupi ameingia Choo cha kike, hyo ni bongo fleva, achague kusuka au kunyoa kama anaimba dini aimbe kama ni bongo fleva aimbe bongo fleva, kipaji chake kipo kwenye dini ila Moyo wake unatamani bongo fleva, na hapa ndo kajionyesha rangi yake halisi , achague kimoja kuunganisha vyote atajipigiza kwenye Jiwe......
Umeongea Mkuu Slowly, wanaomshabikia ni wale wanaosumbuliwa na mapepo ya dunia, lazima wamshangilie kwani hawajui walitendalo, ni kweli anapotea, sasa hivi mtaona anaanza kunywa gongo, mimi niliwahi kuwatahadharisha watu niliokuwa naangalia nao album yake ya kwanza
 
Mashairi ya wimbo hayana shida hata kidogo, maana anaelezea Jinsi maisha anayoishi ambavyo hayampendezi Mungu (Hapa hakuna shida)

Mavazi aliyovaa binafsi pale mwanzo na sehem nyingine ya shooting hayana shida hata kidogo, maana yanaakisi maisha ya kijana ambaye mwenendo wa maisha yake hayampendezi Mungu (Hapa hakuna shida)

Uchezaji wa wacheza show wake, ni style tu ya kunogesha wimbo, na kuamua kutoka kivingine na kwa radha toafauti (Hapa hakuna shida)
Hatuhitaji kunogesha lolote panapokuja swala la kueneza Injili, hii sio Disco.
 
Back
Top Bottom