Ni ngumu sana kwa wakristo kumuelewa Godluck Gozbert kwenye huu wimbo.
Wanazuga kuwa hawapendi Uchezaji na staili ya mavazi kwenye video, lakini kiukweli wanachukia zaidi mashairi ya wimbo.
Mkristo sio mtu anaetaka kuiimba "Nibadilishe", yaani akiri mbele ya watu kuwa yeye ndo ana matatizo, ana dhambi? ni mchungaji gani anaweza upenda huo wimbo? yaani unataka Kakobe au Gwajima, au Nkone, aimbe Mungu Nibadilishe na kuconfess dhambi zake za sirini mbele ya watu? Maana hicho ndicho anachoimba dogo.
Laiti kama dogo angeimba "Mbadilishe" na akawa anafocus kwenye nafsi ya tatu, " Kwanza umenyoa denge, unapenda sana michezo ya nywele......., Omba Ubadilishwe......" Wakristo wengi wangeupenda, regardless ya michezo na mavasi, kwa kuwa wangeutumia kwenye hata ushuhudiaji, na kusemana, maana wanapenda kuwasema sana wale wanaowaona sio wakamilifu.
Yaani kwa maneno machache angeimba nafsi ya tatu, wimbo ungekuwa wa ushuhudiaji, na wakusengenyana, na ndizo wakristo wengi wanazipenda, ila kaimba nafsi ya kwanza, umekuwa wimbo wa confession, ambao wakristo hawapendi kuconfess mbele za watu.